Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,453
- 872,065
Je dunia inaendeshwa na roho 'mtakatifu'? Neno mtakatifu lisikuchanganye ukadhani ni ile ya kiimani. Kila kitu kina pande mbili, upande unaoonekana na upande usioonekana. Upande unaoonekana hauwezi kufanya kazi pekee ni lazima kuwe na muunganiko na upande usioonekana. Kwenye mtiririko wa kitu kinachoitwa mashine. Upande usioonekana unaitwa software, kwenye viumbe hai tunaita uhai na pumzi ama roho, kwenye vitu kama magari tunaita nishati.
Dunia inaendeshwa na nini? Yani ni kipi kinaifanya dunia iitwe ulimwengu ambapo ndani yake kuna jua mwezi na vyota visivyodondoka? Zingatia nimesema ndani yake!
Ni kipi kinaifanya dunia iwe na maji yenye mipaka? Upepo? Hewa? Majira ya mwaka, uoto wa mimea, makuzi ya viumbe, kukua kuharibika mpaka kuoza kabisa!.
Kuna nguvu isiyoonekana inayoendesha haya yote.. Kuna software yenye database ya ajabu kabisa software inayoweza kubalance kati ya vyenye uhai na visivyo na uhai, vyenye nguvu na dhaifu, vyenye kuharibu na vyenye kujenga, kwa uwiano sawia bila kuzidisha bila kupunguza
Ni nguvu hiyo ambayo nimeilinganisha na roho mtakatifu katika ukamilifu wake! Kitu chenye nguvu ya kipekee kabisa. Roho nishati inayoweza kuzi control roho nyingine zote nguvu nyingine zote hata maisha yaweze kuleta uwiano sahihi kwenye mizania ya haki.
Ndio maana watu wanaugua na kupona! Ndio maana watu wananusurika ajali, ndio maana watu wanagombana na kupatana. Ndio maana watu wanapata mahitaji muhimu kama chakula malazi nk. Ndio maana mimea inamea na kukua hadi kukomaa na kuvunwa
Kinyume chake ni nguvu hasi, roho chafu, roho ya maangamizi inayoleta majanga, vifo vita ugomvi magonjwa na kila aina ya jambo baya!