Umasikini mkali: Mwenyekiti wa Kijiji avaa shati lililochanika, January Makamba avua lake na kumpa

Sasa Makamba alitoa wapi shati jingine au anatembea na mawili
Hauoni hata habari kwa picha,tazama hyuma ya Mh,Makamba kuna mtu na bila shaka mtu huyo ni driver au msaidizi Mh,Makamba inaonysha alifungua buti la gari na inaonyesha alitoa nguo kwenye bag la Mh kisha kumkabidhi huyo m/kiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilidhania kavua lake na yeye Kubaki na vest tu kumbe katoa sandukuni kwenye gari lake... rubbish news Trump husema "Wrong"


Ati na kwamba anampa na kumpiga picha na kumtangaza, imani zetu hafifu sana, sijui inamgharimu nini angempa kwa siri kama maandiko yasemavyo,

Tunawatengenezea mazingira duni ya maisha ili tuwape mashati watuone wema kumbe awali tuliwahujumu
 
Na hivyo vibanda vinavyomzunguka je?
Wasaidieni watanzania waweze kupata kipato
cha halali ili watoke kwenye umasikini;
 
Katika hali inayoonyesha umasikini mkali unalikabili taifa,Mwenyekiti wa Kijiji huko Chalinze alikutana na Waziri January Makamba hali ya kuwa shati lake limechanikachanika

Mwenyekiti huyo aliyesifiwa na Waziri Makamba kuwa ni mtunza mazingira mzuri,aligusa imani NA huruma ya Waziri January Makamba ambaye alilazimika kumpa shati lake,kitendo kilichomfanya Mwenyekiti huyo wa Kijiji aangue kilio kikuu

TAFSIRI YANGU

Hali ya umasikini ni mbaya sana mitaanj,mtu mzima kutembea amevaa shati lililochanika,tena yeye akiliona ni shati maalum la kumpokelea Waziri aliye katika Ofisi ya Makamu wa Rais inasikitisha

Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imekuwa ikitamba kwamba ni serikali ya watu masikini,je hii inamaanisha kwamba haitauondoa umasikini kwa kuwa ukiondoka basi inakosa mizizi?

Kilio cha Mwenyekiti huyo wa kijiji,mtu mzima,akatoa machozi baada ya kupewa shati nadhani ana mengi katika familia yake,hatujui watoto wake wanavaa kweli? Wanakula? He hali hii iko kwa watu wangapi katika utawala huu? Je naye ni mpiga dili?

Tangu serikali iingie madarakani hakuna program yeyote ya kuondoa umasikini vijijini,matokeo ndio haya,NA utawala huu sasa una miaka miwili NA nusu,bado miaka miwili uondoke

Pia kuna tamko la kuzuia mitumba eti tutakuwa tunapeleka sisi mitumba ulaya,kwa hali hii kweli?

Japo serikali hii anasema ni ya masikini,lakini haitakiwi kuzidisha idadi ya watu
masikini

Taifa likihoji kuhusu umasikini mkali ulioletwa NA awamu hii,jibu ni MLIZOEA DILI

Badala ya kusisimua uchumi,hela zote tumeficha Benki Kuu,zilizobaki,tunawapeleka vijana wa kizungu wenye viwanda vya ndege za bombadia NA dreamliner

View attachment 554544

CRYING ONLY WONT HELP, DO MORE, HE REPRESENT WATU WENGI SANA WA AINA HIYO
 
CRYING ONLY WONT HELP, DO MORE, HE REPRESENT WATU WENGI SANA WA AINA HIYO
Kabisa

Watumishi,mikopo ya wanafunzi,wawekezaji,wajasiliamali,wanasiasa,vyama vya kijamii,mabinti wenye mimba utotoni,utawala wa sheria,na mengine wengi,wanahitaji kiongozi atakayetuvua shati lililochanika kwa mateso ya awamu hii na atuvike shati jipya
 
Asante Makamba kwa kutuvika Shati jipya.

" Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi ? Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye chakula na afanye hivyo hivyo "
Luka 3 : 10 - 11

Upendo wa kweli unaanza kujionesha katika vitu vidogo sana, ambavyo ni vikubwa.
Zawadi ya nguo na chakula huwa tunazipata kutoka kwa wetu wa karibu wanaotupenda kwa dhati kama, baba, mama, mtoto, kaka, dada nk.
Makamba umeonesha mfano wa kiongozi anayewathamini watu wake na hasa wenye shida.
Endelea na upendo huu,
sisi tuliovaa kaptula za vilaka hapo zamani tunajua jinsi nafsi zetu zinavyofulahi pale tupatapo msaada wa kaptula mpya.
Hakuna zawadi ndogo.
 
Isije ikawa kanunua swagga halafu nyie mnasama limechakaa.
b74cbc258463c520de1eb14f0f2d3d0d.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
Hahhahah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Makamba kwa kutuvika Shati jipya.

" Makutano wakamwuliza, Tufanye nini basi ? Akawajibu akiwaambia, Mwenye kanzu mbili na ampe asiye na kanzu; na mwenye chakula na afanye hivyo hivyo "
Luka 3 : 10 - 11

Upendo wa kweli unaanza kujionesha katika vitu vidogo sana, ambavyo ni vikubwa.
Zawadi ya nguo na chakula huwa tunazipata kutoka kwa wetu wa karibu wanaotupenda kwa dhati kama, baba, mama, mtoto, kaka, dada nk.
Makamba umeonesha mfano wa kiongozi anayewathamini watu wake na hasa wenye shida.
Endelea na upendo huu,
sisi tuliovaa kaptula za vilaka hapo zamani tunajua jinsi nafsi zetu zinavyofulahi pale tupatapo msaada wa kaptula mpya.
Hakuna zawadi ndogo.
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom