Ulikuwa na sifa gani chuoni/shuleni?

Ulikuwa na sifa gani chuoni/shuleni?

Namba 20 inanihusu kwa chuoni kwa kweli. Mnakuwa mmechagua jembe lenu la kupresent. Halafu kuna walimu sijui walistukia kuwa kuna watu wa sampuli yetu, basi ile mnampa tu mwalimu copy yake anaanza kutaja majina. Utasikia fulani anza kupresent. Baada ya muda, fulani, endelea Arrrrrrgh!
 
Darasa lolote lile (hasa vyuoni) lazima liwe na wanafunzi wafuatao:

1. Mwizi/ mdokozi.

2. Playboy/playgirl. Hawezi kutembea na msichana/mvulana mmoja mara mbili.

3. Group ya marafiki watatu. Kila mara wako pamoja.

4. Mtu mwenye maswali ya kuudhi/kukera.

5. Msongolist kimeo. Huyu huwa anasoma sana bt hana bahati ya kufanya vizuri. Yani msuli tembo, bt matokeo sisimizi.

6. Mlafi. Huyu huwa hakatai offer.

7. Mtoro wa kudumu. Haji darasani hata km hana sababu.

8. Mchelewaji wa kudumu. Anakuja kipindi kiko katikati au kinakaribia kuisha.

9. Miss/Mr.Misifa. kila mara ataeleza the way nyumbani kwao walivyo matajiri.

10. Less talkative bt kiwembe. Jamaa mkimya bt unakuta ametembea na karibu wasichana 15 hapo class.

11. Handsome boy ambaye hana mpango na wanawake.

12.Chips addicted. Hawa wanaweza kula chips asubuhi mchana na jioni. Jumatatu hadi jumatatu.

13. Back benchers. Hawa huwa watundu sana na ni watu wa jokes. Huwa hawajibu swali, but wanasubiri wakati wa kushangilia waongeze bezi.

14. Wambea. Hawapitwi na kitu darasani na washazoea kufeli.

15. Mchungaji/Mtumishi wa Mungu,

16. Waimbaji/Wasanii,

17.Walevi

18.Mabishoo.

19. Team popo. Hawa wewe na hela wasiwe na hela wanakesha club,

20.Mwenye aibu kusimama mbele za watu. Wakati wa Presentation anakimbilia kusimama nyuma ya wenzie,

21. Viherehere. Hawa mara nyingi hutokea kupendwa sana na waalimu.

22. Wanaosoma ili kushindana kwny GPA.

23. Kupe. Huyu boom likitoka atawaganda wenzie hadi ziishe, halafu yeye anaanza kula zake alone.

24. Wise man/woman. Huyu huwa ni mtu anayeaminika na kila mtu darasani. Hutumika sn kushauri pale mambo yanapoenda mrama. Mara nyingi huwa ni mtu mzima.

25.Fix man. Huyu atakuomba jero, akafuatilie dili la milioni kumi town, kumbe hana hela ya chai.

26. Photocopy machine. Huyu ukimuonesha majibu kwny mtihani anaweza kucopy hadi jina lako.

Je wewe ulikua namba ngapi??

Kumbe na huku upo? Wewe ni noma.
 
namba 4! mara nyingi huwa naitumia tu kama sehemu ya utani! huhuhuuu!

Nilishawahi kumuuliza swali mgombea urais hapa chuoni, jamaa akaondoka kwa hasira sana na urais hakushinda!

Tabia za uhaya haya hizi mbaya sana!
 
Back
Top Bottom