Ulinganifu wa muundo na utendaji wa tume ya uchaguzi ya Afrika ya kusini [IEC] na [NEC] ya Tanzania

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
ULINGANIFU WA MUUNDO NA UTENDAJI WA TUME YA UCHAGUZI YA AFRIKA YA KUSINI [IEC] NA TANZANIA [NEC&ZEC]:
126c59fd-09df-45f2-a5a7-58ba41aea88d.jpeg

SEHEMU YA KWANZA:

Na. Mbarala Maharagade

Vyama vya CUF, CCM na CHADEMA pamoja na vyama UNITA, MPLA, CASA CE, kutoka [ANGOLA], UDC(BNF) [BOTSWANA], DPP, MCP, PP, kutoka [MALAWI], RENAMO, MDM, [MOZAMBIQUE], PF, UPND, FDD, kutoka [ZAMBIA], na DA-SOUTH AFRICA, wiki iliyopita August 20-24, 2018 vilipata fursa ya kualikwa na kushiriki katika kongamano lililoandaliwa na NDI's Political Parties Strengthening Institute with Collaboration of UNDP lenye madhumuni ya Uimarishaji wa Vyama vya siasa kuendana na siasa za karne ya ishirini ya moja zilizobeba maudhui makuu 3 ikiwa ni TAFAKURI (Reflect), MABORESHO (Reform), KUSHIRIKISHA (Re-Engage)

REFLECTING: [THE STATE OF POLITICAL PARTIES IN THE 21ST CENTURY]
REFORMING: [21ST CENTURY POLITICAL OPERATIONS]
RE-ENGAGE: [DEVELOPING RE-ENGAGEMENT STRATEGIES FOR 21ST CENTURY POLITICAL PARTIES]

Mada takribani 25 ziliwasilishwa na wataalamu wa Kimataifa na washiriki walipata fursa ya kujadiliana kwa pamoja. Mada hizo ni kama zifuatavyo;
REFLECTING:
1. Building and Sustaining 21st Century Parties;
a) Global Trends Affecting Political Parties.
b) Reflections on the State of Political Parties in Africa.
c) Political Parties in Africa and the Inclusion Challenge.
d) Challenges of Youth Political Participation and Inclusion.
e) Understanding new Approaches to Internal Party Organizing.
f) Reform Goal Initiatives.

REFORMING:

2. New Models for Organizing 21st Century Political Parties;
a) New Models in Citizen Outreach for Political parties.
b) Modern political Representation.
c) Inclusion and Representation.

3. 21st Century Political Parties in Election;
a) Strengthening Party Structures at the Local Level.
b) Communication and Messaging.
c) Membership, Supporters and Voters.
d) Design 4 Democracy Initiative
e) Information Integrity and Cyber security for Political Parties.

RE-ENGAGE:
4. Developing Re-engagement Strategies for 21st Century Political Parties;
a) Political Parties and Electoral Processes in Africa.
b) Challenges Electoral Commissions face with political Parties in Africa.
c) Inclusive Electoral processes: Strengthening Women and Youth Participation.

5. Strengthening Foundations for Reform Minded Political Parties;
a) Building 21st century Political Parties: Core Components.
b) Innovations in Party Technology.
c) Identifying and Strengthening Party Leadership.

NB: Nimeziwasilisha mada husika bila kuzitafsiri ili kupunguza maneno katika makala hii.

Mgeni rasmi aliyefungua na baadae kufunga Kongamano hilo Honourable Terry Tselane. ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Afrika Kusini [Independent Electoral Commission (IEC)] ameeleza katika hotuba yake baadhi ya nukta muhimu juu ya IEC, nami kwa msaada wa taarifa kupitia mtandao [website] nimepata fursa ya kufanya uchambuzi wa ulinganifu wa Tume ya uchaguzi Afrika ya Kusini jinsi inavyopatika. Inafanyeje kazi zake. Je ni Tume Huru kweli? Vyama vya siasa vina malalamiko yeyote juu ya uwajibikaji wa TUME, uwazi, uhuru na utendaji wa wake? Fuatilia makala haya kwa kwa kulinganisha na Tume zetu za Tanzania na Zanzibar [NEC +ZEC] katika nukta 23 kama ifuatavyo;

1) Tume Huru ya uchaguzi ya Afrika Kusini [IEC] ina wajumbe 5 tu. NEC ina wajumbe 7 na ZEC ina wajumbe 7.

2) Afrika Kusini -IEC anayetaka kuwa mjumbe wa Tume atalazimika kuomba nafasi hiyo kwa kuandika maombi (Application) na kuyatuma kwa Jopo makhsusi linaloratibu uteuzi wao linalowajumuisha Rais wa Mahakama ya Katiba (Mwenyekiti) [The President of the Constitutional Court (Chair)], Muwakilishi wa Tume ya Haki za Binaadamu nchini, [Representatives of the Human Rights Commission], Muwakilishi wa Tume ya usawa wa kijinsia [The Commission on Gender Equality], na Mwendesha Mashtaka Mkuu [Public Prosecutor] like DPP in Tanzania. NEC na ZEC wajumbe wote wanateuliwa na Rais [Mwenyekiti/Makamu wa CCM] kwa kadri anakavyoona inafaa. [ZEC-wajumbe wawili atashauriana na kiongozi wa upinzani]

3) Afrika Kusini-IEC waombaji wote wanafanyiwa uhakiki na Jopo hilo hapo juu na kupeleka majina yasiyopungua 8 mbele ya kamati ya vyama vya siasa bungeni. [The inter-party committee exams a list of at least eight nominations submitted by a panel]. Tanzania hakuna mchakato huo.

4) Afrika Kusini-IEC, Kamati ya Bunge ya Vyama vya siasa inapendekeza kwa kuwasilisha Bungeni [National Assembly] majina ya wajumbe 4, Bunge likiwapitisha linayapeleka majina hayo kwa Rais [without optional] anatangaza kuwateua tu. [President on the recommendation of the National Assembly, following nominations by a National Assembly inter-party committee]. Rais hana mamlaka ya kuteua mjumbe anayemtaka. Tanzania hakuna mchakato huo na Rais anateua mtu yeyote kwa kadri anavyojisikia.

5) Afrika Kusini-IEC, kati ya wajumbe 5 wa tume mmoja lazima awe Jaji wa Mahakama ambaye nae anachaguliwa kwa kupitia utaratibu makhsusi kupitia Jopo la Majaji na jina lake kuwasilishwa kwa Rais na kumtangaza kuteuliwa kwake. Tanzania Jaji yeyote yule anaweza kuteuliwa kwa matakwa ya Rais [Mwenyekiti/Makamu wa CCM-Ruling Party] kadri atakavyoona inafaa.

HUU NDIO UMUHIMU WA KUWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI NCHINI.

SEHEMU YA PILI:
0a418412-49fc-43a0-b4a0-e71f0d234cfd (1).jpeg

ANGALIA HAPA, KUNA;
1. INDEPENDENT ELECTORAL COMMISSION-IEC (TUME HURU YA UCHAGUZI –AFRIKA YA KUSINI)

2. NATIONAL ELECTORAL COMMISSION-NEC (TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI) NA,

3. ZANZIBAR ELECTORAL COMMISSION-ZEC (TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR)

Umeona tofauti hata tu ya utambulisho wa TUME hizi?

Tuendelee na nukta ya 6 ya maudhui ya Ulinganifu wa TUME na sehemu zitakazofuata tutatoa maoni na hatua zinazopaswa kuchukulia na Serikali na au Watanzania hasa Vyama vya Siasa za USHINDANI ili kuwe na uwanja sawa wa ushindani katika UCHAGUZI. Lazima Tanzania tuwe na UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA. SIO UCHAGUZI WA MABAVU NA UDIKTETA. Haiwezekana na wala Haikubaliki Rais ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama chake apange MAREFA NA TIMU NZIMA YA KUSIMAMIA UCHAGUZI NDANI YA MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA.

Ili kuelewa vizuri makala haya soma pia sehemu yake ya Kwanza.
NUKTA YA;

6) Afrika kusini-IEC, Mwenyekiti na Makamu wake wanapatikana kwa kuchaguana wenyewe miongoni mwa wajumbe 5 wa Tume walioteuliwa. Tanzania pamoja na kuwa na wajumbe 7. Mwenyekiti na Makamu wake wote wanachaguliwa na Rais (NEC) Na (ZEC) [Kazi hiyo inafanywa na Mwenyekiti na Makamu wake (Rais wa Zanzibar- CCM].

7) Afrika kusini-IEC, mjumbe wa Tume hapaswi kuwa au kuwahi kutumikia nafasi ya juu ya kisiasa katika Chama chochote cha kisiasa. Sharti asiwe kabisa mfuasi wa Chama au awe amewahi kuwa mwanachama au kiongozi katika nafasi za chini kabisa ndani ya Chama chake au serikalini [Low Party-Political Profile] sio [Highly Party-Political Profile].

8) Afrika ya kusini-IEC, wajumbe wake wanahudumu kwa muda wa miaka 7. Inayoweza kuongezwa tena kwa kipindi kingine kwa mchakato ule ule wa kupatikana kwao kama tulivyoeleza hapo awali. Tanzania wajumbe wanadumu kwa kipindi cha miaka 5 pia inaweza ongezwa kwa kipinidi kingine cha miaka 5 kwa mchakato ule ule.

9) Afrika Kusini-IEC, Tume inasimamia Chaguzi zote. Chaguzi kuu za Kitaifa(Rais na Bunge), Majimbo na Chaguzi za serikali ya Mitaa. [To manage free and fair elections at all levels of government (The National Assembly, the provincial legislatures and the municipal councils)]. Tanzania NEC/ZEC inasimamia uchaguzi Mkuu pekee wa Rais, Wabunge na Madiwani. Chaguzi za Serikali za mitaa zinasimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Zanzibar hakuna chaguzi za Serikali za Mitaa. Kuna Shehia (Masheha) wanaochaguliwa na ………………………….

10) Afrika Kusini-IEC, inaajiri watendaji wake kwa ngazi zote toka Taifa mpaka ngazi ya chini nchi nzima, ambao hawana majukumu mengine isipokuwa ni kutekeleza majukumu ya Tume-IEC pekee. Tanzania Tume hazina watendaji wake yenyewe ambao ina mamlaka nao wa kuwawajibisha pale wanapokwenda kinyume na utendaji wao. NEC na ZEC zina wasimamizi wa uchaguzi tu walioteuliwa kwa matashi ya kisiasa na Rais Mwenyekiti au Makamu wa CCM na katika ngazi ya Halmashauri Madiwani hushiriki kuwateua Ward Executive Officer-WEO au Village Executive Officer-VEO ambao ndio huwa [Returning Officers during Elections] Marehemu Jaji Lewis Makame aliwahi kueleza kuwa analetewa watendaji ambao hana mamlaka nao na wala hajui watokako.

11) Afrika Kusini-IEC, Mjumbe wa tume ANALINDWA, hawezi kuondolewa na yeyote mpaka yapelekwe malalamiko kwa Mahakama ya Uchaguzi [ELECTORAL COURT] kisha Mahakama itoe maoni/maamuzi yake kwa kamati ya Bunge ya Vyama vya siasa, Kamati lazima imuhoji mtuhumiwa na apate nafasi ya kujitetea. Kamati iwasilishe hoja bungeni kama itabaini makosa. Na hapo kama ikibainika kosa Bunge linampelekea taarifa Rais ili amuondoe muhusika katika nafasi hiyo.

Kosa laweza kuwa kukiuka miiko ya kazi/majukumu-utovu wa nidhamu, huwezo mdogo, kushindwa kusimamia majukumu aliyokabidhiwa, [Members of the IEC may be removed for misconduct, incapacity or incompetence by the President on a resolution of the National Assembly]. Tanzania Rais au waziri mwenye mamlaka na serikali za mitaa akijisikia anaweza kubadilisha Wajumbe na Watendaji wa Tume kwa kadri anavyoona inafaa. Kwa kujisikia tu. Hakuna [Checks and Balance].


12) Afrika Kusini-IEC, Tume inapata fedha kutoka serikalini na inawajibika kwa Bunge moja kwa moja kupitia kwa waziri wa mambo ya ndani. [Publicly funded and accountable to parliament, but it remains an independent institution of the government] Tanzania Tume pamoja na kupata fedha toka serikalini inakuwa sio huru na bajeti yake inapitia ofisi ya Waziri Mkuu. fedha hutolewa na au huzuiwa kutolewa kwa matakwa ya kisiasa.


13) Afrika Kusini –IEC, ni kosa la Jinai kwa Hazina kutotoa fedha zilizopangwa na Bunge kupelekwa Tume kwa mujibu wa Mpango wa Utekelezaji uliowekwa na kupitishwa kwa mwaka husika. Tume inaomba fedha zake moja kwa moja toka Hazina. Tanzania hakuna kosa. Tume haipo huru kutekeleza mipango yake kwa wakati. Serikali uingilia utendaji wake na masuala ya fedha. Tanzania kuna Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge na kuna Bajeti ya Ikulu. Utekelezaji wa bajeti iliyoidhinishwa na Bunge unategemea vipaumbale na maagizo kutoka Ikulu.


“UMUHIMU NA ULAZIMA WA KUWA NA TUME HURU YA UCHAGUZI TANZANIA”

INAENDELEA…………. SEHEMU YA TATU.
 
Pamoja na yote hayo nilimsikia mtangazaji wa VOA akisema SA ni semi democratic country, nikajiuliza sasa sisi ni nchi ya democrasia kweli ?
 
Back
Top Bottom