Ulimwengu ampa rais ajaye - Dr Slaa - ushauri murua

Ulimwengu ampa rais ajaye - Dr Slaa - ushauri murua

Wanajamvi:

Inaonekana safari hii RAIA MWEMA wametoka na vitu vikali – makala hii si kupitwa. Namsifu kwa kumpa Dr Slaa – anyeamini ataukwaa urais 2015 – ushauri mzuri.

Hatari ya vurugu inatoka kwa watawala, Slaa asiwape kisingizio

Jenerali Ulimwengu

KATIKA kipindi hiki tunapoikazania Serikali ya Rais Jakaya Kikwete isifanye mchezo na suala la Katiba, tunalo jukumu la kutuliza akili zetu na kupima kwa kina kila tunachokisema na kukiandika.

Nasema haya kwa sababu naona kama tunalo tatizo linalotokana na Serikali yetu kuonekana kama vile haina msimamo kuhusu suala hili kubwa na zito. Hakuna dalili za wazi zinazoonyesha kwamba Baraza la Mawaziri limeketi na kulijadili kwa undani na kupata msimamo wa pamoja, na wala hakuna dalili kwamba mkuu wa Serikali hiyo, Rais Kikwete amewapa watu wake maagizo kuhusu nini wafanya na nini waseme kuhusu mada hii ya Katiba.

Kinachojitokeza ni taswira ya kuparaganyika kwa mawazo na kutokuelewana miongoni mwa wale wanaotarajiwa kutuongoza. Kwa bahati mbaya, ingawaje sasa naamini watakuwa wamegundua kwamba walichokifikiria kuwa kitu rahisi, ni kigumu kweli kweli na wanatakiwa wajiandae kukishughulikia kwa umakini mkubwa kuliko huo walioudhihirisha hadi sasa.

Ningependa nirejee jambo ambalo nimekuwa nikilishadidia kwa muda mrefu kidogo: Suala la Katiba mpya limeshika kasi isiyokuwa ya kawaida, na wala haliwezi kuondoka kirahisi. Linahitaji kufanyiwa kazi itakayowaridhisha wananchi, na hiyo kazi haiwezekani ikafanyika ila kwa kuwahusisha wananchi kwa kiwango kikubwa kinachowezekana.

Ukweli ni kwamba, hata kama hatukuwa tumezowea hili, hivi sasa wananchi wanataka mabadiliko makubwa katika maisha yao, na wanataka kuanza na Katiba watakayoiandaa wenyewe.

Ni kwa nini wananchi wamefikia kiwango hiki cha utashi, mimi binafsi sina jibu la haraka, na kila mtu anaweza kuwa na maoni yake. Lakini naamini kwamba wananchi wengi wameanza kung’amua kwamba mambo hayaendi kama ambavyo yanatakiwa yaende.

Wanayaona maisha yao yakiwa hayana matarajio tena. wanaona hali zao za kiuchumi na kijamii zikizidi kuzorota. Wanaona maisha bora waliyoahidiwa kama ni mzaha wamechezewa. Wanawaona watawala wao kama waongo na wanafiki, wasiojali, wala rushwa na wauza nchi. Hawaamini lo lote linalosemwa na watawala kwani wamekwisha kudanganywa mara nyingi.

Sasa wamehamanika na wanataka mabadiliko, tena wanataka mabadiliko makubwa.

Nimekuwa nikifuatilia kwa kiasi fulani maandamano na mikutano ya viongozi wa CHADEMA katika mikoa ya Kusini, na nimekuwa nikiangalia maelfu ya watu wanaoshiriki katika maandamano hayo na mikutano hiyo. Ningekuwa mtawala ningeshitushwa na mikusanyiko ile kwa sababu ningetambua kwamba inabeba ujumbe mzito kwangu.

Ujumbe unaotoka katika maandamano yale na mikutano ile ni kwamba wananchi wamechoka. Ukiona kaumu ya watu kama tuliyoiona katika miji midogo na ya ‘pembezoni’ kama Sumbawanga wanaandamana na kukaa mkutanoni wakisikiliza kama watotot wa shule wanavyokaa darasani kumsikiliza mwalimu, unajua kwamba kuna kitu kimebadilika katika jamii ya Watanzania.

Lakini papo hapo ningependa kutoa angalizo. Kama nilivyowahi kuandika huko nyuma, hii si mara ya kwanza tunashuhudia hamaniko la aina hii la kutaka mabadiliko. Nimeandika kwamba tuliwahi kuona, hapa nchini, hamasa walizozua wanasiasa kama Chistopher Mtikila na Augustine Mrema wakati ule. Watu wengi waliwachukulia hawa kama wakombozi wao. Baadaye bila shaka walikuja kugundua kwamba matumaini yao yalikuwa yamegonga mwamba.

Lakini shauku ikiisha kujengeka kwamba hali iliyopo haifai na ni lazima ibadilike, shauku hiyo haiishi kwa sababu manabii waliotarajiwa kufanya kazi ya ukombozi wamedondoka kando ya njia, bali shauku hiyo huhamishwa na jukumu la ukombozi likatafutiwa manabii wengine. Na kwetu ndivyo ilivyokuwa.

Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005 shauku hiyo ilikuwa imehamishiwa kwake. Bila shaka mwenyewe atakuwa anakumbuka kwamba ilifika mahali wakati wa kampeni ndani ya CCM ikasemwa kwamba hata kama CCM wasingemchagua yeye kuwa mgombea, angepata kuwa rais kwa kupitia chama kingine cho chote. Hayo yalisemwa na wana CCM na wanachama wa vyama vya upinzani pia.

Hili nalisisistiza kwa makusudi mazima: Hizi ni dalili za kuhamanika na kukata tamaa kwa Watanzania wengi. Na hali hii imekuwapo kwa muda mrefu toka utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi hadi ule wa Rais Benjamin Mkapa. Sasa inajirudia katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete.

Wananchi wengi wanaona mkombozi wao mpya, nabii wao mpya, ni CHADEMA. Wanachosema katika lugha ya miili yao ambayo naiona kupitia televesheni na kupitia magazeti, ni kwamba wakipata fursa ya kupiga kura na uchaguzi ukawa “huru na wa haki” wanaweza (na uwezekano huo ni mkubwa) watapiga kura kuichagua CHADEMA.

Sasa, kama tunavyojua, uchaguzi mwingine ni mwaka 2015. Bado tunayo miaka minne hadi tupate fursa nyingine ya kupiga kura. Ni vyema kwa wale wanaotaka kufanya mabadiliko katika utawala wa nchi hii kwa njia mbali mbali wakautumia muda uliosalia kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi huo, na wale wanaotaka kuiondoa CCM madarakani wafanye kampeni ya nguvu ya kuwahamasisha wapiga kura kimawazo lakini pia na kuwahamasisha wajitokeza siku ya kupiga kura ili watimize azima yao.

Ndiyo maana nilijikuta nikiwa na wasiwasi (wiki chache zilizopita) nilipomsikia Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willbrod Slaa akizungumza kama vile anao mpango wa kufanya mabadiliko anayotaka kuyafanya kabla ya uchaguzi ujao. Aliposema kwamba kuiondoa serikali ya Kikwete kabla ya 2015 hautakuwa uhaini anaweza kuwa anasema kweli, kwani uwezekano huo upo.

Kwa mfano Bunge linaweza, katika mazingira mahsusi yaliyoainishwa na Katiba, likamshitaki Rais kwa kosa la kuidhalilisha Ofisi yake, na kama akikutwa na hatia likamvua madaraka. Hiyo imeandikwa katika Katiba tuliyo nayo hivi sasa, na wala halina haja ya kusubiri Katiba mpya. Ndiyo maana nasema kwamba anachosema Slaa ni cha kweli kwa maana ya vifungu vya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano kama ilivyo leo.

Kinachonitia hofu ni kwamba napata hisia kwamba Slaa hakujikita katika vifungu vya Katiba, angalau maelezo niliyoyasoma hayakusema hivyo, jambo ambalo linaweza kuzaa tafsiri kwamba njia mojawapo inayofikiriwa ni kuung’oa utawala wa Kikwete kwa maandamano, kama ilivyokuwa Medani Tahrir.

Kama hivyo ndivyo alivyokusudia kusema Slaa, kuna tatizo. Tatizo hilo, kwa mtazamo wangu, linakuwa kubwa zaidi kwa kuangalia matukio ya siku hizi chache zilizopita.

Tatizo lenyewe si kwamba haiwezekani kuung’oa utawala uliopo kupitia maandamano na bado kitendo cha kuung’oa kikawa si uhaini. Nchi nyingi zimeshuhudia hilo likifanyika, ikiwa ni pamoja na Indonesia, Philippines, Georgia na sasa Tunisia na Misri. Kilichotokea katika nchi hizo ni mapinduzi ya umma uliosimama na kusema “Utawala huu sasa basi!” Ni mantiki ya mapinduzi kama hayo kwamba yanapofanikiwa walioyaongoza wanakwenda moja kwa moja Ikulu, lakini wakishindwa wanatiwa kitanzi.

Ni kwa jinsi hii akina Fidel Castro (Cuba) na Nelson Mandela (Afrika Kusini) walikwenda jela lakini hatimaye waliingia madarakani, lakini Pierre Mulele (Kongo) na Mahjoub (Sudan) walitiwa kitanzi.

Naamini kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA alitaka kupeleka ujumbe mzito kwa wakuu wa nchi, lakini kila siku ujumbe unaohusu mambo kama haya hauna budi uandaliwe kwa uangalifu na weledi mkubwa ili usije ukazaa tafsiri zaidi ya moja.

Ingekuwa vyema kama Slaa angeonyesha subira katika matamko yake. Hivi sasa watu wengi wanamwangalia kama “rais mtarajiwa.” Angechukua muda kujiandaa kwa umakini mkubwa, hasa wa kuyasoma matatizo ya nchi yetu na kufikiria njia mbali mbali za kuyakabili kuanzia na hili la Katiba ambalo sasa naamini kwamba iwapo atachaguliwa kuwa rais mwaka 2015 ( na nasema hili linawezekana kabisa), atalikuta bado lipo kwa sababu sioni dhamira ya kweli ya kulishughulikia.

Akijipa muda wa kujifunza zaidi na kukusanya maoni, na kujenga mitandao ya utafiti itakayowahusisha wataalamu wa kumshauri na kukishauri chama chake, akichukua muda kujadili matatizo ya nchi hii na makundi mbali mbali ya kijamii katika shughuli zao mbali mbali na wakamweleza matatizo yao; naye akajadiliana nao... atakuja kugundua kwamba hakuna muda wa kutosha kwa ajili ya maandalizi hayo.

Najua mara nyingi umefanyika uchokozi dhidi ya vyama vya siasa na wanasiasa wa upinzani. Uchokozi huo unafanywa makusudi ili kipatikane kisingizio na wapinzani waweze kushutumiwa kwamba ndio waliodhamiria kuvunja “amani na utulivu” na misemo mingine ya kuchekesha ukiangalia “amani na utulivu” vinavyotawala shughuli za chama-tawala.

Kwangu ni dhahiri kwamba kama kuna ghasia kubwa zitakazotokea nchini humu, zitaanzia katika vurugu zinazoendelea ndani ya chama hicho tawala. Hata hivyo, Slaa angejiweka mbali na kila kinachoweza kumfanya yeye ama chama chake waonekane, hata kama si kweli, kwamba wao ndio wanaochochea vurugu.

Naandika haya nikijua kwamba sasa kuna hamaniko ndani ya duru za watawala, kwa sababu wanajua wamepoteza nguvu za ushawishi na wanachokiona kwamba kinaweza kuwasaidia ni ushawishi wa nguvu, kama ambavyo wanaonekana kutumia mitulinga isiyokuwa na sababu yo yote alimradi tu waonyeshe kwamba wanazo nguvu, kama vile hatujui kwamba wanazo.

Katika kutapatapa wamewaingiza na wakuu fulani wa dini ambao nao sasa wanatoa ‘onyo’ kwa CHADEMA kama vile wamegeuka kuwa idara ya usalama ya serikali au wasemaji wa Jeshi la Polisi.

Hali hii inatisha, lakini si mpya. Imetokea kila mahali utawala ulipozeeka, ukapoteza njia, ukasahau hata asili yake, ukapuyanga na kubahatisha, ukababaisha na kubangaiza, ukayumba na kutetereka, ukatekwa na waporaji, ukaendelea kujitutumua kwa kuonyesha ukali wa kijeshi kumbe ndani ya roho yake kiini chake kilikwisha kugugunwa na mapanya-buku kwa muda mrefu. Utawala kama huo unao uwezo mkubwa wa kusababisha maafa kutokana na udhaifu wake.

Slaa akae chonjo, apunguze hisia, awe m-rais (presidential). Ajifunze zaidi, kwani kama bado ana nia ya kuwania urais mwaka 2015, kazi iliyo mbele yake ni kubwa. Akumbuke tu kwamba, Rais Jakaya Kikwete alikuwa na (angalau) miaka kumi ya kujiandaa kuwa rais, na hii kumi ni ile tunayoijua sisi.

Hata baada ya muda huo wa miaka kumi kupita, na hata baada ya miaka mitano ya kuendesha Serikali, inaelekea bado hajajifunza mambo mengi ya msingi kabisa yanayohusu uongozi na utawala. Slaa afanye hadhari, asije akawa vivyo hivyo.

I bet wale wenye akili za magamba magamba hawatamuelewa Jenerali
 
]Ulimwengu katumwa na Kikwete[/COLOR]. DK. Slaa alishajifunza sana miaka kingi iliyopita. Kwanza, ninyi mnaotaka kumpa heshima huyu kibaka mnaitoa wapi? Unajua huyu akiwa mkuu wa wilaya ndiye aliyezuia mkutano wa kwanza wa mageuzi, hadi pale wanaharakati kama Mabere Marando, Ndimara Tegambage, Anthony Komu walipojitokeza na kupinmga udhalimu wake?

Wanaharakati hao waliandika waraka kwenda nchi za Magharibu na nakumbuka rais wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi aliruhusu wanamageuzi kukutana alipokuwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akienda ulaya kuomba misaaada baada ya kubanwa na wafadhiri. Sasa huyu Ulimwengu analipi la kujivunia.

Pili, Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa kampuni kubwa - Habari Copr - ikamshinda na badala yake akaiuza kwa fisadi Rostam. Sasa mtu aliyeshimdwa kuongoza watu 200 atawezaje kumshauri rais ajaye?

Anachotaka kukionyesha Ulimwengu hapa ni kwamba Slaa hajakomaa kwa urais hivyo ajifunze. Hili si kweli. CV ya Slaa ni kubwa kuliko yeye na kimsingi Slaa amekuwa kiongozi mkubwa wa madhehebu ya dini, mbumge na katbu mkuu.

Ulimwengu aondoke na pumba zake arudishe jibu kwa Kikkwete - Hatudanganyiki. Angekuwa mrtu wa maana Mkapa asingemvua uraia.

JF is for Great thinkers!! Unaweza kututhibitishia kuwa "Ulimwengu katumwa na Kikwete". Kama Mkuu wa Wilaya wa wakati huo kuzuia mikutano ni moja ya majukumu yao.

Kwa kauli zako zinaoonyesha na kudhiirisha dhahiri kuwa level yako ni ya Ulimwengu nisawa na kulingnisha kichuguu na mlima Kilimanjaro. Kwa nini asiweze kumsahuri Rais ajaye. Si humu JF tunomshauri na kumkosoa JK wa sasa acha ajaye tuna nini cha zaidi? Ni aina ya watu kama ninyi ndio mnafanya watanzani wengine waigooe hata hiyo CDM, hivi hamjaingia Ikulu hamataki kukosolewa mkiishaingia itakuwaje?

Kwa kweli DR Slaa alituahidi na anatakiwa kufanya kazi ya kujenga chama. Hivi sasa hata mtu akitaka kadi ya CDM hajui ipate wapi. Nani wa kufanya ypte hayo? Ni Katibu Mkuu. tunahitaji tuwe na vyombo vyetu vya habari TV, Redio na Magazeti, nani wa kufanya yote hayo? Ni Katibu Mkuu.

CDM inatakiwa kuwa na ofisi zenye hadhi, nani wa kupanga na kutekeleza yote hayo? Ni Katibu Mkuu.

Siasa sio chuki wala ugomvi, Jifunze lugha ya kutumia, unaishishia CDM hadhi kwa kauli zako chafu.
 
Jibuni hoja, badala ya kunishambulia. Nimesema Ulimwengu ameshindwa kuendesha kampuni yake ya watu 200 atawezaje kumshauri rais mtarajiwa? Tatizo lenu mnashabikia watu msiowajua. Mtu mwenye uraia wa kuandikishwa atakuwaje mzalendo? Huyu jamaa namfahamu ni mbinafsi kupindukia.

Alipokuwa habari alishindwa hata kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Baadaye kampuni ikazidiwa na mzigo wa madeni. Ikafilisika.

Pamoja na kupewa mtaji na Mkapa na marafiki zake - kabla ya Mkapa hajaamua kumuanika kwa kumtangaza kuwa si raia - tayari Jenerali na wenzake - Salva na Mwambo walishashindwa kuendesha kampuni.

Wafanyakazi wakawa hawalipwi kwa wakati, huku yeye akisafiri kila mwezi kwenda kwa mkewe Afrika Kusini. Naye Salva akawa anaenda Uingereza kwa mkewe. Haikuchukua muda mambo yakaenda kombo.

Alipoingia Kikwete madarakani akaanza kujipendekeza kwa kuandika maka ndefu alizozipa kichwa cha maneno, "Barua ndefu kwa Rais KIkwete." Leo eti anakuja kutaka kumshauri Slaa na kujita mwanademokrasia. Mwanadipromasia gani anayezuia mageuzi? Aaache kujipa sifa asizokuwa nazo.

, kampuni taya

Ni aibu kwa CDM na Dr Slaa kuwa na mshabiki kama wewe!!!!
 
Ulimwengu katumwa na Kikwete. DK. Slaa alishajifunza sana miaka kingi iliyopita. Kwanza, ninyi mnaotaka kumpa heshima huyu kibaka mnaitoa wapi? Unajua huyu akiwa mkuu wa wilaya ndiye aliyezuia mkutano wa kwanza wa mageuzi, hadi pale wanaharakati kama Mabere Marando, Ndimara Tegambage, Anthony Komu walipojitokeza na kupinmga udhalimu wake?

Wanaharakati hao waliandika waraka kwenda nchi za Magharibu na nakumbuka rais wa wakati huo, Ali Hassani Mwinyi aliruhusu wanamageuzi kukutana alipokuwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akienda ulaya kuomba misaaada baada ya kubanwa na wafadhiri. Sasa huyu Ulimwengu analipi la kujivunia.

Pili, Ulimwengu alikuwa mwenyekiti wa kampuni kubwa - Habari Copr - ikamshinda na badala yake akaiuza kwa fisadi Rostam. Sasa mtu aliyeshimdwa kuongoza watu 200 atawezaje kumshauri rais ajaye?

Anachotaka kukionyesha Ulimwengu hapa ni kwamba Slaa hajakomaa kwa urais hivyo ajifunze. Hili si kweli. CV ya Slaa ni kubwa kuliko yeye na kimsingi Slaa amekuwa kiongozi mkubwa wa madhehebu ya dini, mbumge na katbu mkuu.

Ulimwengu aondoke na pumba zake arudishe jibu kwa Kikkwete - Hatudanganyiki. Angekuwa mrtu wa maana Mkapa asingemvua uraia.

Ninawasiwasi na uwezo wako wa kufikiri kwako any way u can refer my signature!!!!!
 
Wewe dogo acha usengele nyuma wakati watu wanajadili mambo ya msingi na yanayotoa mustakabali wa Taifa letu, hakutazwi kupinga na wala sisemi uunge mkono, hayo mashiko unayoyapachika katika hoja zako si mashiko bali ni makalio.

jibu hoja,siyo kuandika matusi.mkiambiwa ukweli mnakimbilia matusi..
 
JF is for Great thinkers!! Unaweza kututhibitishia kuwa "Ulimwengu katumwa na Kikwete". Kama Mkuu wa Wilaya wa wakati huo kuzuia mikutano ni moja ya majukumu yao.

Kwa kauli zako zinaoonyesha na kudhiirisha dhahiri kuwa level yako ni ya Ulimwengu nisawa na kulingnisha kichuguu na mlima Kilimanjaro. Kwa nini asiweze kumsahuri Rais ajaye. Si humu JF tunomshauri na kumkosoa JK wa sasa acha ajaye tuna nini cha zaidi? Ni aina ya watu kama ninyi ndio mnafanya watanzani wengine waigooe hata hiyo CDM, hivi hamjaingia Ikulu hamataki kukosolewa mkiishaingia itakuwaje?

Kwa kweli DR Slaa alituahidi na anatakiwa kufanya kazi ya kujenga chama. Hivi sasa hata mtu akitaka kadi ya CDM hajui ipate wapi. Nani wa kufanya ypte hayo? Ni Katibu Mkuu. tunahitaji tuwe na vyombo vyetu vya habari TV, Redio na Magazeti, nani wa kufanya yote hayo? Ni Katibu Mkuu.

CDM inatakiwa kuwa na ofisi zenye hadhi, nani wa kupanga na kutekeleza yote hayo? Ni Katibu Mkuu.

Siasa sio chuki wala ugomvi, Jifunze lugha ya kutumia, unaishishia CDM hadhi kwa kauli zako chafu.

Ndugu yangu umeongea sawa kabisa, kazi kubwa ya Katibu mkuu Dr Slaa kwa sasa ni kujenga Chama, tumpe muda ana kazi ya miaka mitatu kuhakikisha chama kimejitangaza nchi nzima, kuhusu kadi za Chadema ni kweli kabisa watu wengi wanazihitaji hata wenyeviti wa wilaya na mikoa wengine hawana, hiyo ni kazi ya katibu mkuu.

Tunamwamini Dr Slaa na ndio maana tutayapenda mawazo kama haya ya Ulimwengu amabyo yana nia njema ya kumshauri, ila kwa uelewa na uzoefu ukichangaya na elimu alivyonavyo Dr Slaa anajua nini cha kuchukua kama usahuri na kipi cha kukiacha, Pia sio kila alichoshauri Ulimwengu ni kweli.
 
Ni kweli kwamba kila mmoja ana uwezo wa kumshauri Rais, lakini si kila anayemshauri rais anaweza kuwa mtu wa maana. Ninachopinga hapa mimi ni sifa ambazo mnamshushia Ulimwengu. Huyu jamaa hastahili sifa yoyote katika ukombozi wa taifa hili.

Hii ni kwa sababu alipokuwa mkuu wa wilaya alizuia ujio wa vyama vingi kwa kukataa kutoa kibali kwa wanamageuzi kukutana. Haya ni ninaushahidi nayo. Pili, hata alipiokuwa mkuu wa habari corp mbali na kushindwa kuongoza kampuni alikuwa anapingana na wanaomkosoa. Nakumbuka mwandishihi mmoja wa magazeti yake alifukuzwa kazi baada ya kuomba kwenda kusoma, tena akiwa anajilipia mwenyewe. Sasa huyu ambaye amekandamiza wenzake kwa miaka karibu 15 atawezaje kuwa mshauri wa kiongozi mkuu wa nchi?

Napinga tena napinga, kwamba Jenerali hana jipya kwa taifa hili. Alijikomba kwa Mkapa na kujifanya kuwa yeye ndiyo mshauri mkuu wa serikali. Mkapa alipoanza kukataa ushauri wake akaanza kumshambulia kuwa serikali yake imekithiri kwa rushwa. Kabla hajafukuzwa ikulu ambako alikuwa anakwenda kunywa mvinyo na Mkapa na Balozi Ruhinda, Jenerali hakuwahi kumsema Mkapa.

Lakini Mkapa alipoona mashambulizi yanazidi. akaamua kumvua nguo Jenerali kwa kuumpa changamoto kuwa kama yeye serikali yake imejaa rushwa, naye aseme wapi alikopata fedha za kuanzisha magazeti yake. Nakumbuka Mkapa alitoa kauli hii wakati akizindua ujenzi wa barabara ya Dodoma -Singida.

Na kwa kuwa feedha za kuanzisha gazeti la Mtanzania lililoanza katika kipindio cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 zilitoka kwa Rostam na marafiki wengine wa Mkapa, Jenerali akaishia kuufyta. Hata zile fedha za kununulia mtambo wa kwanza wa kuchapisha magazeti yake - Printech Company Limited ambao ulifungwa pale banda la ngozi barabara ya Pugu Road zilitolewa na Rostam.

Katika mazingira hayo, uko wapi usafi wa Ulimwengu hadi akawa na ubavu wa kumshauri rais mtarajiwa au hata rais wa sasa jinsi ya kuendesha serikali?

Nawasilisha.
 
Someni hili, halafu mtafakari badala ya kunishushia matusi.
 
bua ha ha ha haaa
 
Spanner nimekukubali, nami nakubaliana kabisa na hoja zako na kuponda usharobaro wetu humu ndani, watu wako very empty, hawana hoja ndio maana leo hii wanadiriki kusema budget hii ni nzuri, wavivu kusoma chochote wanachoambiwa ni ndio mzee, wajibu hoja zako, je wamesahau mwanzo tu jenerali bila haya alidiriki ku run article zake mbili mfululizo alizowahi kuziandika 2005 kujikomba komba akijua wazi kwamba umma wa watanzania hawakumchagua kikwete this time kama hapo 2005 lakini asithubutu hata ku replace sentesi kama raisi kikwete watanzania wamekuchagua kwa nguvu, crap. Huyu nae kachoka anatafuta pa kutokea, ni kweli makala yake imedhamiria kuonyesha kwamba slaa bado, kama vile yeye anajua, anyamaze alishakua huko akakimbia sio zamu yake sasa. Hata michango yake kwenye katika inaonekana wazi ni mahoka, akidai kwamba katiba hii kuibadili inataka muda, aende kwao Rwanda huko ndio akapeleke huu upuuzi wake kama anatafuta kuitiwa kazi na kikwete atumie mgongo mwingine sio wa kiharakati. again, spanner, nakukubali sanaaaaaaaaaa
 
Kikubwa zaidi katika hili wakubwa, ni pale kuwa mkubwa wa nchi hajajifunza mambo mengi ya msingi kabisa yanayohusu uongozi na utawala.
Kama hakujielimisha masuala ya msingi kama hayo ni hatari sana kuliko matamshi yoyote ya slaa.
NNadhani ndio sababu amekuwa na maamuzi ya kimgongano, kuingilia hata majukumu yaliyokabidhiwa idara zinazojitegemea. Just imagine, ahadi ailizotoa kama mamilioni ya Kikwete yaliyogawiwa kwa watu ovyo ovyo, uamuzi wa kupitisha barabara Serengeti duukinzana na utawala bora, uondoaji wa kabrasha la kuingiza maeneo ambayo tayari ni urithi wa taifa kuwa urithi dunia ambao kama kuingiza timu world cup, kilimo bora bila kuzingatia uhifadhi wa mazingira ni hatari kwa taifa leo, na ndio maana anaweweseka sana kwa hoja anazoanzisha mwenyewe.
 
Slaa akae chonjo, apunguze hisia, awe m-rais (presidential). Ajifunze zaidi, kwani kama bado ana nia ya kuwania urais mwaka 2015, kazi iliyo mbele yake ni kubwa. Akumbuke tu kwamba, Rais Jakaya Kikwete alikuwa na (angalau) miaka kumi ya kujiandaa kuwa rais, na hii kumi ni ile tunayoijua sisi.

Mkuu asante kwa kuleta hii makala humu jamvini.Mimi ni msomaji mzuri wa Raia mwema toka enzi hizo za Rai.
Ila kwenye makala hii na nimeisoma na kuirudia mara nyingi. Nimeshawishika kuwa Jenerali hajaeleza hasa alichotaka kueleza na kama mwandishi anayeheshimika angeweka wazi mawazo yake.

Kiufupi amejaribu kufunikafunika lakini kiuhalisia anataka au kwa kiasi fulani amemfananisha Dr Slaa na Kikwete,jambo ambalo mimi kwa mtazamo wangu si sahihi.Ameeleza kuwa Kikwete alikuwa na amechukua muda mrefu kuelewa matatizo ya Nchi yetu(Tanzania-Kijamii,Kisiasa na Kiuchumi) na kwamba Dr Slaa anasukumwa au asisukumwe na hisia huu ni upotoshaji na unafiki.

Huwezi kufika mahali ukamfananisha Dr Slaa na Kikwete (Raisi asiyejua umaskini wetu unatokana na NINi).
Pamoja na Elimu zetu za Kata huwezi pia fika mahali ukaondoa mahusiano yaliyopo kati ya HISIA na uhalisia na kwamba sasa anayetaka kuingia Ikulu akawatafute ma Dr na maprofesa au taasisi fulani imfanyie utafiti kuelewa nini matatizo yetu kimaadili(jamii),kiuchumi na Kisiasa. Basi tufike mahali sasa kuwa Raisi wa Tanzania lazima uwe Profesa au angalau Dr!

Mkuu Zak Malang;
Jenerali hapo hajatoa ushauri zaidi ya kuponda.

Hata baada ya muda huo wa miaka kumi kupita, na hata baada ya miaka mitano ya kuendesha Serikali, inaelekea bado hajajifunza mambo mengi ya msingi kabisa yanayohusu uongozi na utawala. Slaa afanye hadhari, asije akawa vivyo hivyo.
 
Ulimwengu ninayemfahamu ni yuleyule hajabadilika. Ni mtu wa kujikomba na majigambo hata pale ambapo hapastahili. Nakumbuka mwaka 1994 gazeti lake la Rai liliandika stori kubwa iliyibeba kichwa cha habari, "CCM yapitisha ponjoro Igunga." Hii ilikuwa baada ya CCM kumpitisha Rostam Aziz kugombea ubunge wa Igunga kutokana na kifo cha Chales Kabeho ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo.

Lakini gafla Rostam akawa anakwenda Mkwepu na haraka akawa anaingia katika vikao vya kuendesha gazeti la Rai na Dimba. Wakati huo yalikuwa ni magazeti hayo mawili. Baadaye wakati huo Jenerali alikuwa mbunge, ponjoro akageuka rafiki mkubwa wa Jenerali na wenzake hadi kuwapa Sh. 60 milioni kununua mtambo wa kuchapishia magazeti. Hadi hapo Jenerali hawezi kupata tena urua wa kumshauri rais mtarajiwa au hata huyu wa sasa.

Kama haya ninayayoyaeleza huyu bwana anabisha, aingie humu kwa jina lake, nami nitajitambulisha.
 
Chadema inatakiwa kuendelea kuhamasisha umma kuhusu haki zao za kiraia
Inahitaji kufungua matawi
Inahitaji kudemonstarte people power
Inahitaji kujipima kujua suport yake
Ikakamilisha miudombinu na elimu ya uraia wananchi watajua nini cha kujadili. Si watanzania wote wana elimu ya kutosha ya uraia, wala forum za majadiliano
Chadema hawana redio wala TV, hivyo maandamano yakiambatana na mikutano ya kuelimisha wananchi wanavyohujumiwa, ndio njia pekee

Maandamano mbele kwa mbele, bila kukoma mpaka 2015. hadanganyiki mtu hapa.:hatari:
 
NIMEFURAHISHWA sana na makala ya generali ulimwengu ktk gazeti la raia tar 9-14 juni.paragraph ya pili toka mwisho.

" SLAA AKAE CHONJO,APUNGUZE HISIA ,AWE M-RAIS[ANEUOTA URAIS]. AJIFUNZE ZAIDI,KAMA BADO ANANIA YA KUWANIA URAIS MWAKA 2015,KAZI ILIYOMBELE YAKE NI KUBWA.AKUMBUKE TU KWAMBA ,RAIS ANAEAMINI KATIKA KUKOSOLEWA NA UHURU WA MAONI JAKAYA KIKWETE,ALIKUWA NA ANGALAU MIAKA 10 YA KUJIANDAA KUWA RAIS, NABADO JK HAJAJIFUNZA MENGI YANAYOHUSU UONGOZI NA UTAWALA.SLAA AFANYE HADHARI[ASIDHARAU],ASIJE AKAWA VIVYO HIVYO.swali langu je wilbrod pita atakubali ushauri wa ulimwengu nakutulia kujifunza njia zakuyaondoa matatizo ya tz? pasi na jazba aliyonayo katika maandamano na kuzungumza?????????
 
Ndiyo maana huwa mnatakiwa kufikiria na sio kufuata mkumbo wa mtoa hoja

Hii nakala ililenga KUMTUKANA SLAA NA NYOTE MMEFANYA HIVYO!!!

Rudia tena kusoma tena na tena, angalia mantiki ya na nia ya Ulimwengu!

Mtu aliyetakiwa kuwa rais mwaka jana anapewa ushauri leo, amefanya nini??

Na ni kweli CDM watamsimamisha Slaa kwa 2015!!!

acheni fuata mkumbo ..HILI NI TUSI LA MWAKA NA
 
Back
Top Bottom