Uliwezaje Kumwabia mchumba/mke mtarajiwa kuwa una mtoto wa ujanani

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,033
173,724
Katika safari ya maisha mengi hutokea kwa vijana wengi ikiwemo swala la kupata watoto mapema zaidi kutokana na mabadiliko ya tabia mwili na vile tunatofautiana viwango vya mihemuko ya ujana.

Kimsingi mtoto ni baraka,faraja, malaika, ndugu, damu na alama isiofutika katika jamii na hutumika kama kitambulisho cha jinsi kamili.

Swala liliopo ni kuwa mara nyingi watu waliotuzalia watoto ujanani ni nadra kukuta ukiwa mtu mzima unaweza kuoa tena maana ni kama connection ya kihisia inakuwa haipo tena tokana na mambo kubadilika ama mazingira. Japo watu wengi huficha ila sidhani kama ni busara kuficha lolote kwa mtu wako maana ukweli hukuweka huru siku zote.

Ishu za kujadili:
1.Ni vipi utaweza ama uliweza kumwambia mchumba wako wa sasa ambae unatarajia kuoa kwamba una mtoto wa ujanani?

2.Je, mnadhani wakati sahihi wa kulisema hilo ni kabla au baada ya kuoa?

3.Wanawake mliokutana na situation hii je mlichukuliaje hilo swala na iliwaathiri kwa namna gani?

NB: Mtoto wa ujanani sio wa baada ya kuoa mke. Ni wa enzi za friendly matches on your teen ages. 13-19 hapo!
 
Ni vyema na ni rahisi zaidi kulisema mwanzoni kabisa.
 
Muda wowote acha uoga kijana.
Hawa wanaokataa ama kuficha watoto zao,wanawanyanyapaa ndo amseme hadharani?kuna jamaa alizaa na mdogo wangu akakimbia hakutaka kujihusisha kwa lolote anzia mimba,wala hata kumtambulisha kwao hadi leo katoto kana miaka 5,akaja akaoa kapata mijike mitupu eti anajileta anadai mtoto familia imemtoa baruuu haamini kabaki kulialia ka jibwa koko
 
Kabla hata sijakutongoza ktk ile stori stori simalizi dk 2 sjamtaja mwanangu kua ananchekeshaga..so lazima ataniuliza hv una mtoto? Namjibu NDIO tena namalizia nampenda vibaya mno..baada ya kuzoeana na ukanijua vizuri ndio nakutongoza sasa hapo tyr ushajua namimi ninae.

Asilimia kubwa ya wadada wana watoto ila wamewaficha huko kwa bibi zao so usipokua wazi kusema wewe mwanaume mapema nae ataogopa kukwambia ukweli..

Muda muafaka wa kulisema hili ni Mapema kabla hata hamjaonyeshana hisia za kutakana..Mtoto hatengwi wala kufichwa MSEME na Jivunie uwepo wake popote unapokua.

Mdada atae nikataa kisa nina mtoto na ANIKATAE tu hanisumbui kichwa hata day 1
 
Unaweza ukasema mwanzoni kabla ya kumtongoza au mwanzoni mapenzi yanapoanza kukolea ndio wakati muafaka anakuwa ameshafurahia mapenzi na anakuwa hana jinsi zaidi ya kukubaliana na hali halisi, usiache mpaka unapoamua kuchumbia ama kuoa ni kosa kubwa sana litakugharimu
 
Mwambie baada ya ndoa kuwa una mtoto wa ujanani uone balaa lake.

Ni wakati mwingine watu uhofia kuwapoteza wale wanaowapenda kwa kuwaambia ukweli, lakini hili ufurahie mapenzi jaribu kuwa muwazi kidogo mwambie kabla penzi halijakolea utamu... Baby, kuna moja, mbili, tatu katika ujana wangu niliruka sarakasi nyingi nikakwaa kisiki.

Hapo unakaa kusubiri majibu yatakuwaje, maana bado ni asubuhi na mapema maamuzi yoyote yanaweza yasiwe machungu sana kwa yoyote kati yenu.
 
Africa mwanaume akizaa ujanani kabla ya kuoa siyo kosa lake ni mihemko tu ila mwanamke akizaa ujanani kabla ya kuolewa ni kosa lake na ni umalaya utadhani wanaume wanazaa kivyao na wanawake wanazaa kivyao haki ya nani vile waafrica bado tuna safari ndefu.

Hata sitaki kubishana na mtu.
 
ww una mtoto? je mpenzi wako wa sasa anajua? uliwezaje kumwambia kuwa una mtoto?
 
Me nadhani mda sahihi nibaada yakumtanua mapaja ndio namueleza ukweli woteee nabaada yahapo yeye ndio atachagua kusuka au kunyoa nampa nakamsemo kawaenga 'ukipenda boga, penda naua lake', 'mchagua shamba sio mkulima',
 
Back
Top Bottom