Roga Roga
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 655
- 500
Kwa wale wapenda mabadiliko hapa Tanzania sasa ni wakati wa kuanza kufurahi na kusherekea kwani muda uliobaki kwa serikali hii ya kijeshi imalize muda wake wa miaka 10 ambayo iliingia madarakani 2005 na ita-expiry mwaka 2015.
Ninaiita serikali ya mpito au ya kijeshi kutokana na mambo kadhaa yaliyotokea katika kipindi hichi na kuzimwa kwa nguvu kubwa ya jeshi la polisi au la wananchi na kuacha sintofahamu kubwa katika jamii, mfano wa matukio hayo ni
1. Sakata la gesi mtwara ambalo lilishuhudia nguvu kubwa ya kijeshi ikitumika na kugharimu maisha ya watu kadhaa, huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu, yatima na kukosa nyumba za kuishi.
2. Mgomo wa madaktari, ambao ilishuhudia wagonjwa wakipoteza maisha sehemu mbalimbali nchini na mgomo huo ulizimwa kwa Dkt Ulimboka kutekwa na kufanyiwa ukatili wa kutisha na watu wa usalama wa Taifa (kwa mjibu wa M.w.a.n.a.h.a.l.i.si)
3. Kuingiliwa uhuru wa vyombo vya habari pale tu vilipoandika ubaya au kuikosoa serikali iliyomadarakani. Mfano ni kufungiwa kwa magazeti kama Mwananchi na Mtanzania.
4. Kuuwawa na kuwadhuru waandishi wa habari, mfano Said Kubenea kumwagiwa tindi kali na Daudi Mwangosi kuuawa huku RPC husika akipandishwa cheo.
5. Jeshi la polisi kugeuka na kufanya kazi za siasa kama moja ya vitengo muhimu pale Lumumba. Mfano ni unyanyasaji wa viongozi wa Upinzani kama Halima Mdee, Wilfred Lwakatale kufunguliwa kesi ya Ugaidi
6. Kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini sehemu mbalimbali huku wahusika wakiwa hawajatiwa mbaloni mpaka leo
7. Kuuwawa watu mbalimbali katika mikutano ya siasa mfano viwanja vya Soweto, muuza magazeti Morogoro na maandamano ya chadema 2011
8. Kuuwawa, kuumizwa, kubakwa, kupewa vilema vya kudumu raia mbalimbali katika kile kilichoitwa oparasheni tokomeza ujangili 2013
9. Kuvurugwa kwa mchakato wa katiba huku nguvu kubwa ikitumika katika hafra ya Sita kumkabidhi Rais Kikwete katiba iliyopendekezwa.
10. Vifo mbalimbali katika chaguzi ndogo na uchaguzi mkuu wa 2010 huku wahusika wakifumbia macho tatizo hilo mfano Arumeru Mashariki na Igunga
11. Baraza la mawaziri kuvunjika kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili huku historia ikiandikwa zaidi kwa idadi kubwa ya mawaziri kujiuzuru katika utawala wa awamu hii.
12. Elimu kuporomoka kwa kiasi kikubwa sana.
Ningeeleza mengi lakini nawaachia mengine mjazie