Umafia wa serikali katika kipindi hiki cha lala salama ya 2010-2015

A JUSTMAN

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
439
555
Utaratibu ambao unatumiwa na serikali katika kuipitisha miswada mitatu kwa pamoja na kwa hati ya dharula ni wa kibabe na haufai.Ikumbukwe kuwa miswada hiyo ilikataliwa na wabunge wa pande zote walipokutana katika semina june 29 na kupendekeza kwamba muda uliobaki kuhitimisha bunge ni mdogo hivyo ni vizuri kusubiri bunge lijalo.

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Petroli wa Mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015 na Muswada wa Sheria ya Uwazi na Uwajibikaji Katika Tasnia ya Uchimbaji Tanzania wa Mwaka 2015.

Pamoja na mapendekezo hayo ya wabunge yaloafikiwa katika ile semina ya awali wanaharakati, wananchi na wazalendo huku uraiani tunastaajabu kuona kile ambacho serikali imeamua na kujiapiza kwa gharama yeyote ile kuipitisha hiyo miswada mitatu bila kujali chochote.

Tumeona wabunge ambao wamekuwa wakipinga hiyo miswada tayari wamefukuzwa kuhudhuria vikao vya bunge vilosalia na sasa ili mpitishe kama mnavyotaka kiulaini bila hoja makini za wabunge mlowatimua.

Tunaona mnaendelea kuijadili bila kujali lolote kana kwamba hii nchi ni ya kwenu pekee na ndio wenye haki zaidi kuamua na kufanya chochote mpendavyo.
Hivi ndivyo mlivyoamua kumalizia kuiuza nchi kwa wageni katika awamu yenu ya mwisho?
Tunafahamu miswada hiyo ni mibovu na haina maslahi kwa nchi na jamii ya watanzania na hakuna ulazima wa kuipitisha sasa au mnafanya haya kwa maslahi ya nani? Tunaomba mnaoshiriki kuipitisha huko bungeni mtupe majibu ya maswali hayo.

Pia wote mnaonshiriki kuipitisha hivi sasa kumbukeni dhambi hii kubwa haitawaacha bure kama mnavyofikiri itawafuata kokote muendako mpaka mtakapohukumiwa barabara kwa matendo na kauli zenu mnavyofanya hivi sasa.

Mnafanya umafia mkubwa wa kuuza raslimali zetu zilizotunzwa na waasisi wa taifa hili kwa umakini mkubwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo wangeamua kujinufaisha wao mnafikiri hivi sasa mngeuza nini?

Dhambi hii mtaibeba tu lazima iwe hivyo hata kama mkitangulia mbele ya haki makaburi yenu yatachapwa bakora na kizazi kijacho.

MUNGU WABARIKI WATANZANIA WANYONGE WANAOTESEKA KWA UDHALIMU WA WATU WACHACHE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom