Uliumbwa kwa mavumbi na mavumbini utarudi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,825
730,243
Hapa ndio penye siri ya dhana ya kifo kwenye mwili uharibikao.

Kwa imani za Mungu mmoja, binadamu aliumbwa toka mavumbini...aliumbwa kinyago mpaka pale alipopuliziwa pumzi ya uhai/kuwekewa roho.

Mungu aliposema natuumbe mtu kwa mfano wetu dhana kuu ilikuwa kwenye ile pumzi ya uhai pumzi ya uzima, uzima wa milele.

Pumzi inayozungumziwa hapa ni ile pumzi ya kimungu ambayo IPO ilikuwepo na itakuwepo milele..haifi wala kuharibika ni pumzi roho isiyokufa.

Ndio maana baadhi ya imani hutumia maneno haya uliumbwa kwa mavumbini na mavumbini utarejea kamwe pumzi yako iliyokutoka haitajwi kwakuwa haijafa bali imerudi panapostahili ama la kwenda pengine popote.

Mungu sio mwili bali ni roho na pumzi ya uzima wa milele ukienda paradiso huendi mwili unaenda roho isiyokufa ukienda jehanam huendi mwili bali unaenda roho iliyobeba ufahamu.

Unapojitahidi sana kuugharamia huu mwili uharibikao kwa nguo na vipodozi vya gharama na karamu za kidunia huku roho ikiwa chafu ni sawa na kujipaka manukato ya bei ghali kwenye mwili mchafu.
 
Safi mkuu ....makanisa mengi ya siku hizi dhambi haihubiriwi ....upendo kwa jirani hauguswi kabisa .....turudi kwenye misingi badala ya kukomaa na kukemea mapepo huku tukibaki na dhambi mbaya za kusengenya, dharau, kutokusaidiana, kutokutenda haki n.k ...

Someni Luka 6 : 27-31 kama moja ya kipimo cha utakatifu ....
 
Amina mkuu asante kwa neno ila leo hata mi nimeshangaa... umeokoka lini? au ndio shetani akizeeka sana anakuwa malaika? (jst joke)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom