Uliwezaje kuachana na mtu uliyempenda?

Nilijikuta namtoa Moyoni mdogomdogo pasi yeye kujua na hatimaye nikamove on
Ingawa alinitafuta ila sikuwa na hisia naye Tena kama mwanzo siyo Siri kipindi yupo Moyoni mwangu hata angenambia nilipe mahari 7m ningekopa equity ili nimuoe
Sometimes MUNGU anakupatia watu frani ili ujifunze.
 
Habari wakuu mm nisingependa kuwachosha naomba niingie moja kwa moja mada husika:

Mwaka 2020 mwezi wa kwanza nilitongoza kadem( 20 age)ka mtaa ambapo nilikua nafanyia biashara zangu, wakati ndo tumeanza mahusiano nikaja kugundua kua huyu binti alikua anatoka na kwenda club usiku, kwakua alikua anaishi na dada yake tu kwenye nyumba za kupanga hivyo alikua na uhuru japo kua dada yake hakua na tabia kama zake.

Nilipo gundua nilikaa nae chini na kumwambia maisha anayo ishi si mazuri hasa kwa mwanamke ambaye anaplan za kupata mume bora, sisi wanaume hua tunachagua sana yupi dem wa kuoa yupi wa kumla tu. Offcouse alinielewa.

Baadae nimeishi nae kama miezi mitatu akaanza kunigusia mambo ya kumtoa out, kwakua mwanzo wiki ya kwanza ya mahusiano alikua anatolewa out na jamaa mmoja hivi ambaye aliondoka mtaa ule kwa baadae, nilipo gundua nikamwambia maisha ya uongo siyapend kwenye mahusiano kama huwezi kua na mie ni bora kmya kmya unipotezee akanielewa.

So kwa sababu hiyo nikaona ni bora mala moja moja niwe nakatoa out tunaenjoy maisha.

Nilikatoa out na siku hiyo ikawa siku ya kwanza mm kufundishwa mambo ya kwenda club na mwanamke pamoja na kunywa pombe, mm binafsi skufurahia maisha hayo ila nilifanya kumfurahisha huyu mpenzi wangu, hata nilipo kua pekeyangu niliapia kua hakika huyu si mwanamke wa ndoto zangu lazima nitaaachana nae, tumeishi wote hatimaye dada ake akahamia kalibu na getoni kwangu.

Dada yake alikua na boyfriend ambaye alikua anakuja kula na kupiga mbunye kwa sisita na kuondoka, baada ya mm kuishi na mdogo wake dada ake akachukulia kama chance ya kumvuta huyo boy wake kwake na wakaanza kuishi wote.

Dem wangu hakua na namna ikabid awe analala kwangu tukaanza maisha akawa akuja jion anapika asubuh anaenda kwa dada ake mwishoe akaonekana kama mke wangu hata kwa wapangaji wenzangu, lakin mm na yeye tulitambua kua tupoje.

Maisha yakaenda mikasa na changamoto tukapitia + kusaidiana mpaka mwaka ukaisha tukiwa ote kwenye mahusiano na mwezi wa kwanza mwkaa 2022 tunakamilisha miaka miwili ya mahusiano. Bado naapa hata leo hakika huyu si mke wangu kwakua bado anapenda kunywa pombe.

Sifa za huyu dem mbaya na nzuri.

1: Ni msafi sana anajua kupika na ana nijali ila hapendi kukosolewa.

2: Hajasoma kaishia darasa la saba.

3: Hajui biashara yoyote tofauti wala hana future na maisha yake.

4:Hasali.

5: Sio mchoyo kwa upande wa chakula na

6 : Mcheshi sana na nchangamfu hata kwa wageni.

7: Kutokana na maisha yake ya uhuru sana hana tabia ya kunipelekea maji ya kuoga bafuni ila nilimfindisha akawa anapeleka.

Hizo hapo juu ni sifa zake baadhi ambazo mimi naona hazitoshi kua mama wa watoto wangu.

Kwasasa mimi nimeanza kuyumba kiuchumi, na nimeyumba kweli sababu kubwa ni wezi, na biashara kukosa wateja ni (m.pesa na tigo pesa) nazani hii biashara kwa sasa mawakala wanajua inavyo waumiza akili.

Kutokana na sababu ya kiuchumi nimekusudia kuhama mkoa na kwenda mbali kiutafutaji, nikajipange upya lakini pia sababu ya kiuchumi inanipa nguvu na kunikumbusha huyu si mke wa ndoto zangu hivyo natakiwa nimuache mala moja.

Sasa wadau mda umefika na nilimuweka wazi hali ya kiuchumi niliyo nayo kwa sasa na yeye mwenyewe anaona uhalisia ila jana nimemwambia kua mda wa mm kuondoka umefika naona kaishiwa raha na mda wote analia, anaonekana ni mtu wa mawazo sana na kiukweli ananipunguzia nguvu ya kuamua kuondoka na kwenda kupambania maisha yangu huko ninako kwenda.

Nimedhamilia kumuachia hela ya mtaji, na nitaondoka nitamwachia geto ambapo nimekusudia nisipo rudi litakua ni sadaka kwake yeye aanzie maisha yake hapa, nitamuachia chakula cha kutosha ndani.

Nafanya hivyo ili iwe kama kulipa fadhira ya wema alio nitendea kwangu(kunipikia,kufua uaminifu wake kwangu) hivyo yani.

Ila nimeanua kumuacha kwakua hawezi kuacha pombe kwakua nilisha muonya ila bado anakunywa kmya kmya na kumpiga siwezi, nilimwambia aanze kwenda kanisani ila hatekelezi, hana maarifa hivyo nahofia kumuoa akiwa mama watoto wangu tutagombana juu ya kulea watoto kwakua mm nataka watoto wangu wapate malezi wawe na maadili ya kidini, ila yeye hayupo hivyo.

Wadau naombeni ushauri na experience uliwezaje kuachana na mtu unaye mpenda?
Kaka wee mpige chini tuu wala usiangalie nyuma. Kama hupendi mnywa pombe usijilazimishe eti kisa utambadilisha hilo halipo. Utapata majanga tuu huko mbeleni. Achana nae mbususu zipo nyingi tuu.

Alafu wee kupika tangu lini ikawa kigezo cha kumsifia mwanamke bwana? Mwanamke tako na uzuri. Kupika sii unakula ata kwa mama ntilie na maisha yanaenda
 
Ni worse of time au lucky of time...Kuna muda nili kutana na watu sahihi kwenye wakati usio sahihi
Aluta continue kwa wanaume wote wapambanaji kuna muda wa kuchagua RIDE OR DIE
Wakati mwingine kuchagua familia ni Opportunity cost
It means una forgone all other issue....ndoto na matarajio

Asante Mungu kwa pumzi haya mengine ni ya ziada tu.
 
Huna sababu ya maana ya kumuacha

Sababu zote ulizotaja ni za kawaida sana, yaan sana

Nikwambie tu moja, wanawake hawapendagi kukosolewa, wanahisi kusimangwa,humpendi, una gubu n.k

Huko kunywa pombe ataacha tu, nenda naye taratibu
 
Huna sababu ya maana ya kumuacha

Sababu zote ulizotaja ni za kawaida sana, yaan sana

Nikwambie tu moja, wanawake hawapendagi kukosolewa, wanahisi kusimangwa,humpendi, una gubu n.k

Huko kunywa pombe ataacha tu, nenda naye taratibu
Tatzo Mkuu nataka kuhama ki utafutaji na yeye hayupo Tayari mm kuondoka anajua namuacha, lakin namuacha sehem salama, namuacha akiwa na dada ake lakin pia namuacha akiwa karibu na nyumbani kwao mm huko ninako kwenda naenda kiupambanaji ntamuita Mambo yaki kaa sawa.
 
Ndugu kwenye suala la pombe kama ulikuta tayari anakunywa ,usimlaumu sasa..

sio rahisi kuacha pombe, shukuru Mungu hujaingia kwenye pombe, pombe ikikuingia kuiacha n ngumu na inachukua muda ungeenda nae taratibu..

jambo lingine ungejivunia mwanamke ambaye anakuomba umtoe mtoke wote, yani anajivunia na haoni aibu kuwa nawe..

pia mkuu, umesema huyo demu ana miaka 20, huo ndo muda wake wa kufanya hvyo vistarehe atoe ushamba wakifikaga miaka 25 wanatulia wenyewe,..umri huo anakuwa na kaushamba fulani hivi ,na kuiga kwingi, kwanza alitakiwa awe sekondari anasumbuana na walimu na kuishi kwa viboko, hivyo huo ndo umri wake wa usmbufu kaka..

kama asipotoka out sahv na kunywa pombe sahiv atapata tabu baadae atalazimisha kuvifanya hvyo vitu katika muda ambao sio sahihi..
 
Mkuu upo future nini?, maana umeandika mmeanza 2020 na mwaka 2022 mmetimiza miaka miwili, sisi bado tupo 2021
 
Aisee changamoto japo sio sana.

Kwanza kwenye swala la.ulevi hakuna mtu aliezaliwa mlevi nenda nae taratibu tu mda ukifika ataacha.
Ongea nae taratibu atakuelewa ww akuruuhusu utangulie baadae yeye atafatia.
Kuhusu kutokusoma unaweza kuanza kumfundisha taratibu elimu ya biashara na kumwambia umhimu wa yeye kujikita kwenye uzalishaji pia ili inapotokea ww umeanguka/ haupo asijepata shida kwenye kuendesha life lake mwenyewe computer
 
Mpesa na tigo pesa + demu choro=lazima ufirisike mkuu
Ila we dada unajiskiaje kumuita mwanamke mwenzako choro?ni wivu au ni nin?na pia kuidharau biashara ya tigo pesa na mpesa unazozidharau wakat zinawaweka watu mjin,sijapenda mchango wako umekaa kidharau Sana na kujikweza,cjaona kosa la huyo binti,kwanza bado Yuko katika kipind cha ukuaji hizo baadh ya tabia zinazomkera mwenzake cjaona km ni tatizo Sana na zinaweza kuisha kadri huyo bint atakavyo kuwa anakua au kuanzisha familia yake Kama kupata watoto
 
Ila we dada unajiskiaje kumuita mwanamke mwenzako choro?ni wivu au ni nin?na pia kuidharau biashara ya tigo pesa na mpesa unazozidharau wakat zinawaweka watu mjin,sijapenda mchango wako umekaa kidharau Sana na kujikweza,cjaona kosa la huyo binti,kwanza bado Yuko katika kipind cha ukuaji hizo baadh ya tabia zinazomkera mwenzake cjaona km ni tatizo Sana na zinaweza kuisha kadri huyo bint atakavyo kuwa anakua au kuanzisha familia yake Kama kupata watoto
Pole mkuu,binadamu tunatofautiana matumizi ya ndimi.usikasirike tafadhali maana mwenyewe naishi kwa kuungaunga tu
 
Back
Top Bottom