Habari wana JF,
Mitaa ya mingi ya kata ya Azimio na Tandika wilaya ya Temeke kuna zoezi la ulinzi shirikishi limeanzishwa. Kila mwananchi inabidi alinde japo siku moja kwa wiki. Ulinzi unaanza saa moja kamili usiku hadi saa kumi na moja na nusu asubuhi.
Kuna vikao kama viwili walikaa wananchi na mwenyekiti wa serikali ya mtaa kujadili swala la ulinzi shirikishi kikao kilihudhuliwa na OCD na mkuu wa upelelezi wa Temeke.
Wananchi walieleza hoja nyingi hasa ugumu wa zoezi lenyewe la kulinda. Ukizingatia muda uliopangwa na aina ya shughuli za watu. Kwa kifupi watu hawakulipokea vizuri swala.
Majibu kutoka kwa OCD na mkuu wa upelelezi ni kwamba lazima wananchi wajilinde wenyewe. Na ni sheria iliyotungwa na manispaa mwaka 1982.
Watu ambao hawajashiriki ili zoezi wameshapelekwa mahakama ya wilaya Temeke, adhabu yao ni faini ya shilingi elfu hamsini (50,000) au jela miezi sita.
Inasemekana swala la wananchi kujilinda wenyewe alilianzisha Mh. Augustine Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani miaka hiyo.
Kulikuwa na kikundi cha ulinzi (sungusungu) ambao walikuwa wanalipwa kila mwezi na wananchi. Kikundi kimevunjwa na viongozi wa serikali za mitaa na kulazimisha wananchi waanze kulinda.
Hili swala limekuwa ni kero kubwa kwa wananchi sasa hivi, watu wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu ya kulazimishwa kukesha kujilinda. Wananchi wanakamatwa kutoka katika majumba yao kwa kutokulinda na kupelekwa mahabusu halafu mahakamani na kulazimishwa kulipa faini au kwenda jela miezi 6.
Polisi kituo cha chang'ombe Temeke ndo wasimamizi wakubwa wa zoezi hili.
Wana JF hivi hili swala liko kweli kisheria? Vipi wilaya zingine za Dar Es Salaam kuna zoezi hili pia?
Mwenye nakala ya hiyo sheria naomba atuwekee hapa!