youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,879
- 4,035
THE DANGER OF BEING ACADEMICALLY SMART: KUAMINI KWAMBA DUNIA INAKUDAI MAISHA MAZURI KWA SABABU ULIKUWA MZURI DARASANI.
Kuna tatizo ambalo watu wengi waliokuwa academically smart wanakutana nalo wanapoingia kwenye maisha halisi.
Kwa sababu walikuwa wanafanya vizuri shuleni, wanapata alama nzuri na walikuwa miongoni mwa wanafunzi bora, wanaanza kuamini kwamba dunia inawadai excellence, kazi nzuri, kipato kikubwa na maisha mazuri kwa sababu tu walikuwa better than others academically.
Lakini maisha yana mfumo tofauti na shule.
Ukweli ni kwamba, dunia haikulazimiki kukupa maisha mazuri kwa sababu ulikuwa mwanafunzi bora.
Huwezi kutegemea kupata kazi nzuri kwa sababu tu ulikuwa unapata A darasani. Huwezi kutegemea kupata pesa nyingi kwa sababu tu ulikuwa na akili kuliko wenzako. Huwezi kutegemea watu wakuheshimu kwa sababu tu una vyeti vingi.
Katika maisha halisi, kuna watu ambao hawakuwa wanafunzi bora lakini wamejenga biashara kubwa, wamefanikiwa kwenye uwekezaji na wanaishi maisha ambayo watu wengi waliokuwa academically smart wanayatamani.
Kwa nini?
Kwa sababu maisha yanahitaji zaidi ya akili za darasani.
Yanahitaji:
* Uwezo wa kutatua matatizo.
* Uwezo wa kuuza na kujadiliana.
* Emotional intelligence.
* Uwezo wa kujenga mahusiano na connections.
* Nidhamu ya kifedha.
* Uwezo wa kuchukua hatua na kuvumilia changamoto.
* Uwezo wa kujifunza na kubadilika.
Jambo muhimu nililopaswa kujifunza ni kwamba, kuwa smart hakumaanishi kwamba unastahili kupata kila kitu bila kupambana.
Ulikuwa bora darasani? Hongera. Lakini sasa unahitaji kujithibitisha kwenye maisha halisi.
Acha kutegemea dunia ikutambue kwa sababu ya uwezo wako wa zamani. Jenga uwezo mpya, jifunze skills zinazoweza kukuletea kipato, tafuta fursa na uwe tayari kuanza chini.
Your academic intelligence may open the door, but your ability to adapt, create value and execute will determine how far you go.
Usitumie maisha yako kujaribu kuthibitisha kwamba wewe ni bora kuliko wengine. Tumia muda wako kujenga maisha unayoyataka.
Dunia haikulazimiki kukulipa kwa kuwa smart. Inakulipa pale unapoweza kutengeneza thamani ambayo watu wanahitaji.