Uliwahi kukutana na Mauzauza gani ya giza/uchawi katika Nyumba ya Kupanga au ulipohamia nyumba mpya?

[QUUlikuwOTE="Jojo123, post: 46162779, member: 122463"]
Mbona sijawahi kwenda kwa waganga maisha yangu yote

Ulikuwa connected kiroho bila kujua na mtu uliyeanzisha naye mahusiano[/QUOTE]Nime kuinbox kijana ili nijifunze jambo abt your answer
 
Je nivitu gani kwenye ukoo vinavyo weza kunifuatilia bila kutoa order au kueleweka yaan mtu ambeye sina connection na mambo ya giza alafu nifatwe mjini kiajabu bila mtu yeyote kujitokeza na kusema kama wana nihitaji?
Kumbuka kuna maagano ya ukoo ya vizazi vilivofanya wew kuwa hapo ulipo hivo c jambo rahic kukwepa viapo hivo na wala havitoki kwa maombi ila kiasili kama vilivowekwa ndivo vinavotolewa
Hvo kuandamwa na mambo yaliyoapwa na waliokutangulia ni jambo rahic tu na ni pocble 100%
 
Kumbuka kuna maagano ya ukoo ya vizazi vilivofanya wew kuwa hapo ulipo hivo c jambo rahic kukwepa viapo hivo na wala havitoki kwa maombi ila kiasili kama vilivowekwa ndivo vinavotolewa
Hvo kuandamwa na mambo yaliyoapwa na waliokutangulia ni jambo rahic tu na ni pocble 100%
Dah.. haya Mambo ni hatari sana Mungu at hurumie kwa kweli
 
Kwenye huu uzi nimegundua tunao umizwa ni wengi sana.. hakika kila eneo kuna hitsjika nguvu ya Mungu
 
sitosahau mwaka jana yaliyonikuta mwaka ambao sitaki niukumbuke kabisa stori inaanzia hivi;
Nlihama mbezi kupisha ujenzi wa magufuli stand coz nlikuwa naishi nyumba zilizolipwa pale nyuma ya stand, hivyo nikalazimika kuhamia kigogo mti pesa
nlipanga nyumba moja nzuri tuu yenye riziki sana sema tulishindwana sababu nyumba ya urithi kila mtoto anamiliki vyumba vyake. kero ilikuwa kwa mabint wadogo wamiliki walikuwa na mdomo sana heshima hamna nikahama
Kimbebe kinaanza nlihama nikapata chumba mazingira jirani kizuri haswa, nliingia vyema baada ya mwezi kuna siku nliamka asubuhi niko nje, lile swala halikuniingia akilini nikajiuliza sana labda nlikula mtungi nikatoka nje usiku ila hapana jana yake sikunywa pombe kabisa.
Ile hali ilinisumbua sana nikaanza kuota mandoto ya ajabu biashara yangu kariakoo ikawa inaanza kusuasua, kuna shemeji yenu nlikuwa najilia vyangu akawa anakuja maramojamoja nikamdokeza nae akanijuza akija hua anaota ndoto mbaya sana. Jumapili moja nipo home nimetoka kuoga naingia ndani nikakutana na nyoka(mwenye uwezo wa kudhuru) anateleza kwenye tiles ndani nikampiga nimauua.
Baada ya kumuua nikatoa tahadhari kwa wenye watoto wadogo pia, nikamjuza mwenye nyumba manake ni yanki tuu kaachiwa urithi nae. Baada ya kumuua yule nyoka nlianza kuona damu ndani mwangu sio mara moja nikitafuta kilichofia ndani kwangu ama kuingia kimeumia sikuoa kabisa , nipatwa hofu nikaaza kusali udhuria makanisa ya kiroho sana nlizidi endelea kuona damu mzito ndanimwangu hofu ilizidi sana.
Kufupisha tuu damu nlikuwa naona mimi na shemeji yenu nae aliwahi kuona mara kadhaa ile nyumba nlifilisika nikiwa pale mtaji wa ml6.5 sijui uliishaje sina matumizi makubwa sio mtu wa bar wala wanawake, nlifikia kupigwa makofi ndani usiku anayekupiga humwoni nliteseka sana wapangaji wenzangu nao wakawa wanapitia hali ngumu sana nao. Kiufupi nlifiwa na mtoto pia kwenye ile nyumba nikawa sina hili wala lile kuna siku shemeji yenu anakaribia kujifungua usiku nlipigwa bonge moja ya kelbu afu nikachekwa kicheko kimoja hicho mwanangu alikuja zaliwa vyema ila aliishi week 2 hakuwa na tatizo hata kidogo ilikuwa ajabu sani nimeweza kurudi mbezi kwa mara nyingine sasa.
NB uswahilini sio kuzuri kabisa yapo mengi sana haya ni machache.
Pole sana ndugu ndo Dunia
 
Kuna story kama mbili niliwahi kuzisikia Clouds FM kipindi cha Leo Tena, Segment ya Hekaheka chini ya mtangazaji Geah Habib.

Ebana ee Story ya kwanza ni ya mama mmoja mfanyakazi Dar es salaam, alikuwa na maisha mazuri tu na alikuwa na mfanyakazi wa ndani. Siku moja huyo mama alikuwa anaenda kazini, kapanda gari lake kaenda kazini, kabla hajafika mbali akakumbuka kasahau kitu ndani, ikabidi ageuze gari kurudi nyumbani kuchukua hicho kitu, kafika nyumbani kakuta beki tatu (mfanyakazi wa ndani) kasafisha nyumba, kaosha vyombo, Kashaivisha na chakula kila kitu kiko vizuri, alafu dada wa kazi kakaa sebuleni ananitizama TV, aisee huyo mama alipigwa na butwaa kumbuka huyo mama alifanya kitendo cha kutoa gari nje na kisha kurudi nyumbani kuchukua kitu alichosahau, huyo mama anasema kitendo cha kutoka na kurudi hakikuzidi nusu saa, ila alikuta mpaka chakula kishapikwa, na usafi umefanyika... ilibidi tu huyo mama amtimue beki tatu...

Tukio la pili ni la kisa kingine ambacho kuna mama mmoja huko huko Dar, alikuwa kila ikifika usiku mida fulani anamsikia beki tatu (mfanyakazi wa ndani) anatoka nje kwenda chooni. Sasa kuna siku mmoja ikabidi afuatilie kuona nini kinaendelea. Siku hiyo akamuona beki tatu anatoka nje kama kawaida kwenda chooni, cha kushangaza akaona mbona Beki tatu amekaa chooni muda mrefu bila kutoka, jambo ambalo kibinaadamu sio la kawaida. Ikabidi huyo mama atoke nje kwenda chooni kumtizama huyo beki kuona kwa nini amekaa chooni muda mrefu. Kufika chooni anaita binti haitiki, kufungua mlango wa chooni anakuta nguo za beki tatu zimetundikwa tu na binti hayupo. Ikabidi usiku huo huo mama wa watu arudi ndani, akasubiri baadae sana akaona binti anatoka chooni anarudi ndani. Mama yule ikabidi asubuhi yake ambananishe yule beki tatu, yule binti sasa ndipo akafunguka huku analia na kujutia, kuwa anapitwa usiku na ndugu zake wa vijijini huko kigoma kwenda kuwanga, na walikuwa wanampango wa kumchukua mtoto wa kiume wa huyo mama wakamfanyie yao. Huyo mama alipigwa na butwaa, na kumtimulia mbali huyo binti, japo binti yeye hakutaka kurudi kwao tena na alikuwa analia kuonesha kama huo uchawi analazimishwa na ndugu zake
 
Kama kichwa cha habari kinavyo uliza..

Ili kuwasaidia watu wengine wano pitia majanga katika nyumba za kupanga.

Twambia ulikutana na mambo gani ya kustajabisha na uliyatatua vipi?

Kwa mimi hapa nimekutana na mambo ya ajabu katika miaka yangu 12 ya kupangisha hapa Dar es Salaam, Kwanza kabisa kuna nyumba nilipangisha Makumbusho nikawa nikilala nafunga mlango vizuri ila nikiamka nakuta mlango uko wazi umefunguliwa kabisa mbu wana aingia baridi kali.. nika hisi mm ndio nime jisahau nika puuza baada ya siku tatu tena nika kuta upo wazi kabisa. hapo nikawa najiuliza mbona jana nilifunga na nika kumbuka nilifunga na ufunguo kwa ndani na nilikuwa na ongea na demu wangu uku nikimwambia mm ndio nafunga ni lale na nika zima taa vizuri uku simu ipo sikion nikaingia kwenye net uku tuna ongea na demu mpaka nikaishia usingizini. Ajabu asubuhi mlango uko wazi baridi kali na mbu ndani kibao. NILI HAMA NDANI YA MIEZI MIWILI TU A WAKAGOMA KUNIRUDISHIA HELA ZANGU.

2. Kisa kingine nikikuwa naishi Mwananyamala ile nyumba ilikuwa ina mauza uza ajabu, ukificha hela na ume zihesabu vizuri unakuta zimepungua asubuhi na ndani naishi mwenyewe. mlango unefungwa, na nikilala naota ndoto za ajabu na kutisha.. NILIHAMA MWENYEWE.

3. Kisa cha tatu. Kuna nyumba nilikuwa naishi hapo Salasala nikawa nalala vizuri ila nikiamka najikuta ule upande wa miguuni ndio kichwa kipo na nguo nili lala na boxer ila namka boxer ipo pembeni ikawa hivyo mara kadhaa, mwishowe nikawa sina amani nika hama.

TWAMBIE MWENZETU ULISHA KUTWA NA MAUZA UZA AU KWAKO SHWARI TU.?
Tusimulie vizuri kwenye kuvuliwa Boxer,,

Wanakuvua tu wakuache au?
 
Back
Top Bottom