Umasikini Ngara wamtisha Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umasikini Ngara wamtisha Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 10, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Umasikini Ngara wamtisha Pinda Wednesday, 09 March 2011 20:31 0diggsdigg

  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda

  Phinias Bashaya,Ngara

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amezitaka halmashauri za wilaya nchini, kuharakisha 
mipango ya upimaji wa vijiji na kuwasaidia wananchi, kuendesha kilimo chenye tija 
kama njia ya kuwakomboa dhidi ya umasikini wa kipato.

  
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Ngara juzi, Waziri mkuu alielezea kusikitishwa kwake juu ya kukithiri kwa kiwango cha umasikini, huku viongozi wakishindwa 
kuwasidia wananchi kutumia fursa zilizopo, kujiendeleza.

  Kwa mujibu wa Pinda, fursa hizo ni pamoja na matumizi bora ya ardhi kwa shughuli za kilimo.

  
Alisema halmashauri za wilaya nchini, lazima zitoe kipaumbele katika upimaji wa vijiji 
na kwamba kufanya hivyo, mipango ya halmashauri, itakuwa imetafsiriwa kwa vitendo, vitakavyosaidia kubadili maisha ya 
wananchi.

  
Baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Salumu Nyakonji, Pinda 
alisema mazingira aliyoyaona kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kumubuga, katika Kata ya 
Mulusagamba, yalitoa tafsiri halisi ya kiwango cha umasikini kwa wananchi.

  
"Wanafunzi niliowaona hali zao ni kielelezo cha umasikini katika familia 
wanazotoka, halmashauri zina mawazo mazuri ambayo hayajatafsiriwa kwa vitendo ili 
kubadili maisha ya wananchi, kuna fursa za ardhi, maji na mifugo wakisaidiwa 
wanaweza kujilisha na kuwa na kipato cha kutosha,"alisema Pinda.

  
Waziri mkuu pia alionyesha kutoridhishwa kwake kuhusu halmashauri za 
wilaya, kujivunia ukusanyaji mkubwa wa mapato huku makusanyo ya mapato hayo yakishindwa kuonekana katika kubadili maisha ya wananchi.
  
Alisema wastani wa pato la wananchi katika wilaya hiyo yenye kaya 
50,000 uko chini mno ikilinganishwa na fursa zilizopo.

  
Akiwa wilayani Ngara, Pinda pia alifungua Zahanati ya Kumubuga, Shule ya Sekondari Kibogora na kuhutubia mkutano wa 
hadhara, katika eneo la Mulusagamba.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Pinda anaishi Tanzania ipi mpaka aende Ngara ndiyo atishike na umaskini wa kutisha wa Watanzania? Mbona umaskini wa kutisha umewakumba Watanzania walio wengi katika kila kona ya nchi yetu? Analaumu Halmashauri za Wilaya je Serikali imefanya yepi katika kupunguza kero mbali mbali za Wananchi ikiwemo umaskini wa kutisha? Kwa maoni yangu huyu naye ni msanii wa hali ya juu anataka kulaumu Halmashauri za Wilaya wakati Serikali yake inafanya madudu makubwa zaidi lakini hayaoni!!!!!
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Inakatisha tamaa, Inatia uchungu, Inatia aibu, kiongozi mwingine aishiye masaki anapokataa maandamano ya CDM wanaotoa hoja mbali mbali za kumsaidia mwananchi. Lakini mwisho wa siku, inatupa moyo zaidi wa kuendeleza mapambano dhidi ya viongozi wetu wanaojiona wao ndo wenye haki ya kuendelea kuongoza hata kama fikra zao hazileti wala kusaidia kuleta uhalisia wa maisha ya mtanzania kutokana na rasilimali tulizonazo.

  Its time to work up and keep fighting and protect our nation against the New blalk colonial masters, who don't care about their neighbours, about the lives of the people! they care about Ndiyo Mzee and so on.
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ajalia
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Anashangaa nini wakati CCM ndio imewafikisha watanzania hapo, huyu mung'amba nae amezidisha :blah::blah:
   
 6. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hata kule Rukwa au Katavi anakotoka hajaona umaskini wa kutupwa?
   
 7. Ontuzu

  Ontuzu Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Ni katika kuzima moto ule wa CDM nyanda za juu kaskazini, sasa serikali ndio imeamka na kuanza utendaji kwa lugha safi tunaita 'zimamoto'. Pinda alikuwa wapi kutembelea wilaya hii awamu ya kwanza na kujua kama wananchi wake ni maskini. Watafute ufumbuzi wa haraka, ni dhahiri kuwa CDM sasa inaongoza nchi
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kama yeye pia analia na kusikitika basi hatuna kiongozi! Kwani huko ngara ndo amegundua umasikini wa watanzania? Their inaction in fighting poverty while condoning embezlement just increases umasikini!
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu mzee manafiki sana..sipendi haa kumsikia akiongea mie ..kila kitu anajifanya kushangaa wakati yeye ndo waziri mkuu..watu wengine bana wanataka tutukane humu tupigwe BAN
   
 10. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwani anayosema yana tofauti gani na yanayosemwa na cdm, au anataka kusababisha uvunjifu wa amani?
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Huyu si nmtoto wa mkulima, familia yao wanamiliki ekali si zaidi ya 20 na wanazolima si zaidi ya ekali 6 leo anajiita mtoto wa mkulima ? hayumo kwenye orodha ya wakulima, kwao wasukuma wanalima zaidi ya ekali 300 kwa familia moja na ndiyo maana anawachukia wasukuma.Anashangaa nini wakati pale mpanda watu wanaomiliki nyumba za bati ni wageni wa kuja na si wenyeji .Kwao wamepigika kinoma.Hiloooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Eti anashangaa mapato makubwa lakini hakuna chochote,hivi serikali kuu nayo si ndio vivyo hivyo..mdogo anaiga kwa mkubwa..
   
 13. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwani anashangaa nini hali halisi alikuwa haijui?
   
 14. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ni bora hata hao wa Ngara wa kule kwake Rukwa hajawaona? eti amesikitishwa na umaskini? statement ya kinafiki inanikumbusha lile shairi la "BUILDING THE NATION"
   
Loading...