Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Katika mfumo huru na rafiki wa maisha kuheshimu, kuruhusu, kukubali na kusikiliza maoni ya mtu ni nguzo ya ueledi, ustahimilivu, uungwana na ukomavu.
Hakuna mahali palipostaarabika duniani ambapo watu wamefungiwa milango na madirisha ya kutoa maoni na mawazo yao halafu jamii ikapiga hatua. Libya ilikuwa nchi tajiri kupindukia. Raia walipewa kila walichohitaji kwasababu serikali ilidhibiti kila kitu na ilikuwa na fedha za kufanya chochote lakini kilichomtokea Ghadafi ni matokeo ya raia kuchoshwa na ukandamizwaji wa hali ya juu. Hata kama ubeberu wa wamarekani ndio uliomng'oa Ghadafi, ukweli ni kwamba raia waliokuwa wamekandamizwa kwa miaka lukuki walipata ahueni na wengi wao waliunga mkono ubeberu ule japo kwa maslahi tofauti.
Katika siasa za Tanzania leo tunashangilia kuingia katika enzi ya tofauti ambapo wala nchi wanaadhibiwa na angalau ishara za kurejesha nidhamu ya uwajibikaji zinaonekana. Hali hii inatoa matumaini japo yanafifishwa na kinachoendelea nyuma ya pazia na ambacho kadri siku zinavyokwenda kinajidhihirisha peupe.
Ni hali ya kuzuia kwa nguvu zote watu na taasisi kuchambua, kujadili na kutoa mawazo mbadala dhidi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano. Katika mazingira tuliyonayo haiingii akilini kwamba serikali makini kama ya Dr. Magufuli itaogopa mijadala, kukosolewa na kushauriwa. Kuzuiwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya mijadala bungeni na kupigwa marufuku mikutano ya vyama vya upinzani nchini ni kielelezo cha serikali kudhihirisha udhaifu wake katika kupokea na kuhimili mawazo mbadala.
Kuhusu bunge sihitaji kulisema tena kwasababu limesemwa sana. Najiuliza i wapi nia njema ya kuviacha vyama vya siasa viendelee na wajibu wao wa kisiasa? Vyama hivi vimesajiliwa kufanya kazi za kisiasa.
Unapovizuia vyama kukutana na wanachama wake mikutanoni unatuma ujumbe kwa taifa kwamba hakuhitajiki mawazo mbadala. Hii ni kansa ya kuliua taifa. Watawala jifunzeni kwenye historia. Tunajenga kesho yetu kwa tunachokipanda leo.