Umefika wakati Tanganyika ijuvue gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umefika wakati Tanganyika ijuvue gamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Apr 12, 2011.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  katika kipindi hiki cha karibuni, tumeshuhudia mambo mengi, likiwamo la kuzungumzia na kuchangia muswada unaotarajiwa kupelekwa bungeni hivi karibuni kwa ajili ya kuweka ramani ya kutupeleka kwenye katiba mpya.

  pia tumeshuhudia chama tawala ambacho ndicho kilichohusika kwa kiasi kikubwa na muungano wetu, kikiwa katika harakati za kujivua gamba.

  sasa kwenye muswaada ambao unajadiliwa kuna mengi yamesemwa, na hasa kuhusu muungano wetu. wako wanaoona kuwa na uwakilishi sawa katika uundwaji wa katiba hii mpya sio sahihi kwa kuwa nchi moja ina watu wengi na eneo kubwa kuliko nyengine. kutokana na hoja hio wao wanaona ni kuwadhulumu wengi kwa kuamuliwa mambo yao na wachache.

  baada ya kutafakari nimegundua hoja ingekuwa hivi, kwa vile serikali ya jamhuri wa muungano ndani yake mna serikali ya tanganyika, sio sawa kwa wazanzibari kuwaamulia watanganyika mambo yao. maana wao hayawahusu, wao wana katiba yao na huko wanapanga mambo yao.

  sasa ili hili lisiwe kikwazo imefika wakati sasa tanganyika kujivua gamba na kubaki Tanganyika mbali na tanzania mbali, ili watanganyika waunde katiba yao kwa mujibu watakavyo, na baada ya hapo ndio tukae wazanzibari na watanganyika kuunda katiba ya jamhuri ya tanzania

  na nnaamini kama tanganyika ikijivua gamba matatizo mengi ya muungano yatapatiwa ufumbuzi.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaaaa nimelifurahia sana neno kujivua gamba nadhani msimu wake umeshafika litatumika kwa muda na baadae kupotea!!kwa hiyo mapendekezo yako tuwe na serikali 3?
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ndo maana yake, iwe serikali ya tanganyika yenye mamlaka kwa mambo ya tanganyika. na tuunde serikali ndogo tu kwa ajili ya yale tunayoshirikiana baina ya tanganyika na zanzibar

  tuwahimize watanganyika kujivua gamba
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haya tuambie tukivua hilo "gamba la Muungano" litatusaidiaje kupambana na umaskini, ufisadi, nk? Unapowataja Wazanzibari usisahau kwamba na wao ni Watanzania, kwa hiyo wanapochangia hoja kuhusu Katiba mpya wako sahihi kabisa! Roho yako ya ubaguzi itaiangamiza nafsi yako!
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Roho ya ubaguzi itawamaliza!
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hamna sio roho ya ubaguzi, bali ukiangalia Katiba ya Jamhuri vifungu vingi vinaigusa Tanganyika as pe see so hakuna haja ya kuwa na timu ya watu sawa wakati wengine kuna mambo hayawagusi.

  ndio nikatoa ushauri wa kujivua gamba ili kuwe na uhuru tosha kwa tanganyika kuangalia vipao mbele vya taifa lao, kisha tukae pamoja kama watanzania kuangalia ni kipi na kipi tushirikiane


  tukiangalia hili suali kwa umakini wake utaona faida zake, mfano tutapunguza marejeo ya mambo kama vile kuwa na wizara ya muungano mbali za tanganyika mbali, kupunguza idadi ya wabunge kwa zanzibar kuwa na wabunge 70 wote wa nn, nnnadhani tukijipanga bunge lote la muungano linaweza kuwa na watu 50 wanatosha
   
 7. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hili wazo mnaliangaliaje ?
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,766
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mtu wa pwani nakubaliana na wewe tanganyika yangu ije na iwe na katiba yake ndipo twende kwenye muungano wakuu!
   
 9. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Hili wazo lako nila msingi sana... kuna mambo yasiyowahusu kabisa... tukae sisi kama sisi tuyatengeneze kwa jinsi tunavyotaka then ndo tuungane kuongelea mambo ya muungano!!
   
 10. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hilo la Tanganyika analisemea sana Mtikila na watu wakamwona kama mropokaji. Ukweli ndio huo kwamba Tanganyika inapaswa kuwapo ili muungano unaosemwa upate kuonekana. Sasa Muungano wa Tanzania ni sawa na kufungishana ndoa kwa nguvu kati ya ndoa ya mtu aliye hai na marehemu. Yaani tumia lugha zote ukweli ndio huo. Ndio maana wakubwa wana kigugumizi kutetea muungano huo wakati Zanzibar wanadai wao wanamezwa lakini upande mwingine wapemba wamejaa kila kona ya Tanganyika wakiporomosha maghorofa, wenyeji wakibeba zege tu vifua wazi ati ndio muungano halisi. Mbara nenda visiwaninkama utapewa hata nafasi ya kuchagua mjumbe wa nyumba kumi mtaani kwako ulikopanga.

  Ni kazi ngumu sana kuutetea ujinga watu wakakuelewa, isipokuwa ukiwa mbabe watu waitikie kibwagizo tu ili waishi hata kama ni kwa hofu.
   
 11. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono tz kujivua gamba na pia nakubali kuwa wazenj ni watz wa kuandikishwa kwani wana nchi yao ya asili, labda niliweke wazi hili kuwa mimi sio shabiki wa muungano watz kwa jinsi ulivyo sasa na jinsi ulivokuwa tangu mwanzo.. naamini kuwa watanganyika wamekosewa heshima yao kwa kuiua nchi yao na kwa hili Nyerere alifanya kosa.
  Kujivua kwa gamba ninaoukubali mimi kwa tz ni kuua muungano uliopo halafu turudi kwa wanacnhi tuwaulize kama wanautaka muungano na wanataka muungano wa namna gani..
  Takuja tz imejivua gamba vinginevo litatutesa, wazenj wanasema katba ya tanzania ndo inafanyiwa marekebisho na wametamka kuwa wanataka talaka na wamewataka wenzao warudi zenj ili wasaidiane kudai talaka yao.. yani tayari wao wanajiona waliolewa kwenye muungano. sasa yanini kung'ang'ania? sijui kama ni kutikisa kiberiti
  huo sio ubaguz. mimi naamini ktk kusikiliza maoni ya watu wenyewe
   
 12. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Tuvunje muungano tukutane kule ktk EAF, hakuna haja ya kuwa na muungano ndani ya muungano wa EAF. Hata tukiwa na serikali tatu bado tutaendelea kupingana tu makao makuu ya huo muungano yawe wapi.

  Na bado tutaendelea kupingana tu ktk suala zima la uchumi na uwakirishi ktk serikali hiyo. Maana ninavyofahamu mimi wazanzibar watataka uwakirishi wa nusu kwa nusu ktk serikali hiyo na bajeti ya hiyo serikali aghalamiwe na Tanganyika kwa 99.9%. Maana sidhani na wala sitaki kuamini ya kwamba bajeti ya hiyo serikali itachangiwa nusu kwa nusu.

  Cha mhimu na suluhu iliyo na tija na mwafaka kwa kizazi hiki ni kuachana na huu muungano, tuunganishwe tu na EAF, kwa maana EAF inakidhi mahitaji ya mwananchi wa pande zote, kwa ajira, makazi nk.

  Muungano uvunjwe ni hasara tupu kila pande inavuna ktk huu muungano uchwara.
   
 13. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,188
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  Serkali3 hazina tija, kama uchumba muda umekwisha kilicho baki tufunge ndoa ya kweli ambayo zenj ife kama tg ilivyo kufa tuwe na serkali1 ya TZ TU.
  Kama si hivyo muungano ufe tu.
   
Loading...