Ulishawahi kuugua tumbo ukiwa safarini?

Ulishawahi kuugua tumbo ukiwa safarini?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,965
Reaction score
26,160
Wakuu kwema?

Ebana nilikuaga naskia tu watu wakilalamika kuchafukwa na matumbo wawapo safarini.

Sasa me yamenikuta last week nikiwa safarini toka mkoa fulani wa Kanda ya Ziwa kuja Dar, yani ilinibidi nishukie Singida ili kuepuka ile aibu ya kuwasumbua makondakta kwenda kuchimba dawa kila dakika.

Sitasahau ile siku asee niliharisha mpaka nikahisi utumbo nao umetoka , shukrani za pekee ziwaendee wale traffic police wa pale stand ya mkoa wa Singida kwa msaada walionipa na pia madaktari wa hospital ya mkoa wa Singida kwa kunipa huduma stahiki kwa wakati.

Kuna aliewahi kupata mkasa kama huu?
 
Niliwahi kukamatwa na tumbo morogoro wakati nakuja dar. Sikuwa na namna zaidi ya kuomba nikaharishe tuu.

Cha kutia moyo ni kwamba nyakati kama hizo aibu huondoka kabisaaaa, yani either uchague kujinyea ama uombe msaada[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ha ha..umenikumbusha safari yangu ya arusha to mbeya miaka 12 iliyopita enzi hizo bado kachalii kadogo kabisa,nimefika iringa tumbo likanichenchia..siku hiyo niliweka aibu pembeni asee..
 
punguzeni ubuge ubuge kila kitu unataka ule
 
dawa yake ni ndogo sana unanunua Coca cola soda hii kidogo tuu unakunywa pamoja na chumvi unalamba kidogo inachukua dakika chache tuu kukata hii dawa wanaijua madereva wale wa masafa marefu tunawaita madereva wa UEFA wanaoenda Bulawayo au Harare na Congo na Mara nyingi unawakuta na chumvi kidogo ndani ya bus soda zipo tuu...huwezi kushuka kisa unaharisha utapewa hiyo dawa yao na safari unaendelea hii sio dawa ya kutumia nyumbani ni kwa ajili ya dharula tuu maana hatujui ukichanganya soda na chumvi huko tumboni kinachotokea...
 
Wakuu kwema?
Ebana nilikuaga naskia tu watu wakilalamika kuchafukwa na matumbo wawapo safarini.. Sasa me yamenikuta last week nikiwa safarini toka mkoa flani wa kanda ya ziwa kuja Dar, yani ilinibidi nishukie singida ili kuepuka ile aibu ya kuwasumbua makondakta kwenda kuchimba dawa kila dakika.. Sitasahau ile siku asee niliharisha mpaka nikahisi utumbo nao umetoka , shukrani za pekee ziwaendee wale traffic police wa pale stand ya mkoa wa singida kwa msaada walionipa na pia madaktari wa hospital ya mkoa wa singida kwa kunipa huduma stahiki kwa wakati.
Kuna aliewahi kupata mkasa kama huu?
ulikula kyepe cha shinyanga stendi nini?
 
du, usiombe yakukute. Nimetokea zangu Moshi, baadaya la kula chakula tu pale Mombo tumbo likanishika. Nilijikaza mpaka nikatoaka jasho baada ya hapo nikamwita binti(konda) asimamishe nikaharishe porini. Ile wamesimamisha tu basi nichimbe dawa; kumbe sikuwa peke yangu, watu aliingia vichakani mfululizo mpaka makonda wenyewe hahahahahahaaa
 
Tumbo si mchezo! Mie nilikamatwa na tumbo safari ya Dar -Mby, nilipambana nalo ile kufika kona za Iyovu basi likala pancha ya mbele wakati abiria wamepagawa mie kimoyomoyo nikawa nashangilia najua hapo si chini ya dk.15 ambazo zilikuwa zinanitosha kushusha mzigo
 
Dar To Dom, huwa dipendi kula safarini but siku hyo kufika moro nikachukua tambi na azam mult. ile tunaisaka dakawa tumbo likaanza starter, nikajipa moyo kama litazingua hata dumila nitaomba msaada..
but kufeel shy ile watu wanisubiti mimi tuu mikate gogo.
nikajipa hope naweza kukaza kaza kama hali mbayanitaomba msaada gairo.
but kama mwanzo nokakausha tena.
balaa la mabalaa ni muda tunaitafuta kibaigwa.
ni jasho linanitoka kila nikiangalia nje ya gari kila nyumba natamani iwe choo halafu naombea gari liharibike.
lakini wapi hali ilizidi kuwa mbaya kufika kibaigwa nilimuambia tuu dereva shusheni begi langu hali ya tumbo langu si nzuri na nikawaomba wasinisubiri maana kama nilijua.
nilijisaidia zaidi ya lisaa pale kwenye choo cha sheli ya kibaigwa. sintasahau aisee na nilikua nawahi harusi.
mpaka leo, sili chakula chakununua zaidi ya matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siji kusahau safari ya Mwanza dar... Nimefika dom nikaparamia zabibu, baada ya hapo yalikuwa majanga..

Sent using Jamii Forums mobile app
Daa! Zabibu ndo balaa! nilikula zabibu Dom, baada ya hapo niwaomba wanishushe mlandizi nikate gogo. Niliona hata bar ipo mbali wakati ipo tu barabarani. Mtu ukisafiri ni bora ule biscuits tu au ule vyakula ulivyovizoea
 
Wakuu kwema?
Ebana nilikuaga naskia tu watu wakilalamika kuchafukwa na matumbo wawapo safarini.. Sasa me yamenikuta last week nikiwa safarini toka mkoa flani wa kanda ya ziwa kuja Dar, yani ilinibidi nishukie singida ili kuepuka ile aibu ya kuwasumbua makondakta kwenda kuchimba dawa kila dakika.. Sitasahau ile siku asee niliharisha mpaka nikahisi utumbo nao umetoka , shukrani za pekee ziwaendee wale traffic police wa pale stand ya mkoa wa singida kwa msaada walionipa na pia madaktari wa hospital ya mkoa wa singida kwa kunipa huduma stahiki kwa wakati.
Kuna aliewahi kupata mkasa kama huu?
Usipende kula vyakula vya mchuzi njiani kama wali au ugali nyama na chai za maziwa.
Enzi za Safina, Upendo, Matema Beach, Comfort unavalishwa pampasi unawekwa kiti cha nyuma ujishughurikie kwa raha zako ili basi lifike Mbeya saa tisa.
 
du, usiombe yakukute. Nimetokea zangu Moshi, baadaya la kula chakula tu pale Mombo tumbo likanishika. Nilijikaza mpaka nikatoaka jasho baada ya hapo nikamwita binti(konda) asimamishe nikaharishe porini. Ile wamesimamisha tu basi nichimbe dawa; kumbe sikuwa peke yangu, watu aliingia vichakani mfululizo mpaka makonda wenyewe hahahahahahaaa
Walikuona mkombozi wao aisee haahaa
 
Dar To Dom, huwa dipendi kula safarini but siku hyo kufika moro nikachukua tambi na azam mult. ile tunaisaka dakawa tumbo likaanza starter, nikajipa moyo kama litazingua hata dumila nitaomba msaada..
but kufeel shy ile watu wanisubiti mimi tuu mikate gogo.
nikajipa hope naweza kukaza kaza kama hali mbayanitaomba msaada gairo.
but kama mwanzo nokakausha tena.
balaa la mabalaa ni muda tunaitafuta kibaigwa.
ni jasho linanitoka kila nikiangalia nje ya gari kila nyumba natamani iwe choo halafu naombea gari liharibike.
lakini wapi hali ilizidi kuwa mbaya kufika kibaigwa nilimuambia tuu dereva shusheni begi langu hali ya tumbo langu si nzuri na nikawaomba wasinisubiri maana kama nilijua.
nilijisaidia zaidi ya lisaa pale kwenye choo cha sheli ya kibaigwa. sintasahau aisee na nilikua nawahi harusi.
mpaka leo, sili chakula chakununua zaidi ya matunda.
Sent using Jamii Forums mobile app
Zaidi ya lisaa we unashusha mzigo tu,huko tumboni sijui kulikuwa na hali gani
 
Back
Top Bottom