Ulipokuwa una umri wa miaka 10 ulikuwa unaweza kufanya kazi gani za nyumbani?

Katkit

JF-Expert Member
Mar 12, 2023
1,893
4,593
Poleni na mihangaiko ya hapa na pale.

Kama title inavyosomeka hapo juu, hebu tueleze kipindi una miaka 10 uliweza kufanya kazi za nyumbni au ndo ulikuwa bado unashikiwa fimbo kwenye kula?

Binafsi katika umri huo nilikuwa tayari nimeshafundishwa kazi zote za nyumbani na Bi. Mkubwa, nilikuwa naweza kupika, kuosha vyombo, kufua, kufanya usafi wa nyumba, kupiga pasi na kama ningekuwa nimekulia kijijini basi hata kulima ningekuwa naweza kudadeki.

Nimeandika huu uzi kwasababu naona watoto wengi wa siku hizi wenye umri huo, hawawezi kufanya chochote zaidi ya kusoma na kucheza tu, imagine mtoto wa kike mwenye umri huo hawezi hata kuprocess chai!

THIS IS JOKE!!!! Mdogo angu wa mwisho yupo na miaka 11 sasa lakini hata kufua soksi zake za shule hawezi, kila kitu anamtegemea Bibi amfanyie.

Najua hata humu mpo wengi ambao kwenye age hiyo mlikuwa ni tegemezi kwa kila kitu pengine hata kujikojolea kitandani mlikuwa hamjaacha bado PUMBAVU ZENU.

Haya shusheni mapovu yenu hapa.👇👇👇👇👇
 
Nilikuwa nauwezo wa kulima nguo, zangu nilikuwa nauwezo aa kuzifua kasoro nguo ngumu kama mablanketi nk.
 
Nilikuwa naweza fua nguo zangu na kufagia uwanja . Nguo zilikuwa zinafubaa, kuchota maji. Kupika nimeanza darasa la 6
 
Hapo kwa shangazi enzi hizo
1.Nikiamka asubuhi kwanza kutandika kitanda
2.Kufagia uwanja(niligaiwa kipande changu)
3.Nikitoka shule kufua shati na soksi
4.Nikila naosha vyombo vyangu
5.Kulikua na mbwa flan hivi jion lazima niwawekee mazingira ya msosi(wapikaji ni wengine)
6.Kukaa dukani kusaidia kazi

mwanzo niliona kama ananionea flan nilikua na ratiba ngumu nafasi ya kucheza ilikua ndogo ila Asante sana alinifundisha jinsi ya kujisimamia.
 
Nami nilikuwa naweza kazi zote za nyumbani,nilishaanza kuwachakata mbususu kila dada wa kazi aliyewahi kufanya kazi home.
Nilishaanza pia tabia ya udokozi wa pesa kabatini za kwenda kutumia shuleni.umri huo pia nilishakuwa na marafiki wavuta bangi ingawa mimi sikuwahi kuvuta.

Umri huo tayari nilishakuwa maarufu upande wa michezo hasa soka,nilifahamika kwa kila aliyewahi kunitizama nacheza mpira waliniita edibily lunyamila.

Upande wa kuzichapa ngumi sikuwa nyuma pia,nilikuwa natembeza vichapo si haba,huku waliniita bruce leee kutokana na umbo langu la Jembamba mifupa mitupu.

Sijui nyota yangu ilipotelea wapi *****...
 
Zote,Kasoro kusonga ugali imechukuwa muda kuweza kwasababu kwetu tulikuwa tunaishi timu enzi hizo,
 
Nami nilikuwa naweza kazi zote za nyumbani,nilishaanza kuwachakata mbususu kila dada wa kazi aliyewahi kufanya kazi home.
Nilishaanza pia tabia ya udokozi wa pesa kabatini za kwenda kutumia shuleni.umri huo pia nilishakuwa na marafiki wavuta bangi ingawa mimi sikuwahi kuvuta.

Umri huo tayari nilishakuwa maarufu upande wa michezo hasa soka,nilifahamika kwa kila aliyewahi kunitizama nacheza mpira waliniita edibily lunyamila.

Upande wa kuzichapa ngumi sikuwa nyuma pia,nilikuwa natembeza vichapo si hapa,huku waliniita bruce leee kutokana na umbo langu la Jembamba mifupa mitupu.

Sijui nyota yangu ilipotelea wapi *****...
🤣🤣🤣We bangi ulivuta banah 🤣 ucheze mpira,ukae na wavuta bhange afu usivute 🤔
 
We bangi ulivuta banah ucheze mpira,ukae na wavuta bhange afu usivute
Mama yangu angenitoa roho sikuwahi kuthubutu.hao friends zangu wawili waliishia jela miaka 30( uporaji wa kutumia silaha SMG)
Kuna mmoja ni kichaa ,wengine hata sijui wapo wapi.

Malezi ya mama (single mother) yalikuwa bora.
 
Ahhh si wanawatukana masingo maza huku jf kila leo,kwamba hawana malezi,basi wewe ulibahatika🤔
 
Swali lako limenikumbusha sista angu wa mwisho alivyokua by that age.

Sisi wengine wote by 10yrs tulikua tunajua kazi zote mpaka kulima ila huyu alikuja kivyake.

Huyu bibie alikua hapendi kazi za nyumbani hasa za jikoni na mpaka kawa mtu mzima ila hapendi wala hajui kupika vizuri.

Maza alichapa sana ila haikusaidia.Maza alikua akimwambia "Ukikua utakua na maisha ya shida sana sbb ya uvivu wako" dogo alikua anasema "nitahakikisha nakua na hela nyingi niwalipe watu wanifanyie kazi zangu".

Akiwa la nne,familia nzima ndo tulijua kuwa dogo ni mvivu wa manual work ila kichwa cha fursa ya pesa anacho.Dogo alimuomba maza amruhusu awe anauza maembe mabichi kwa wahindi anaosoma nao.Dogo akaelezea vizurii mpango mzima utakqvyokua bila kuathiri masomo yake.Maza akamkubalia.Biashara ya dogo ilikua mpaka ikavuka mipaka ya shule na ikabidi maza na yeye aingie kufanya.Na kuanzia hapa sista ikawa ni biashara to biashara mpaka level za kwenda maulaya.

Hapa tunapoongea sista angu huyo anaishi maisha aloyatabiri akiwa la nne.Maisha ya kuwa na hela ya kumudu kuajiri hata Italian au Thai chef ampikie akitaka.Maisha ya kufanyiwa kila kitu ambacho toka mdogo hapendi kufanya.
 
🤣🤣🤣Ewahh hapa umenigusa Kabisaa, mule mule
 
Back
Top Bottom