Weltmeisterschaftung
JF-Expert Member
- Aug 27, 2014
- 364
- 247
Mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma.
Siku ya kwanza nilipokwenda kwenda ku-report kazini mwaka 2011 kampuni moja ya Dar kabla ya kuletwa huku Tanga,nilichomekea suruali yangu nzuri tu nimeipiga pasi upanga unangaa mtoto wa kiume na shati safi pamoja na tai moja matata sana kama nilivyozoeshwa taratibu za uvaaji nikiwa primary, o level na hata high school.
Nilipofika kwenye ofisi na meneja rasilimali watu alinipokea vizuri sana na kuanza kunipitisha kwenye partition ya kila department nikitambulishwa kuwa mimi ni mfanyakazi wao mpya hivyo wanipe ushirikiano wa kutosha katika shughuli zangu.
Kilichonishangaza ni kwamba watu walikuwa wakinong'ona chini kwa chini kwa kila idara niliyokuwa nikitambulishwa na nilipokuja kuuliza baadaye baada ya kuzoeana nao nikaambiwa kuwa nilikuja ofisini nimevaa kama babu mzee wakati wao wanatupia vimodo vya kijanja. Kuna wakati watu wanatupia mpaka vimodo vinaishia chini ya magoti utafikiri anaenda disko kusakata rumba.
Nilishangaa sana na kujiuliza zile tabia njema za uvaaji tunazofundishwa mashuleni huwa zinapoteleaga wapi? Lakini kwa kuwa nilijua kwa maisha ya mjini kila mtu huwa ana ustaarabu wake nilipotezea.
Sasa unajua ni nini kilitokea,baada kupiga mzigo wa kufa mtu kama miezi sita nikapewa transfer kuletwa Tanga kuwa assistant branch manager na kuwaacha "wajanja wa mjini" wakiwa mdomo wazi hawana la kusema. Nilichojifunza tangu siku hiyo ni kuwa usafi unalipa sana pahala pa kazi na utaonekana ni mtu tofauti sana kama utajipenda na kujijali.