Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Hivi karibuni niliandika kuhusu chuki inavyoshamiri kila kona. Leo naangalia tena ni chuki gani inaendelea kukua. Zimebaki siku 9 tu tufunge Mwaka huu tuufikie mwaka wa Uchaguzi.
Hivi karibuni nimewaona Chama cha Upinzani wamefanya Uchaguzi wao ambapo viongozi waliotokeza kuongoza Chama wanaonekana ni wale wa mikikimkiki (hata gazeti oja limesema hivyo). Chama hicho kimekuja na usemi wa "no hate no fear'.
Nilifurahi kuona neno hate linatokeza katika slogan yao nikatambua kuwa kumbe wameshagundua kwamba kuna chuki sana inaendelea miongoni wa Watanzania.
Chama hicho pia kimekuja na hoja ya kusema wanachukia umaskini na kulaumu chama Tawala kuwa kinajenga hoja kwa kujfianya kinatetea walalahoi yaani maskini.
Kwamba maskini waendelee kuwepo ili waendelee kutetewa wakiwa katika hali hiyo hiyo ya umaskini. Hii kali kweli.
Leo kwa kweli naona nigusie chuki ambayo imejengeka kwa watumishi wa umma. Nchi yetu ina familia ambayo at least katika wanafamilia anakuwepo aliyeajiriwa Serikalini.
Sasa hao wanafamilia hujivunia ndugu zao waliopo Serikalini kwa sababu wale wanaojali undugu angalau huwakwamua hao ndugu kimaisha na hasa shida ndogondogo.
Sasa kwa hali ilivyo kwa sasa wanafamilia wenzetu wanaofanya kazi Serikalini ni kweli wamekuwa na chuki sana na Serikali hii. Kuna mengi yanasababisha chuki lkn katika uchunguzi wangu nitaongela angalau haya.
La kwanza, kuhusu kupandishwa kwa mishahara - ukweli wafanyakazi wameumizwa sana awamu hii ya utawala.
Serikali hii ilipoingia madarakani ikaja na hoja ya kuonguza mishahara badala ya kupandisha. Wafanyakazi mishahara haipandi - mwaka unaisha wakiwa wanyonge - yaani hamna kitu.
Ndugu yangu mmoja ambaye ni IT expert Serikalini kaja kukopa kwangu jana shilingi laki 2 na nusu ili afanye manunuzi ya Sikukuu.
Nikiangalia familia yake na hiyo laki 2 unusu nashangaa kabisa. Maneno aliyoyatoa kuhusu utawala huu ni hatari tupu pamoja na kuwa alikuwa amejawa na woga mkuu. Hakika sio uwongo kilichomo moyoni mwa watumishi wengi wa Serikali ni Mungu mwenyewe anajua.
Nasema watumishi wengi kwa sababu wapo ambao kwa sasa wanakulia kivulini - mfano wale wa TANROAD, TARURA, Wizara ya Fedha, Ikulu n.k.
Wengine wengi wanalalama tu hakuna kitu ndiyo maana wanasubiri kuinjinjilia mbali Serikali hii Mwaka 2020.
La pili, hili la pili ni wale watumishi wa vyeti feki. Kama nilivyosema hapo pia hawa nao walikuwa na wategemezi kibao ambao wameathirika sana na zoezi hilo ambalo kutokana na uzembe wa Serikali yenyewe ilishindwa kuwatambua huko awali na ukawapa ajira.
Badala ya Serikali kuwatoa hao watu kwa utaratibu mzuri wengi walifukuzwa kama mbwa - ndiyo walifanya makosa lkn si tunaona mfano hata Wamarekani wanataka kumuondoa Rais wao madarakani mbona wanafuata utaratibu?
Hawa watu hata kusikilizwa hawakuwahi. Serikali hii wanaichukia sana. Siku zote ubabe huwatokea puani wababe. ni suala la muda tu na 2020 ishafika.
Tatu - kuna tabaka la watumishi wastaafu. Baada ya Mwaka jana Mifuko kuunganishwa basi watumishi wengi wakajua kuna ahueni watakuwa wanalipwa mafao yao kwa wakati.
Hata hivyo mpaka Mwezi Novemba mwishoni niliongea na mfanyakazi wa Mfuko huo mpya akanijulisha kuwa watumishi wote, akiwepo shangazi yangu, waliostaafu kabla kati ya Aprili mpaka Novemba mwaka huu hawajalipwa pensheni zao za mkupuo na hata za kila Mwezi kwa kuwa Mfuko huo hauna fedha.
Sasa hili likitamkwa wazi yule atakayetamka maneno hayo hawezi kuwa salama kwa sababu ataoenkana kutoa siri za Serikalini ila mie nina uhakikahakuna fedha kwa sababu hata shangazi yangu alistaafu Julai na mpaka sasa hajalipwa chochote. Hapo kuna chuki kubwa pia.
Nne, Serikali imeamua kuwa na ubabe wa kuhamisha hamisha hovyo wafanyakazi bila ridhaa zao. Wengine wanashushwa vyeo bila kusikilizwa na wengine kutishiwa tishiwa tu.
Ili kuwafanya wafanyakazi wasilalamike hata Kanuni za utumishi wa Umma zilibadilishwa ili zitamke kuwa Mfanyakazi anaweza kuhamishwa bila hata ya ridhaa yake. Wengi wanaacha kazi kwa ajli ya ubabe huu ni hivyo kujenga chuki dhidi ya Serikali.
Kuna mengi yanayosababisha chuki dhidi ya Serikali hii ya Utawala wa awamu ya 5 lakini kwa leo naishi kwa hayo.