Uliemteua akikusifia sana gutuka

Uliemteua akikusifia sana gutuka

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,255
Reaction score
16,185
Hakuna asiyependa kusifiwa, lakini kusifia sana kitu ni sawa na kukijaladia ili rangi yake halisi isionekane na kujulikana. Sifa nyingi ni sawa na ganzi inayomfanya mtu asijisikie maumivu akikwaruzwa.

Sifa muhimu yenye maana kwa aliyekuteua ni kufanya vizuri sana kwenye kazi alizokutaka uzifanye, baaasi. Watu wezi, wavivu na wazembe wa kazi wanamziba mdomo, macho na masikio aliyewateua kwa kumpamba na sifa zilizopitiliza uhalisia.

Ukiwa kwenye mamlaka ya uteuzi penda kukutana na kazi zenye takwimu za wateuliwa sio maneno na hotuba ndefu kama za kwenye kampeni za uchaguzi majimboni.

Ukikuta mteule anakupamba sana kwenye mikutano usivimbe kichwa bali mchunguze sana na sana na sana lazima utamkuta na madudu mengi sana.

Nikupe mfano wa mteule mmoja ambae alipewa idara nyeti sana na kubwa, mteule huyu alikuwa anajua kuyapanga maneno, alikuwa kwenye hotuba zake alikuwa akilitaja jina lote la mteule wake karibu hotuba yote, na maneno ya mh. fulani oyeeee! Kila wakati na mpigieni makofi Mh. Fulani kila wakati. Lakiñi kila akikaguliwa anakutwa na ugoigoi kwenye kazi zake hadi akaambiwa na mamlaka kuwa ajirekebishe ama sivyo asaidiwe, na hatimae akasaidiwa kweli kwa kuwekwa pembeni kwenye idara hiyo.

Ukiona mteule anamsifu kupita kiasi aliyemteua tuma jopo kubwa kukagua kazi zake na mwenendo wake, lazima utamkuta na kasoro.

Viongozi msilevywe na sifa za wateule wenu.
 
Hizi ni tabia za wanaCCM na makada wengi walioramba teuzi pasipo kutegemea tumeshawazoea maana ni trending..

Awamu ya Tano ilikithiri sana, kwa mama bado wanasoma mchezo.

Siasa za kijinga sana hizi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikupe mfano wa mteule mmoja ambae alipewa idara nyeti sana na kubwa, mteule huyu alikuwa anajua kuyapanga maneno, alikuwa kwenye hotuba zake alikuwa akilitaja jina lote la mteule wake karibu hotuba yote, na maneno ya mh. fulani oyeeee! Kila wakati na mpigieni makofu Mh. Fulani kila wakati. Lakiñi kila akikaguliwa anakubwa na ugoigoi kwenye kazi zake hadi hadi akaambiwa na mamlaka kuwa ajirekebishe ama sivyo asaidiwe, na hatimae akasaidiwa kwa kuwekwa pembeni kwenye idara hiyo.

Ukiona mteule anamsifu kupita kiasi aliyemteua tuma jopo kubwa kukagua kazi zake na mwenendo wake, lazima utamkuta na kasoro.

Viongozi msilevywe na sifa za wateule wenu.
Aweso nae jana alizidisha mno
 
Hizi ni tabia za wanaCCM na makada wengi walioramba teuzi pasipo kutegemea tumeshawazoea maana ni trending..

Awamu ya Tano ilikithiri sana, kwa mama bado wanasoma mchezo.

Siasa za kijinga sana hizi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo la hao wasifiaji... upatie watakusifu... ukosee watakisifu... utengue kauli watakisifu!
Ila ukiwachukulia hatua za kinidhamu au ukistaafu watakugeuka kama si wao vile!
 
Hakuna asiyependa kusifiwa, lakini kusifia sana kitu ni sawa na kukijaladia ili rangi yake halisi isionekane na kujulikana. Sifa nyingi ni sawa na ganzi inayomfanya mtu asijisikie maumivu akikwaruzwa.

Sifa muhimu yenye maana kwa aliyekuteua ni kufanya vizuri sana kwenye kazi alizokutaka uzifanye, baaasi. Watu wezi, wavivu na wazembe wa kazi wanamziba mdomo, macho na masikio aliyewateua kwa kumpamba na sifa zilizopitiliza uhalisia.

Ukiwa kwenye mamlaka ya uteuzi penda kukutana na kazi zenye takwimu za wateuliwa sio maneno na hotuba ndefu kama za kwenye kampeni za uchaguzi majimboni.

Ukikuta mteule anakupamba sana kwenye mikutano usivimbe kichwa bali mchunguze sana na sana na sana lazima utamkuta na madudu mengi sana.

Nikupe mfano wa mteule mmoja ambae alipewa idara nyeti sana na kubwa, mteule huyu alikuwa anajua kuyapanga maneno, alikuwa kwenye hotuba zake alikuwa akilitaja jina lote la mteule wake karibu hotuba yote, na maneno ya mh. fulani oyeeee! Kila wakati na mpigieni makofi Mh. Fulani kila wakati. Lakiñi kila akikaguliwa anakutwa na ugoigoi kwenye kazi zake hadi akaambiwa na mamlaka kuwa ajirekebishe ama sivyo asaidiwe, na hatimae akasaidiwa kweli kwa kuwekwa pembeni kwenye idara hiyo.

Ukiona mteule anamsifu kupita kiasi aliyemteua tuma jopo kubwa kukagua kazi zake na mwenendo wake, lazima utamkuta na kasoro.

Viongozi msilevywe na sifa za wateule wenu.
Kweli kabisa 100% truth !!
 
Tatizo la hao wasifiaji... upatie watakusifu... ukosee watakisifu... utengue kauli watakisifu!
Ila ukiwachukulia hatua za kinidhamu au ukistaafu watakugeuka kama si wao vile!
Mara nyingi sifa hizi ni jitihada za kuziba pengo la mapungufu Yao kwenye kuleta matokeo. Na wengine ni "mtumikie kafiri upate maradi wako" vinginevyo hawana heri na wewe.
 
Ukiona mtu mzima anakusifu ujue kuna mahali kakutoboa tundu linaruhusu unamlipia bili zake za maisha.
 
Back
Top Bottom