Ulijuaje unadate na wakishua

Ulijuaje unadate na wakishua

Mwanangu nshawi kukutana na pisi miaka flani ya 2015 au16 hv, niliazma gari kwa bro appointment ikawa mlimani city, pisi ikataka ice cream nikanunu, ikataka na viujinga ujinga snacks za hapa na pale nikanunua, dakika za majerui nikawa napiga hesabu naona hela nlobaki nayo haitoshi hata kurudishia mafuta ya watu, ile frustration usoni kwangu haikufichika. Demu alijiongeza akanipa kadi yake ya bank akanambia katoe hela chap.
Atasaaa atasaaa atasaa!....
 
Kuna mtu alishangaa kuona nimekula slice mbili za mkate na kipande cha yai halafu nikamwambia nimeshiba sana, hadi leo ananiita wa wakishua, ananikeraaaa
 
Duh sijakuelewa
2026_03_11_17.15.26.jpg
 

Hii inekaa kiutani lakini kuna mengine yametokea kweli.

Hii ya "Alisema anatoka mara moja kumbe anaenda Japan" imenikumbusha mbali sana.

Kuna mchizi alitufanyia hiyo, katuacha nyumbani kwake tume chill na mdogo wake. Kasema anatoka mara moja.

Basi tumekaa tunaangalia ITV tukamuona kwenye taarifa ya habari anapanda ngazi za ndege. ITV wanasema "Ujumbe wa Tanzania umeondoka leo kwenda Japan..."

Tukasema yule pale si mchizi mwenyewe katuaga anatoka mara moja hapa yule?

Tena ilikuwa hivyo hivyo Japan.
 
Wale wa kishua og wakisoma hizo comment hawaelewi chochote
 
Back
Top Bottom