gogo la shamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 6,669
- 2,165
katika sifa za kikwete umesahahu kumfunga Babu seya na watoto wake maisha
MAZURI ya Kikwete ambayo hayajawahi kufanywa na marais waliomtangulia HAYA HAPA
Katika kipindi cha Kikwete masuala yafuatayo lazima tumpe Credit kwani baadhi yamefanywa na JK wa mwanzo tu na hayakufanywa na Mwinyi wala Mkapa.
1. Ujenzi wa Sekondari za Kata ni maamuzi sahihi ingawa yana changamoto zake zinazoweza kutatuliwa na watakaomfuatia, lakini hapa JK ametumia madaraka yake vizuri
2. Ameendelea na uendelezaji wa Miradi ya Barabara, suala lililoanza kujitokea wakati wa awamu ya 3, JK ameendelea nalo suala hilo kwa kasi kubwa na kwa kipindi chote
3. Daraja Kigamboni, Malagarasi na Kilombero ni miongoni mwa mambo yatakayokumbukwa forever
4. Ongezeko la Taasisi za Elimu ya Juu limefanyika vizuri sana katika awamu ya Kikwete, mbali na UDOM lakini taasisi na vyuo vingi vimeimarishwa, kupandishwa hadhi na vyuo vingi binafsi vimeanziswa. Kwa sasa Taifa haliko tena na dhana ya UDII, Mzumbe na SUA. Aidha ari na moyo wa watanzania kulipia huduma za elimu umeongezeka.
5. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ajira ukilinganisha na awamu mbili zilizomtangulia. Mkapa aliendesha Serikali nyembamba, suala ambalo ni zuri lakini lina changamoto zake kwa wale waliokuwepo wameliona hata akapewa sifa ya mzee wa "ukapa"
6. Mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwa lengo la kutatua kero ya Umeme ni hatua nzuri ambayo haijawahi kufanywa katika awamu ya 2 na ya Tatu (Vyanzo vya Nishati)
7. Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Chuma (Kule Liganga?) ambao maandalizi ya ujenzi wake yamekamilika ni hatua nzuri ili kuvutia au kuanzisha uwekezaji wa zana za Chuma pamoja na Viwanda vikubwa.
8. Hatua ya Kujenga Bandari mpya eneo la Bagamoyo yenye hadhi ya 4th Generation ni tukio litakalokumbukwa na vizazi Dahri vijavyo.
9. Hatua ya Utekelezaji wa mradi wa DRT ambao ulikuwepo miaka mingi pia ni miongoni mwa mazuri yaliyotendeka katika awamu ya JK
10. Zoezi la kutambua na kuwarudisha kwao wahamiaji haramu pia ni zoezi zuri ambalo bila shaka halijawahi kufanywa katika uongozi wa awamu nyinginezo kwa kiwango na utashi wa namna hiyo
11. Kitendo cha utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya Taifa ni credit kubwa kwa JK ambao hakuna sababu za wazi kwanini nchi imekaa miaka 50 pasipo na vitambulisho vya uraia kwa wakazi wake na raia wake
12. Ameendelea kuiweka Tanzania kwenye mahusiano mazuri kimataifa hususan SADC, UN na nyanja nyingine za Kitaifa. Ukiacha EAC ambayo sababu za kuzorota kwake ziko wazi, lakini maeneo mengine ame-play well.
picha; maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni eneo la kurasini jijini dsm. ujenzi ulikuwa asilimia 47 mwezi july
Ameongeza Ma-brigedia Generals wengi katika historia ya Tanzania...

Ila watanzania wasirudie kosa tena kuchagua ccm..itakula kwao mno
katika hii Lizaboni hawezi kukujibu.Ameonyesha "ubinadamu" kwa kuwasamehe wauza madawa ya kulevya ili waendelee na biashara licha ya kusema anawajua maana ndio wafadhili wa chama "chetu"
Kwa huruma kabisa na utu uliotukuka aliwaambia wale walioiba fedha za EPA warudishe tuu maana ni ndugu zetu na Tanzania ni moja.
Majangili kawaonya kuwa hata kama wanaua Tembo basi sio vizuri wakawaua sana maana lazima wabaki wengine ili wazaliane na biashara isife kwa kuwa anawafahamu wahusika.
Kaamua hayo ya IPTL ayaache tuu maana hao waliokwapua ni watendaji wake wakuu ya nini kuumbuana kwa Bil 400 wakati katika tembeatembea yake akiomba wafadhili wamejitolea matrilioni?
Mazuri ni mengi sana kwa kweli.