Umalaya: Utamaduni unaokubalika Tanzania

Umalaya: Utamaduni unaokubalika Tanzania

Glasnost

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2017
Posts
266
Reaction score
259
Jamii ya watanzania imekumbwa na janga kubwa la kusikitisha. Utamaduni wa kuendekeza ngono na kufanya umalaya wa kila aina kati ya wanandoa na walio kwenye mahusiano umeshamiri, unazidi kukua kila siku na imegeuka tabia inayokubalika katika jamii ya watanzania hususan vijana na wazee-vijana kwa ujumla.

Tabia ya walio kwenye ndoa kuchepuka au kuwa na mahusiano nje ya ndoa inaonekana ni tabia ya kawaida sasa hata katika mahusiano ya uchumba, bado unakuta wanasaliti wapenzi wao. Imekuwa kawaida kumkuta mtu anayetarajia kufunga ndoa kuwa bado kwenye mahusiano mengine bila hata uoga au heshima kwa mpenzi wake. Na hata baada ya ndoa kumkuta anaendelea kuwa na mahusiano ya nje. Hivyohivyo kwa walio kwenye uchumba.

Na watu wa aina hii ujisifu kwa kusema kwamba “Mwanaume rijali lazima uwe na wanawake wengi au wanawake ni urithi wetu” kuashiria kuwa ni haki na ni sahihi kuwa malaya. Au mwanamke yupo kwenye ndoa sababu ya pesa na si upendo au ni hulka tu na anapenda kuchepuka na mtu au watu wengine. Japokuwa kwao neno malaya laweza kuwa halina maana yoyote au halipo kwenye fikra zao.

Tangu lini umalaya ikawa sifa? tena bila aibu mtu kukubali yeye ni malaya na ana michepuko kila sehemu. Kwamba yupo na mtu flani kwa sababu ya pesa, mapenzi ya kihuni au hapati raha akifanya na mtu mmoja kwa mda mrefu.

Sio tabia nzuri hata kidogo kwani inajenga jamii mbovu, isiyo na maadili mema kwa vizazi vya sasa na vya baadae. Pia inajenga uoga, wivu na magonjwa ya kiakili kwa baadhi ya watu wanaotamani siku mmoja waoe au waolewe. Kwa walio kwenye ndoa magonjwa, mimba isiyotarajiwa au kubambikiwa, kujiua ni baadhi ya mambo hutokea.
 
Kuwa na demu mmoja hapa bongo ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe,bora kufyekelea mbali papuchi za aina mbalimbali Maisha yaende
 
Kwa sababu demu mmoja akishagundua unampenda na yuko peke ake basi ataanza kujiamini na kukuletea vituko kibao vya kukupa stress kwa kujua huna pa kwenda kupunguzia nyege zako,hata kama huna mchepuko basi jitahidi uwe unaenda nunua malaya
Kwa nini?
 
Sio kweli lakini pia jaribu kujiamini wapo wanawake waaminifu
 
Umesema umalaya ni utamaduni unaokubalika tz kumbe
 
Sisi waafrika by nature tunatakiwa kupractice POLYGAMY haya mambo ya MONOGAMY ni ya wazungu ...
Umalaya unatokana na sisi kujifanya tunawaiga wazungu kuwa na mke mmoja wakati hatuwezi.

Tukihalalisha wake wengi haiwi umalaya .
Maana definition ya umalaya tunaitengeneza sisi wenyewe tunavyotaka
 
Kwa maana hiyo turuhusu ndoa za kimila/kikabila na tuache kufuata mafunzo ya dini za kikristo?
 
Ndio. Maana kuwa na mke mmoja sio nature yetu ni mambo ya kuletewa tu.. hata kwenye biblia watu wengi tu kwenye old testament wana wake zaidi ya mmoja inakuwaje sisi tulazimishwe kuoa mmoja??
Kwa maana hiyo turuhusu ndoa za kimila/kikabila na tuache kufuata mafunzo ya dini za kikristo na kiislamu?
 
Umalaya ni biashara kongwe duniani ambayo imeanza hata kabla ya cain na abel.

Tanzania hakuna umalaya. Ukienda Thailand au Ufilipino ndo utajua wanawake wa Tanzania wameokoka.
 
Ndio. Maana kuwa na mke mmoja sio nature yetu ni mambo ya kuletewa tu.. hata kwenye biblia watu wengi tu kwenye old testament wana wake zaidi ya mmoja inakuwaje sisi tulazimishwe kuoa mmoja??
Lakini umalaya ni tabia hata kipindi hicho kuna baadhi walikuwa na concubines. Sidhani ni suluhisho bali watu wakubali kuwa ni tabia mbaya na wabadilike kwa manufaa ya familia na maendeleo kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom