Umeambiwa, Lowassa ni muongo, tapeli, fisadi, na bado una mshabikia! Una matatizo makubwa

Hatumtukani mzee, ila mzee anatushangaza makengeza ameyapata lini? Alikuwa na orodha ya mafisadi 11 lakini sasa orodha yake anamwona mmoja tu, hata huyo mmoja hajampeleka mahakamani kama mtuhumiwa alivyoomba mwenyewe!
Sasa mtu anayelazimisha makengeza wakati hana lengo lake ni nini?
Kama ana ubavu aende mahakamani!

Hao wengine wote hawagombei urais na hata kuwashughulikia ni rahisi tu maana JM anakuja na dawa yao lkn fisadi hawezi washughulikia wenzake zaidi ya kuwaalika kufisadi zaidi. Vilevile Slaa alikuwa katibu mkuu wa cdm iliyokuwa alama ya mapambano ya ufisadi nchii hii, imemshangaza kuwaleta kushika chama.
 
Mashabiki wa magamba kwa kujifanya wana makengeza hawajambo! Watakuambia hapakuwepo na mafuriko ya watu pale jangwani siku ya uzinduzi wa kampeni ya chadema na ukawa eti picha live kwenye TV ni za kutengeneza na picha kwenye magazeti ni za kutengeneza! Sasa huyu hapa naye analazimisha makengeza na kusema wanaomponda babu slaa na uongo wake hawafiki kumi! Pole!
Na hii ni karata ya mwisho ya magamba kujaribu kuzuia mafuriko kwa mkono na karata hii imeshindwa vibaya kama ile ya lipumbi!

October 25 jibu litapatikana
 
Kama umesikia maelezo ya Slaa basi Lisu katufumbua kitu kingine tulichokuwa tunajiuliza siku nyingi. Slaa kaweka wazi hana tatizo na Mbowe na kwamba amemjengea mpaka nyumba maana yeye Slaa hana hela. Mwansheria tena wa chama anasema Slaa anaishi kwenye nyumba ya chama so CHADEMA=MBOWE kuna chama hapo? Ndiyo maana anauwezo hata kuchagua mgombea bila kufuata taratibu za kidemokrasia...du hii ni NGO

Too late, train ikiondoka haisimami ikisimama inashusha na kupakia. Slaa ameshushwa na Sumaye kapanda, safari inaendelea
 
Leo tumesikia mbivu na mbichi toka kwa Dr Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Tumesikia jinsi alivyoingia uongozini CHADEMA kwa nguvu yake ya pesa, na jinsi anvyobebwa na watu kama Rostam Aziz.
Tumesikia jinsi Dr Slaa alivyo fungashiwa rushwa ya tshs 500 million ili akubali kumsafisha fisadi.

Tumesikia jinsi Richmond ilivyo bado mbichi kabisa.

Sasa kijana anaye mshabikia fisadi, mwizi na muongo tumwelewe vipi?

Lazima mtu huyo ana matatizo makubwa.

Mimi nina matatizo makubwa ya kuipenda Chadema na Ukawa kwa ujumla. Nimekunywa doz moja ya Lipum lakini bado.sasa nimeanzishiwa ya Dr sla Rich leo ndo matatizo yamezidi kabisa.
 
Yethu wangu maria na yosefu pamoja na maelezo mazuri bado watu wanang'ang'ania makapi? Kweli sikio la kufa halisikii dawa

Ndio mjue kuwa watz hatudanganyiki tena. Mlidhani mkimtumia dr ndio mtapunguza kasi ya mafuriko ya EL, yaani ndio kwanza mafuriko yatazidi mara dufu kuanzia mikutano ya leo. Kwa hili nimeamini maneno ya ZZK kuwa usimwamini mwanasiasa yeyote. Kama kweli sisiemu wamegharimia press conference ya jana na gharama za kurusha matangazo kwenye vituo kadhaa vya television na radio basi hatuna cha kujadili kuhusu dr. Itakuwa ni usaliti wa karne. Wanachadema tujipe pole sana kwa kuwa na katibu mkuu mamluki kwa kipindi chote hicho. Tunamshukuru Mungu kwa jambo hili lililotokea. Kwani tusingeyajua haya. Kweli safari hii ni ya uhakika mpaka Ikulu bila mamluki na wasaliti kama dr na Prof lip
 
mkeo akiwa na mapungufu huwezi kumsema nje unatakiwa umseme ndani mamvi alivo kua huko kwann hamkumuita fisadi alivo kuja huku mnasema fisadi
 
Leo tumesikia mbivu na mbichi toka kwa Dr Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Tumesikia jinsi alivyoingia uongozini CHADEMA kwa nguvu yake ya pesa, na jinsi anvyobebwa na watu kama Rostam Aziz.
Tumesikia jinsi Dr Slaa alivyo fungashiwa rushwa ya tshs 500 million ili akubali kumsafisha fisadi.

Tumesikia jinsi Richmond ilivyo bado mbichi kabisa.

Sasa kijana anaye mshabikia fisadi, mwizi na muongo tumwelewe vipi?

Lazima mtu huyo ana matatizo makubwa.

Kwa hiyo tumchague nani ambaye ni msafi?
 
CCM ilikuwa imebakiza risasi moja tu katika bunduki yao ya kuimaliza UKAWA. Risasi hiyo ni hotuba mbovu,isiyokuwa na ukweli na ya kumezeshwa ya Dr.Slaa kuiponda UKAWA na Lowassa. Kutokana na kuwa Lowassa ni mpango mkubwa wa MUNGU kuikomboa Tanzania kutoka katika kundi hatari la CCM Dr Slaa ameweweseka na kujikuta akipiga risasi katika upande wake yeye na watu wake hao waliomtuma,kumlipia hotel na ndege ya kukodi kutoka Afrika ya Kusini,na kwenda Marekani ambapo ataendeleza propaganda za siasa nyeusi na chafu.Hatojali tena maslahi mapana ya Wananchi wa Tanzania.Amelipua bomu na ametokomea kukwepa madhara yake huku watu wa upande wake wakiangamia.TUNASONGA MBELE!!
 
kwa nini Lowasa, kwenu sasa, ndiyo anaonekana ni fisadi? Poleni Lowasa is our next president-even with the on going campaign to deface him.. we will never retreat, waver ..... our resolve is unshakable.
 
Leo tumesikia mbivu na mbichi toka kwa Dr Slaa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Tumesikia jinsi alivyoingia uongozini CHADEMA kwa nguvu yake ya pesa, na jinsi anvyobebwa na watu kama Rostam Aziz.
Tumesikia jinsi Dr Slaa alivyo fungashiwa rushwa ya tshs 500 million ili akubali kumsafisha fisadi.

Tumesikia jinsi Richmond ilivyo bado mbichi kabisa.

Sasa kijana anaye mshabikia fisadi, mwizi na muongo tumwelewe vipi?

Lazima mtu huyo ana matatizo makubwa.

Yoote hayo "mmesikia" wala Hamna ushahidi, hiyo ni biashara ya kawaida Siku hizi kuhongwa 500m/- ili umchafue mtu kwa fitna kwa mfano Lowasa kajiunga juzi tu na UKAWA na hajafanya ufisadi wowote tangu ajiunge na chadema lakini anavyopambwa na hadithi utadhani kakaa miaka 30 cdm.
 
CCM ilikuwa imebakiza risasi moja tu katika bunduki yao ya kuimaliza UKAWA. Risasi hiyo ni hotuba mbovu,isiyokuwa na ukweli na ya kumezeshwa ya Dr.Slaa kuiponda UKAWA na Lowassa. Kutokana na kuwa Lowassa ni mpango mkubwa wa MUNGU kuikomboa Tanzania kutoka katika kundi hatari la CCM Dr Slaa ameweweseka na kujikuta akipiga risasi katika upande wake yeye na watu wake hao waliomtuma,kumlipia hotel na ndege ya kukodi kutoka Afrika ya Kusini,na kwenda Marekani ambapo ataendeleza propaganda za siasa nyeusi na chafu.Hatojali tena maslahi mapana ya Wananchi wa Tanzania.Amelipua bomu na ametokomea kukwepa madhara yake huku watu wa upande wake wakiangamia.TUNASONGA MBELE!!

Wewe unasema ni mbovu lakini sisi wanaharakati tumeielewa sana tu!
 
Sisimu kuna yupi ss ambaye hana kashfa na shutuma?mfumo sisimu ndo tatizo,lazima kikafie mbali hiki chama
 
Back
Top Bottom