Binafsi nina uzoefu wa kazi ya unasihi (Psychotherapy/Counseling) kwa miaka minne, miaka 2 baada ya chuo nilipata kazi kupitia kujitolea zahanati moja hivi, nafasi zilitoka za shirika fulani hivi nika apply nikapata kazi ya mkataba wa miaka 2, ilivooisha hiyo nikaiingia mtaani, nachojikubali ni kuwa siogopagi kuingia ofisi yeyote ile ila bahati pekee niliyonayo ni kukubaliwa kwa nafasi za kujitolea, sijabahatika kuomba nikapata kazi full.
Kuanzia mwaka jana mwezi wa 10 nilienda radio station moja ya kidini hapa Dar nikaomba kazi ya kutoa maudhui ya afya ya akili na saikolojia wakasema hawawezi kunilipa, ikabidi niombe kufanya bure ila nikubaliwe kutoa namba zangu, wakakubali, nikapewa kipindi cha saa 1. Miezi kadhaa baadae upande wa TV yao wakanihitaji pia na wao hawanilipi ila sasa nimeamua nifanye bali namba za simu zangu ndo zitanisaidia kupata wateja na ninafanya hivo, hapo TV wamenipa ½ saa naamini ipo siku itafika nitatoboa maana kwa sasa nimeanza kuwa maarufu fulani hivi.
Nashukuru kupitia kujitolea napata chochote kutokana na huduma.nayotoa kwa wateja wangu.
Bado natafuta kazi huku nikijitafuta nijiajiri mwenyewe kama Professional Psychosocial & Psychological Mental Health Counseling Psychologist. Niwe na ofisi yangu kuliko kuwafata wateja makwao!
Kama kuna mtu anahitaji mtu wa namna yangu nipo hapa, iwe private hospital, school, college, NGOs etc.