Ulimwengu wa kiroho sehemu ya pili

Ulimwengu wa kiroho sehemu ya pili

Showio

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2019
Posts
254
Reaction score
482
ULIMWENGU WA ROHO
sehemu ya pili:

Katika Biblia iko elimu kubwa pengine kuzidi uwezo wetu wa kutambua na kutumia maarifa yaliyopo ndani ya Biblia Takatifu.

Elimu ya nadharia ni elimu isiyo na matendo, kujifunza kitu pasina uhalisia, yaani kupewa maelekezo juu ya maarifa flani lakini bila kuwa eneo husika la kutekeleza hayo maarifa uliyo funzwa.

Maandiko maTakatifu katika Biblia ni nadharia, ukiyasoma utapata uelewa ama ufahamu wa kuwepo kwa matendo makuu ya Mungu, lakini maandiko hayo hayakubebi kukuingiza sehemu ya matendo hayo, kwa sababu hiyo nasema Elimu iliyopo katika Biblia Takatifu ni nadharia, kwakuwa wengi husoma na kubaki nayo kama hadhiti ya kale lakini hawana namna ya kutumia Elimu hiyo Kubwa na Takatifu:

Mungu alimteua Nuhu, Ibrahimu Isaka Kisha Yakobo, katika Yakobo Mungu akatenda matendo mengi na makuu ili kwahayo aufunze ulimwengu wote.

Wakati wote huu kulikuwa na makaburi ya kumbu kumbu, Waliofariki kipindi chote hicho walilala makaburini kimiya wakisubiri ufufuo wa wafu.

Kwa mkono wa Musa, MUNGU aliandika torati, na baada ya miaka kwenda na watu kubadilika, Mungu alitumia manabii mbali mbali kuboresha Torati kwendana na wakati, ama pale watu walipo tumia vibaya sehemu ya torati ama kwa kuto kujua na kutenda dhambi, Mungu alimtuma nabii na kubadhili vivingu kadhaa ili kuwanusuru watu wake.

Ujio wa Yesu Kristo, si ili sisi tuomboleze yale aliyo pitia, wala si kazi yetu kumuonea huruma, bali tunawajibu wa kumsifu Mungu kwa hiyo ishara yake na namna anavyo okoa hata toka kuzimu.

Tukio la Yesu kufariki na kufufuka baada ya siku3, ni hitimisho na ufufuo wa wafu, na Yesu hana kumbukumbu makaburini,
Hivyo toka kufufuka kwa Yesu, hakuna tena kumbukumbu makaburini.

Biblia inatuambia Yesu alifufuka pamoja na watakatifu wengi, yaani watu wema waliyo kufa miaka mingi kabla ya Yesu, kwa Lugha nyepes ni kwamba roho zilizo shikiliwa kuzimu siliachiliwa tangu ushindi wa Masihi wa Mungu, Yesu Kristo wa nasaret.

Roho silizokuwa safi na walioishi wakimcha Mungu walipaa pamoja na Yesu, na Roho silizo tenda maofu zilibaki sikihangaika huku na kule pamoja na malaika waasi.

Tangu siku hiyo, mtu akifariki, mwili unapelekwa kaburini lakini roho inahangaika huku la kule, ikiwa mtu huyo si mcha Mungu.

Hapa ndipo chanzo cha kuwaleteeni Elimu ya Ulimwengu wa Roho, ambao umegawanyika vitengo vingi.

Kitengo cha karibu na watu wengi ni kile cha watu waliyo fariki, wengi huita mababu, ikiwa walifariki dhambini, roho zao hasitaondoka mbali na makazi yao ya awali, na wataendelea kushirikiana na watoto wao wakiwatendesha yale yale waliyo yatenda wao na yakawakozesha mbingu.

Mizimu hii huwa miungu kwa jamaa zao, na hiki ndicho kiini cha matambiko, matambiko ni kwaajili ya kuonyesha ushirikiano na hii mizimu.

Watu wengi wanakawaida hata wanapo kula, kwa bahati mbaya chakula kikamwagika, utawasikia wakisema, "wazee wangu wamekula" hii ni kudihirisha ule ukaribu uliopo kati yake na wafu, na hii ni hatari kubwa.

Sehemu ya maandiko Yesu alisema kuwa, baba atamkana mwana na mwana atamkana mama, pengine maneno haya yanaonekana mepezi lakini ni magumu,

Maana yake utakataa kazi za mababa na mababa watakukataa kwakuwa umewakataa, pili baba atamkataa mwana kwakuwa mwana atajiunga na mambo ya kigeni, ukisha mkana kuwa si mwana wako tena kwa amini ya kweli hawezi kukudhuru tena kwa mambo ya kishirikina toka ulimwengu wa giza (ulimwengu wa roho wa ibilis)

**********************************

Huu ni utangulizi ili kukupatia uelewa mzuri,
1 maisha ya ulimwengu wa roho yanakopa katika maisha ya mwili.
2 mbinu za vita na mapambano katika ulimwengu waroho yanaandaliwa ulimwengu wa nyama
3 silaha madhubuti za kivita ulimwengu wa roho zinatengenezwa ulimwengu wa mwili,

Hivyo maisha ya mwili ni msingi wa maisha ya Roho, ndipoza tunatakiwa kuishi tukijichunga sana:

Wakati ujao tutafikia hayo na kukupa maarifa makubwa
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Back
Top Bottom