Miaka miwili si bado tunatembeza bahasha.
Hata ukipata kazi ndani ya mwaka mmoja baada ya chuo. Miaka miwili huwezi kusema elimu yako imekutoa. Kwasababu sehemu nyingi utaajiriwa kama trainee au graduate. Mshahara laki 9, laki 8 au laki 7 unaoweza kuondoka nao kwenu. Miaka miwili hii hela hata usipokula ukaieka yote akiba bado haijafika hata milioni 30. Hapo ndio utasema umetoka? Mana hata gari ya kununua kwa pesa yako hujaweza kununua bila msaada wa mkopo. Unachoweza ni kula, kuvaa, kuchangia michango ya hapa na pale.