Ulipambanaje na stress za kuachwa na mwanamke umpendaye?

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Zamani nilikuwa napenda kama kuku bwenge, nikimpenda mwanamke nilikuwa sisikii wala kuona. Nilikuwa naomba msamaha kwa kosa ambalo sijafanya mimi ili kulinda upendo wangu. Nilikuwa masta wa kuonga sana, lakini pamoja na kupenda hivyo sikuwahi kumpata mwanamke ambaye alikuja kunipenda na kunijali kama huyu ex valantine wangu.

Huyu alinipenda na kunijali sana, na toka tuachane sasa hivi tuna miaka 3. Cha kusikitisha toka tuachane nimekuwa mwanaume ambaye nina mapenzi ya uongo kwa wanawake wengine. Yaani nimejikuta sipendi tena kwa dhati. Ninajaribu kujilazimisha kupenda moyo unakataa.

Sijui wenzangu hali hii inawapata na ninyi pale mnapo tengana na wapenzi wenu ambao mliwapenda kwa dhati?

Kama ndiyo, mlipambanaje na hali hii mpaka kuja kwenye hali yenu ya kawaida?
 
Sina la kukushauri kwasababu sina experience ya kuachwa na mwanamke ktk maisha yangu ya mahusiano. mimi ndio huwa nawaacha halafu wakikaa baada ya muda huwa wao wenyewe wanaanza kunitafuta.
 
Pole sanaaa.
Ila umekuwa mbinafsi sanaa kama baada ya miaka 3 umeshindwa kumuacha aende na bado ukaendelea kuanzisha mahusiano mapya!

Unatakiwa kwanza utambue huyo sio wako tena,hiyo sio kwakuambiwa jiambie mwenyewe,pia amua kujisamehe pale ambapo unaona ulikuwa sababu ya kukatisha mahusiano yako.
Embu jaribu kufikiria tu,hao unaowapotezea muda wao na wanakupenda kwa dhati,nao wakigundua huwapendi bali unataka kuwatumia hiyo chain ya roho kama yako itafika wapi na tunawezaje kuwa na jamii bora mbeleni?

Kama unamwamini Mungu,muombe msamaha,mwambie ni kwa namna gani umeumiza wengine kwa ubinafsi wako na muombe akusaidie kubadili njia yako,huku nawe ukiendelea kujijenga kiimani zaidi.

Unaweza ikiwa utawafikiria wengine kwanza,kwamba nao wanahitaji upendo wa kweli na wadhati.
All the best
 
Mkuu ni kukubali tu kuwa muda umeisha basi unaendelea na maisha. Me niliachwa kwa sababu za kijiingaa mnooo tena mnoo hata hazina mashiko.

Ila nkajua tu muda sio rafiki so kila mtu akapata mpenzi wake na maisha yakaendelea fresh tu.
 
Cha kusikitisha toka tuachane nimekuwa mwanaume ambaye nina mapenzi ya uongo kwa wanawake wengine. Yaani nimejikuta sipendi tena kwa dhati. Ninajaribu kujilazimisha kupenda moyo unakataa.
Usisikitike mwanetu hapo shangilia tu

Hapo ndo uko sahihi hawa viumbe usiwapende kwa dhati wala usiwakabidhi moyo endelea hivyohivyo na mapenzi ya uongo

Wewe tongoza, wadanganye, chilimba, sepa. Utaenjoy nakwambia
 
Zamani nilikuwa napenda kama kuku bwenge, nikimpenda mwanamke nilikuwa sisikii wala kuona. Nilikuwa naomba msamaha kwa kosa ambalo sijafanya mimi ili kulinda upendo wangu. Nilikuwa masta wa kuonga sana, lakini pamoja na kupenda hivyo sikuwahi kumpata mwanamke ambaye alikuja kunipenda na kunijali kama huyu ex valantine wangu.

Huyu alinipenda na kunijali sana, na toka tuachane sasa hivi tuna miaka 3. Cha kusikitisha toka tuachane nimekuwa mwanaume ambaye nina mapenzi ya uongo kwa wanawake wengine. Yaani nimejikuta sipendi tena kwa dhati. Ninajaribu kujilazimisha kupenda moyo unakataa.

Sijui wenzangu hali hii inawapata na ninyi pale mnapo tengana na wapenzi wenu ambao mliwapenda kwa dhati?

Kama ndiyo, mlipambanaje na hali hii mpaka kuja kwenye hali yenu ya kawaida?
Ni rahisi sana kumsahau, jifunze kumpenda, kumzingatia na kutazama mazuri ya uliye nae.
 
Mkuu, fanya shughuli zako, tafuta sana hela, mambo ya kupenda na kupendwa waachie teenagers, wewe tumia hela maliza haja zako sepa, usipende kuweka vibanda au kambi.
 
Dawa ni kupata chuma kingine kikali kuliko kile cha mwanzo kisha jimalize ila hakikisha km alikua na mattercall makubwa basi mtafute tandamu kuzidi yule uliekua nae awe na mattercall makubwa zaidi ya yule wa mwanzo alafu acha kuhonga,.

Nakuja..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom