Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 557
- 1,544
Kwa mfano imetokea wewe kijana umefungwa kwa kumtia mimba mwanafunzi. Miaka 30 baadaye, ukarejea na kukutana na ukweli mchungu ambao hukutarajia.
📜
Kwa mfano, wewe ni kijana wa kiume na katika harakati za hapa na pale katika ujana wako, ukajikuta unamtia mimba mwanafunzi wa shule. Kwa kosa hilo la kisheria, ukahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Miaka imepita, maisha yakabadilika. Baada ya kutumikia kifungo chako, unarudi uraiani ni mtu mzima sasa hapo unasogelea miaka 49 ila unajipa matumaini kwamba yule mtoto sasa ni mkubwa umejipa matumaini hayo na ukapiga moyo konde na kuanza upya. Katika kumbukumbu zako, bado unamkumbuka yule msichana uliyetia mimba. Moyo wako unakuambia kuna mtu wako duniani—labda mtoto wako.
Unachukua hatua ya kumtafuta. Yule mwanafunzi aliyesababisha uende jela miaka, bahati nzuri mnaona sasa ni mwanamke mzima, ana watoto watano, maisha yanaonekana kuendelea vizuri kwake.
Kwa hisia mchanganyiko, unaamua kumuuliza:
"Katika hawa watoto watano, ni yupi ni mwanangu ambae nilifanya makosa nikaenda kuoga miaka 30 gerezani?"
Anakutazama kwa huzuni huku akitazama chini kwa huzuni, anakujibu:
“Mimba ile iliharibika akiwa na miezi miwili tu.”
Ghafla, unapata mshtuko kwa huzuni unasimama. Miaka yote 30 ya mateso, unyanyapaa, kupoteza ujana wako… kwa maisha ambayo hayakuendelea kuwepo. Hakuna mtoto. Huna chakurithi damu yako huna. Na yule uliyemtegemea kuwa mwanaye, hakuishi hata kuona mwanga wa dunia.
Sasa nakuacha na maswali ya kujiuliza:
Je, kama wewe ndiye mwanaume huyo, utachukua uamuzi gani?