Umasikini wa Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umasikini wa Afrika

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by butogwa, Jul 17, 2011.

 1. b

  butogwa Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 34
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nchi za kiarabu ni tajiri kwa ajiri ya mafuta na gas. Madini,mafuta na gas vya africa vinamnufaisha nani?
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Kweli hujui vinamnufaisha nani!
   
 3. Kelema

  Kelema Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zinawanufaisha wachache waliochungulia line mapema. Lakini yote hii ni kwa sababu ya ubinafsi uliokithiri. Tanzania ni nchi tajiri ajabu!!!! Fikiria nchi kama Burundi na Rwanda, hazina bandari, zinategemea Tanzania kupitisha mizigo yao, na zinalipa. Lakini kimaendeleo ziko mbele kuliko Tanzania.

  Fikiria madini tuliyonayo, mbuga zetu za wanyama, n.k. Hakika umaskini unasababishwa na wachache tu. Kama tungekuwa na umoja, tungewang'oa hao (sababu wanajulikana) kisha tuwapate waadilifu. SWALI LANGU NI: Je, hao waadilifu watakuwepo? Je, hawaingia kwenye mtindo ule ule?? Tutafakari.
   
 4. khayanda

  khayanda JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Umasikini unasababishwa na sisi wenyewe tunaowaweka na kuwachekea viongozi wanatuchome nyama wakija kutulaghai. Tunawasganilia kwa ari na nguvu zaidi wao wakila nchi hii kwa kasi zaidi.
  Tukiamua hatutakuwa masikini. wewe, mimi, na mwingine na mwingine tuseme wote kwa moyo wa dhati, kwamba basi inatosha na tubadilike sasa.
  Tuukatae utawal mbovu, tuukemee uovu wote na matendo yao ya kidhalimu ndipo tutabaki slama.
  Sasa hivi hata wale tunaowajua ni wezi wameishaanza kujiandaa kuingia ikulu awamu ijayo, wakituchomea nyama tutawakubali na kuwaruhusu wapanue midomo yao kuendelea kujilambia asali yetu bila huruma.
  Tuseme BASI INATOSHA, TUKATE SHAURI ILI TUBAKI SALAMA. Tusiwe kama wabunge wetu sijui wanamuwakilisha nani, utakuta mbunge anaanza kuchangia hoja kwa kushukuru tuliomuweka pale, halafu analalamika toka na kuhuzunika jinsi serikali au waziri fulani anavyotutenda, cha AJABU MWISHO WA YOTE UTASIKIA Naunga hoja kwa asilimia 200, Pumbafu sana hawa..... MUngu awahukumu kwa wanayotutendea.
  Sasa wamejigawa kuwa wapo makundi matatu.1= Wabunge wanaofikiri kwa Matumbo, 2= Wabunge wanafikiri kwa vichwa na 3= wabunge wakambi ya upinzani- Hatuponi hata kidogo, tumekwisha kabisa
   
 5. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Tukiamua kabisa kwa dhati tutafaidi utajiri wetu lakini kwa mtindo huu wa kuiba kila mtu hatutasogea mpaka Yesu aje
   
 6. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  hivi tukiamua kuung'oa uongozi kwa nguvu ya uma,je ni jeshi ndilo litakaloongoza au ni nani atakayeiongoza Tanzania yetu mpya?
   
 7. Kelema

  Kelema Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wanaomwamini Mungu na hata ambao hawana uhakika juu ya Mungu, tafadhali soma kwenye Biblia, Neno loa Mungu, Danieli 2:44.
  Mwenyezi Mungu atakapoisimamisha Serikali yake duniani, ndio mwisho wa matatizo yote kwetu na kwa nchi zote duniani. Kwa sasa, tumwombe atupe hekima, tuchague viongozi wenye angalau uchungu na nchi, k.m. Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere. Nao wanaweza kumalizwam kama Sokoine.
   
Loading...