OK,
Vipi kama nilitaka kuoa, na nikatoa kauli kwamba nataka kuoa, lakini katika kipindi cha uchumba, au hata siku ya arusi, nikagundua kwamba huyu mwanamke si wife material.Mimi sikudanganya na wala sikuwa na nia mbaya, ila nimepata information mpya au simply nimebadilisha mawazo kuhusu kuoa (ever heard of cold feet or getting the marriage creeps?), sitaki kuoa tena, lakini sijawahi kudanganya kwa kudhamiria na wala sidanganyi, nabadilisha mawazo tu. Hizi sheria zinataka kunichukulia uhuru wangu wa kubadilisha mawazo?
Hapo mtanifanyaje? Mtahakikishaje kwamba kubadili mawazo hapa ni kudanganya na hapa ni mtu ameamua kubadili mawazo.
Hizi sheria si za kitalibani zitakazomuondolea mtu hata uhuru wa kubadilisha mawazo? Watu wanabadilisha mawazo hata dakika ya mwisho na sijawahi kusikia wakiletewa mashtaka.
Ina maana mnataka kuuchukua uhuru wa mtu kubadilisha mawazo altareni? Mbona hata kanisa linatambua kwamba mtu ana uhuru wa kubadili mawazo hata dakika ya mwisho na ndiyo maana hata padre anayefungisha ndoa huuliza maharusi hata dakika ya mwisho wakiwa altareni?
Kama ndoa inaweza kuvunjwa baada ya kufungwa kwa talaka, kwa nini mipango ya kufunga ndoa isiweze kuahirishwa wakati wowote kabla ya ndoa?
This does not make sense and goes against my libertarian strains, not that I would ever dream of getting married but the precedent set here is dangerous.
Tukianza na kulazimishana ndoa, whats next? Tutalazimisha watu wote waliojiandikisha kupiga kura wapige kura? Whats the difference?