Ulipataje mtaji?

Ulipataje mtaji?

Head Gelo

Senior Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
122
Reaction score
210
Wakuu habari zenu
Kwa wale wafanya biashara, mliofanikiwa kutoboa kimaisha hebu tupeane uzoefu yamkini stori yako inaweza kunitoa hatua moja kwenda nyingine.

Mbali na kuajiriwa mimi napenda sana biashara yani biashara ipo kwenye damu kiukweli ila suala la mtaji wa kuanzia hasa ukizingatia frem zimekuwa juu sana limekuwa changamoto kwani kuna majukumu mengine ambayo lazima nayo ufanye.

Alafu naona wafanya biashara ndo watu wanaotamba kimaisha (hali nzuri) , wasomi tumetupwa mbali si maprof si wale wa kawaida

Wale wafanya biashara tuambizane ulianzaje na ulipataje mtaji????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa huo mtaji usiotosha ulionao unafanya biashara gani tuanzie hapo. Kama kweli iko kwenye blood
 
Mimi nafanya biashara ndogo ya nguo za kike,pazia, nguo za ndani taulo heleni na mambo yanayofanana na hayo

Ila ndoto yangu haiko hapo kabisa, ndoto yangu ni kuwa na duka la vifaa vya ujenzi au pharmacy ila mtaji sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera Head Gelo mimi kwa uzoefu wangu wa biashara zangu zote ukuaji wake kutoka kuwa ndogo hadi kubwa huwa unakuwa kwa process na unakukuta ukiwa ulishaanza na sio kwamba upate mtaji ndo uanzishe kwahyo so far uko kwenye raiti track. Hongera
 
Tatizo ni kwamba aina ya biashara ambayo naitamani ni kama uwezekano wa kuanza mdo mdo ni mdogo, mfano vifaa vya ujenzi au phamarcy, hizi lazima uwe na frem ambayo gharama yake is not less than 300k, kwa jinsi ambavyo dawa na hizi materials zipo naanzaje taratibu? Msaada
Hongera Head Gelo mimi kwa uzoefu wangu wa biashara zangu zote ukuaji wake kutoka kuwa ndogo hadi kubwa huwa unakuwa kwa process na unakukuta ukiwa ulishaanza na sio kwamba upate mtaji ndo uanzishe kwahyo so far uko kwenye raiti track. Hongera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaji wa kwanza ni matumizi bora ya akili yako.
Hapa ninamaanisha ni lazima ukubali maisha yako ili uweze kubaki kuwa kuwa wewe(usiige au kutamani maisha yasiyo yako.

Mtaji wa pili ni nidhamu,uaminifu na uadilifu.
Vijana wengi hatuaminiki na hii hutuondolea kutokubalika ktk jamii.Mafanikio ni hatua na ni lazima uzifuate.Kuvuka hatua moja kunasababisha kuikosa nyingine.
Unapopewa dhamana ya kitu,hiyo ni fursa kitendee haki kwa kufanya kadri uwezavyo kukifanikisha ili kumuwezesha aliyekupa kufikia malengo yake.
Unapofanya hivyo,Wewe binafsi unajifunza lkn pia unajijengea soko na kujiamini hivyo utaweza kupata UTHUBUTU wa kuwa na cha kwako.Wakati huohuo tayari uliyemfanyia kazi anabaki kuwa mdhamini kwa unachotarajia.
Mtaji wa tatu ni kupenda kufanya kazi. Usipende kuitwa bosi wakati mradi wako haujafikia nafasi ya kulipa watu.
Fanya unachokijua na ktk hatua ya awali kifanye mwenyewe kubana matumizi na pia kutambua changamoto zake
Mtaji wa nne ni subira.
Hili ni muhimu ktk kufikia mwisho
IMG_20190409_085057.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta sehemu zenye watu wengi hasa wapangaji wengiwengi wa hali ya chini ufungue banda la matunda ya kila aina na mbogamboga kisha uache usharobaro nyumbani, kaa kwenye kibanda chako mpaka watu wakuzoee huku ukikatakata mboga za wale wanaopenda kukatiwa.
Kama mtaji wako ni mkubwa kidogo weka na sigara, kama una msaidizi weka na mihogo hapo nje ile mizuri iliyokaangwa vizuri.
Kama una nguvu weka na friji yako uwe na soda za baridi, maji, na vinywaji vingine watakavyokuwa wanahitaji wateja

Nilishamiliki hela nzuri tu na kazi mara ghafla nikafilisika ila kilichoniokoa ni genge la matunda+viroba+mafuta ya taa +bigG+soda +banana na bia kama cret 2.

Nilinyanyuka haraka sana maana nilikuwa nikienda sokoni nikachukua matunda ya 25,000
Nyanya za 30,000
Vitunguu vya 3,000 au 7,000
Membe kidogo na mboga mboga nilikuwa napiga karibia faida pasu kwa pasu.

Ilikuwa kila baada ya siku 2 au 3 narudi sokoni na baiskeli langu,,,, hata mwaka haukuisha nikajikuta nimenunua toyo mpya ya kuendea sokoni

Kiufupi ikiwa na banda lako sehemu nzuri unaweza kuweka mtaji wa laki 5 ukaingiza faida ya laki tisa kwa mwezi hadi milioni na chenchi.

Cha muhimu usikurupuke! Za kuambiwa changanya na za kwako
 
Hili ni muhimu ktk kufikia mwishoView attachment 1068882

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana kwa ushauri mzuri.

Kubwa ambalo nimelichukua moja kwa moja ni hili la HATUA, kuna hatua lazima uzipitie

Ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta sehemu zenye watu wengi hasa wapangaji wengiwengi wa hali ya chini ufungue banda la matunda ya kila aina na mbogamboga kisha uache usharobaro nyumbani, kaa kwenye kibanda chako mpaka watu wakuzoee huku ukikatakata mboga za wale wanaopenda kukatiwa.
Kama mtaji wako ni mkubwa kidogo weka na sigara, kama una msaidizi weka na mihogo hapo nje ile mizuri iliyokaangwa vizuri.
Kama una nguvu weka na friji yako uwe na soda za baridi, maji, na vinywaji vingine watakavyokuwa wanahitaji wateja

Nilishamiliki hela nzuri tu na kazi mara ghafla nikafilisika ila kilichoniokoa ni genge la matunda+viroba+mafuta ya taa +bigG+soda +banana na bia kama cret 2.

Nilinyanyuka haraka sana maana nilikuwa nikienda sokoni nikachukua matunda ya 25,000
Nyanya za 30,000
Vitunguu vya 3,000 au 7,000
Membe kidogo na mboga mboga nilikuwa napiga karibia faida pasu kwa pasu.

Ilikuwa kila baada ya siku 2 au 3 narudi sokoni na baiskeli langu,,,, hata mwaka haukuisha nikajikuta nimenunua toyo mpya ya kuendea sokoni

Kiufupi ikiwa na banda lako sehemu nzuri unaweza kuweka mtaji wa laki 5 ukaingiza faida ya laki tisa kwa mwezi hadi milioni na chenchi.

Cha muhimu usikurupuke! Za kuambiwa changanya na za kwako
Hii nayo nimeipenda asante kwa ushauri kaka,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaji wa kwanza ni matumizi bora ya akili yako.
Hapa ninamaanisha ni lazima ukubali maisha yako ili uweze kubaki kuwa kuwa wewe(usiige au kutamani maisha yasiyo yako.

Mtaji wa pili ni nidhamu,uaminifu na uadilifu.
Vijana wengi hatuaminiki na hii hutuondolea kutokubalika ktk jamii.Mafanikio ni hatua na ni lazima uzifuate.Kuvuka hatua moja kunasababisha kuikosa nyingine.
Unapopewa dhamana ya kitu,hiyo ni fursa kitendee haki kwa kufanya kadri uwezavyo kukifanikisha ili kumuwezesha aliyekupa kufikia malengo yake.
Unapofanya hivyo,Wewe binafsi unajifunza lkn pia unajijengea soko na kujiamini hivyo utaweza kupata UTHUBUTU wa kuwa na cha kwako.Wakati huohuo tayari uliyemfanyia kazi anabaki kuwa mdhamini kwa unachotarajia.
Mtaji wa tatu ni kupenda kufanya kazi. Usipende kuitwa bosi wakati mradi wako haujafikia nafasi ya kulipa watu.
Fanya unachokijua na ktk hatua ya awali kifanye mwenyewe kubana matumizi na pia kutambua changamoto zake
Mtaji wa nne ni subira.
Hili ni muhimu ktk kufikia mwishoView attachment 1068882

Sent using Jamii Forums mobile app
Hill ni jengo la shule ya awali na msingi ninayoimiliki sasa lkn wakati ninaianzisha sikuwa na hata shilingi moja.
Safari ya kumiliki shule ilianza miaka 20 iliyopita lkn kwa hatua.
Mimi ni Mwl wa masomo ya Chem na Bios.Sikuwahi kuwadanganya wanafunzi wangu na nilihakikisha wsnafanikiwa kufaulu na kimaisha kwa kuwashauri ktk kujisonea.
Hiyo ilinipa solo nikapata Ualimu Mkuu shule ya awali na msingi ambapo pia nilifanya kazi kwa bidii,kujiheshimu na kwa uadilifu mkubwa.
Nilifanikiwa kuanzisha yangu baada ya kuamini kuwa ninakubarika na idadi kubwa ya wazazi.
Nilikutana na matatizo mengi lkn nilibaki na imani kuwa ninaweza.
Jamii ilikubali kazi yangu ns wapi walionichangia pesa ,vifaa na hata ufundi.
Kufanikiwa ni jambo zuri lkn lialopitia ktk njia mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaji......
Kuna mitaji miwili mikubwa ambayo Watanzania hawana.
1. Mtaji wa wazo la biashara
2. Mtaji fedha na elimu ya kukuza biashara
Elimu tunazo shida ni matarajio makubwa bila kujitazama nafasi zetu.
Huwezi kutaka kazi ya ofisini wakati haipo.Tuache kujipa thamani zisizo zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hill ni jengo la shule ya awali na msingi ninayoimiliki sasa lkn wakati ninaianzisha sikuwa na hata shilingi moja.
Safari ya kumiliki shule ilianza miaka 20 iliyopita lkn kwa hatua.
Mimi ni Mwl wa masomo ya Chem na Bios.Sikuwahi kuwadanganya wanafunzi wangu na nilihakikisha wsnafanikiwa kufaulu na kimaisha kwa kuwashauri ktk kujisonea.
Hiyo ilinipa solo nikapata Ualimu Mkuu shule ya awali na msingi ambapo pia nilifanya kazi kwa bidii,kujiheshimu na kwa uadilifu mkubwa.
Nilifanikiwa kuanzisha yangu baada ya kuamini kuwa ninakubarika na idadi kubwa ya wazazi.
Nilikutana na matatizo mengi lkn nilibaki na imani kuwa ninaweza.
Jamii ilikubali kazi yangu ns wapi walionichangia pesa ,vifaa na hata ufundi.
Kufanikiwa ni jambo zuri lkn lialopitia ktk njia mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeipenda stori yako na hapa kuna la kujifunza, nikupongeze sana kwa hatua hii, naamini kila kijana akichukua hii sprit tutafika mbali

Asante ndg.
Ninawausia vijana wenzangu.Ni lazima tutumie mitandao kujifunza.Tusiige maisha ya watu tunaofikiri wamefanikiwa bila kujiuliza wanefikaje.Mawazo yetu yajielekeze kutafuta pesa.
Tajiri hahesabiwi kwa pesa alizotumia bali kwa pesa alizohifadhi.
Wewe huna lkn ukipata unamuiga matumizi badala ya kuhifadhi huku ukitaka unfikie itawezekana kweli!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom