Ulikuwa Unashika Nafasi ya ngapi darasani

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
Ulikuwa unashika nafasi ya ngapi ulipokuwa unasoma shule?



Kwanza nianze binafsi nimesoma shule ya kata toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne , licha ya uzero IQ wangu ile naanza skuli darasa la kwanza na la pili nilikuwa wa ishirini plus huko, ila kuanzia darasa la tatu mpaka saba nilianza kuwa top 3,

Nilivyofika seco ile form one nilikuwa fresh top 3,form two mtihani wa taifa kishule nilikuwa wa 3,ilivyofika form 3 sasa mbunye zikaanza kunichanganya aseee form 4 nikawa wa 8 kishule ule mtihani wa nekta nikapata three yangu nikalala mbele,

Kwenda six nikaona mzozo nikapita short cut college miaka yangu 2 tu pale ya course ya pharmacy basi maisha yenyewe namna gani vipi nikaona nisisumbue wazee kwa usawa huu ada yenyewe tu milioni 2 plus nisije kuwafanya wazee wauze nyumba bure nikaingia zangu kitaa,


ile top 3 yangu japo ya shule za kata now napikia kiepe tu hapa na certificate yangu nimeiweka kwenye begi maisha yanasonga kiubishi .


Nb;
Mwanzo nilijua Elimu ndio kila kitu na sometime nililaumu sana kuzaliwa kwenye familia ambayo haikuwa na uwezo wa kunisomesha mpaka kufikia malengo yangu ila tangu niingie kitaa naona mwake Nainjoi maisha kuliko ata yule mwenye kazi ya kuajiliwa Am free na kitu ninachoinjoi ni kuona ata mimi leo natoa msaada kwa wazee wangu kitu ambacho sikujua kwamba nitaweza bila kuajiriwa.


Cc Zero IQ.
 
Ubora wa shule ndiyo kila kitu. Mtoto wa kumi shule A anaweza kuwa wa kwanza shule B. Au wa mwisho shule C anaweza kuwa wa tatu shule D.
Na ubora wa shule ni walimu, miundombinu, vitabu nk.
Kuna shule za private wajanja sana. Watoto wote ni number za juu ili waendelee kuwakamua wazazi.
 
Ubora wa shule ndiyo kila kitu. Mtoto wa kumi shule A anaweza kuwa wa kwanza shule B.
Na ubora qa shule ni walimu, miundombinu, vitabu nk.
Kuna shule za private wajanja sana. Watoto wote ni number za juu ili waendelee kuwakamua wazazi.
Mkuu mi nimesoma shule ya kata nafikiri unazijua vyema maticha ni changamoto huwezi amini kuna baadhi ya masomo tulianza kufundishwa kidato cha tatu hapo ni wewe unakomaa kivyako tu
 
Vipi hiyo nafas uliokuwa shule 1,2,3,4,5,6,7,8,9,10 zimekusaidiaje kwenye huu uchumi wa VIWANDA?
Haujasoma Andiko mbona limeelezea kila kitu au wewe ni wale wazee wa kusoma heading na kukomenti?
 
Nilikuwa nachezeaga kwenye 40 daily....
Bahati nzuri nikaenda sekondari ya kata, nikalamba 3 yangu ya 23, maisha yanasonga.

Mambo ya vyuo nayasikiaga tu humu JF.

Baada ya kumaliza form 4 yangu nikadunduliza kamtaji kwa kuuza vimbuzi vyangu kule kijijini nikapata mtaji wa duka la vyombo.
Mambo si mabaya sana maana kwa kupitia kaduka kangu ka vyombo ninapata hela ya kuunga bando la internet, hela ya kuhonga na jioni pesa ya bia mbili sikosi daily.
 
Kipindi nipo Shule ya msingi nilikuwa na uwezo mzuri sana 1,2,3,4,5,-11 hizo zilikuwa zangu ila sekondari familia ikaleta mambo ya kalimakenge kakataa kwenda shule nikashuka sana kitaalamu.

Mtihani wangu wa kwanza nafanya nikiwa Form one nilikuwa wa 99.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] wazee walizingua nini mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…