Ulikutana na Changamoto gani wakati wa Uchumba (kabla ya Ndoa)?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,464
Nyie wa dada wa mie
Mnasikia.. 👌

Kuna kitu wanawake wanaita kujishusha, wanasema usipojishusha basi utamkosa mwanaume. Nikweli mara nyingi mwanamke unatakiwa kujishusha lakini wanawake wengi hawajui kujishusha ni nini?

Kujishusha ni ile hali ya kua mpole, kumheshimu mwanaume, kupunguza malumbano na hata kama una hela kuongea naye kistaarabu na kumsikiliza. Lakini kumuomba mwanaume msamaha wakati kosa ni lake huko si kujishusha ni kule upumbavu na mateso.

Kwamba umemfumania, akakupiga halafu unaomba msamaha wewe, huo ni ujinga na kama unafanya hivyo basi jua unamtengenezea kiburi na mbaya zaidi unamuambia unaweza kufanya kosa lolote nitakusmaehe na pia nitakunyenyekea, unamuambia mimi si binadamu ni kama jalala lako.

Kuna makosa ambayo utayaacha yapite kwakua ni ya kawaida lakini maosa kama usaliti, kupigwa, kutukanwa, kunyanyaswa usiruhusu ayafanye na kuacha yakapita bila yeye kujutia. Wakati wa uchumba ndiyo wakati wakumua kuwa wewe hutaki kitu gani na kitu gani, ukivumilia wakati wa uchumba jua baada ya ndoa atazidisha.

Hivyo kabla hujaomba msamaha jiulize je unataka maisha yako yote yawe hivyo, kupigwa na kuomba msamaha kama hutaki basi muambie aombe msamaha yeye na kama hatataka basi ondoka na tafuta ustaraabu mwingine kwani hata akikuoa unaenda kwenye mateso tu.
 
Ya nini kujishusha kwenye uchumba halafu baada ya ndoa aoneshe makucha!!?
 
Kweli shetani hapendi taasisi ya ndoa.yaani katika kipindi cha kuelekea ndoa.michepuko yote inafufuka na maoffer na mabundle ya kufa mtu.
Bundle la gari,bundle la mtaji.,bundle la kwenda ulaya etc.ukiangalia unakoenda hata choo hakuna
hapo ndo utajua kwanini shetani alifukuzwa mbinguni
Tuombeane jamani maana wengine gunia mbili za mkaa hazitatosha wala meno hayatabaki kwa ajili ya dna
 
Back
Top Bottom