Ulishawahi Kumfikiria Prof. Sospeter Muhongo kama Waziri Mkuu?

Mm nahisi waziri mkuu atakuwa mwakyembe, january makamba waziri wa nje, pro muhongo waziri wa nishati , mwingilu nchemba ..mambo ya ndani, fulikonjombe ..ujenzi., jerry slaa Naibu waziri wa vijana utamaduni na michezo, n.k
 
Waziri mkuu sidhani kama atatokana na Mbunge wa kuteuliwa kwani Dr. Slaa kwa sasa hajagombea Ubunge mahali popote.
Kwani wabunge tayari walishapigiwa kura? Kumbe hata picha hujui kuangalia? Mchezo uko hivi, kufikia wakati wa kampeni atakuwa ameachiwa jimbo mojawapo ili agombee!!
 
muhongo msomi number one east afrika, the man deserve to be even a president and fit at all vacancies, jamaa kasoma hadi mwisho wa elimu, na sio akina mbowe ambao wali hata form6 walishindwa "kutoboa". namkubali sana hilo jembe, hapo wote akina mwakyembe wanasubiri sana kwa huyo mtu and they "pay tribute to muhongo" for his c.v
 
Anafaa zaidi kuwa Mkuu wa Chuo period. Arrogance ktk siasa ni hatari sana hata kama unafanya mambo mazuri ambayo kimsingi ni wajibu.
Arrogance? Magufuli is even more arrogant than Muhongo!
 
Habari Wanajamvi,

Naomba nianze kwa kwa kukiri niko upande wa Mabadiliko, upande unaoamini katika Upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa gharama nafuu, Nachotaka Serikali inifanyie ni Kunipa maji safi na salama, matibabu, miundombinu, elimu bora nakadhalika sihitaji Zaidi.

Takribani miaka 54 ya uhuru sasa nchi yetu imekua ikitegemea Kilimo kama uti wa mgongo, baada ya kufa kwa mazoa ya Biashara na Vyama vya ushirika kilibaki kilimo cha mkono kisicho na tija kilichoweza kukidhi mahitaji ya chakula cha ndani, Sera mbalimbali zinatengenezwa kwa awamu zote zikiwa na lengo la kufanya mapinduzi ya kilimo, sera ya “KILIMO KWANZA” ikiwa imeshika hatamu na dhamira ya dhati ya kufanya mabadiliko ya kilimo.

Tofauti na matarajio ya wengi, kilimo kinanufaisha matajiri wachache wanaoamua bei ya mazao nchini jukumu ambalo lingefanywa na wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushikirikiana nia wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika, kwa kushirikiana na wadau husika serikali inapaswa kufanya tafiti za mazao yenye soko na yanayokubali mazingira yetu lakini kubwa zaidi ni soko la uhakika na bei halisi(ikiwezekana taaasisi za Serikali ziwe mawakala wa mazao yetu- Government should own major means of Production (Basics), tofauti na ilivyo sasa wafanyabiashara wenye asili ya kiasia ambao wanamiliki uchumi wa Nchi kuamua bei za pembejeo na bei za mazao Mf. Quality Group, Mohamed Enterprises,, Fidal Hussein, Murzal Group, Wachina,etc . Wafanya Biashara hawa wana nguvu sana, iko wapi ile Skendo kubwa ya sukari aliyotamba nayo ZItto Kabwe? Hu ndio ukubwa wa nguvu yao wanafikia hatua ya kubadilisha mawaziri.

Wote tunashuhudia Uchumi wa Tanzania ukibadilishwa na Neema ya Madini na Nishati, ugunduzi wa Gas, Uranium, Oil, Gypsum, Chuma na menngine kama hayo unaifanya Tanzania kua Tishio kwa Ukanda wa Africa siku za Usoni.

Ustawi wa sector hii unategemea na aina ya mikataba na usimamizi ambao untafanywa na serikali katika hatua za awali. Kwa mfano Intergration ya TPDC ni muhimu sana ili kuleta professionalism katika sector nyeti hii ambayo hatuna uzoefu nayo, yenye risk kubwa ya kimazingira na uwekezaji mkubwa.

Nisingeshangaa wawekezaji wa kihindi (Local Indians) kutoshinikiza Muswada wa Gesi na Mafuta bungeni kwa hati ya dharura ilihali ndo ilikua dhumuni kubwa la kuratibu safari ya mkuu wetu kule India.

Sector hii imevutia wawekezaji ambao tayari wameigawana Mtwara, Tanga, lindi na maeneo yote potential nchini.Kuna Shinikizo kubwa kutoka nchi za Mashariki ya kati, America, Ulaya, China, IMF, WorldBank na taasisi nyingine za kifedha za kuhakikisha wanatumia wakati huu wa uchaguzi kuinfluence mtu atayelinda maslahi yao.

Ulishawahi Kumfikiria Prof. Sospeter Muhongo kama PM wa Tanzania?
Mtaalam huyu ambaye wote hatuna shaka na Elimu na utaalam wake katika masuala ya Miamba na Madini, Ndie anayetajwa kuongoza Tanzania wakati tunaelekea mapinduzu makubwa ya kiuchumi.

Hakuna Shaka mtaalam huyu kada wa muda mrefu wa CCM ambaye ni Vice president for Commisioning of the Geological Map of the World, aliyewin Awards nyingi duniani za Geologia ndio mwenye CV inayovutia kuliko Mwanasiasa au naweza kusema mtu yoyote Tanzania katika Masuala ya Geologia.

Kada huyu, aliyeingia CCM kama vijana wengine alipata upinzani mkubwa toka alivyoingia madarakani Mei 2012, juhudi za makusudi zinafanywa ili kubeza jitihada zake katika Wizara ya Nishati na Madini.

Kundi linalobeza utendaji wake kwa maslahi ya wafanyabiashara wanaotaka kutumia Ujanja ujanja kufaidika. Kulikoni mtu mmoja kumiliki neema hiyo ni bora Serikali isigawe vitalu kwa wazawa, Serikali iwe Shareholder wa andalau 25% ili keki hii tuifaidi wote.

Kundihili linatumia hoja dhaifu kwamba Muhongo hakua mbunifu yale yote aliyoyafanya katika Wizara hiyo kama kusambaza umeme vijijini kwa bei nafuu, kukagua makampuni ya uchimbaji madini, Mtambo wa kinyerezi, Mfuko wa Madini na mengine mengi yalibuniwa na waliomtangulia.

Kwangu hata kama ni kweli, tunahitaji anayesimamia na kutekeleza, “katiba yetu bado ni nzuri kama tutaifata na kuitekeleza”

Ni Prof. sospeter Muhongo aliyesafishwa na State House kuhusiana na kashfa ya Escrow, hii ni moja ya hatua za kumpa uhalali wa kushika Madaraka Makubwa Nchini.
Tujiulize.

Kama unampigia Chapuo Lowassa kuwa Raisi wa Nchi hii ni nani anaweza kukebehi Muhongo kuwa PM?

Je, unadhani ni nani Mwenye sifa Zaidi ya Muhongo?

Karibuni,
Wenu,

Batili.
Dakawa.

Tatizo ni CHAMA ndugu yangu!
 
Tatizo ni CHAMA ndugu yangu!

Prof.Lipumba kaacha Contradiction, kasema tatizo ni mfumo, lakin at the same time kasema tatizo ni watu wanaopokelewa kutoka CCM.

Mchungaji kushika Qouran tukufu na kuhubiri masheikh.
Tatizo ni methodology ya kumpata mgombea, tatizo sio Lowassa tatizo ni Mbowe.
 
Muhongo is good, kama akipewa anaweza, kasoro zipo za kibinadamu, ila EL mhh majanga hafai kabisa hata udiwani mana mrafi

Prof. Muhongo need to learn something out of his proffesional-Politics,
Mengi anamiliki vitalu 59 vya madini sawa na 3,752.37 (sq km) ameshindwa kuziendeleza ataweza Gesi, wafanyabiashara wa Tz hawana uwezo wa kufanya biashara hiyo, msipende kuongopewa.
 
Anafaa ila wampeleke Tution ya siasa, mambo ya kutukana Billy Gates wetu kwamba wana uwezo wa kutengeneza juice tu si vizuri. Mh. Mengi na Bakressa ni role model wetu sababu utajiri wao wameupata kwa kujishughulisha si urithi wala Ufisadi.
 
Back
Top Bottom