Umachinga ni bomu kubwa sana

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
735
191
Ndugu wana JF. Umachinga ambao serikali yetu imekuwa ikiutukuza ni bomu kubwa na linalosubiri kulipuka. Kwenye kampeni yake ya urais Dr. Dr. Dr. Kikwete alitangaza kuwa atajenga machinga complex mpya TANO. Jambo la kujiuliza tu ni kuwa iwapo wote tutakuwa machinga nani atazalisha bidhaa zetu muhimu kama chakula na mazao ya biashara? Tunawezaje kuwa na jamii ya wauzaji pekee bila kuwa na wazalishaji? Tumeona madhara ya Umachinga kwa mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara ambako hali si shwari kiasi hata vyakula n tatizo.

Tuache jamani kukuza umachinga, tukuze ajira zenye tija na mwelekeo ya kuendeleza uchumi wa nchi. Hili BOMU la machini siku likipasuka litatumaliza wengi.
 
Back
Top Bottom