Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,701
- 9,779
Ndugu zanguni, mkiniona nimekuwa sugu la mapenzi kiasi hiki, jueni tu nimepitia mianzi ya kila kiwango. Nipende tu kusema haya mapenzi hayana mwenyewe. Enzi zile nilipokuwa napata taarifa ya usaliti ama kitelekezwa nililia sana, hii ni kwa kuwa nilikuwa napenda mpaka napenda tena, yaani unaingia kwenye mahusiano na mwanamke wa ndoto yako ambaye amekidhi vigezo vya kimwonekano na tabia uzitakazo, hivyo akina Aisha Kibunda unaamua kuwatupilia mbali bila kujali huenda wakawa wafariji wako kwa dunia ya kesho. Sasa hivi mi ni zaidi ya sugu
Mara ya mwisho kuachwa:
Ilikuwa ni mapema sana siku ya weekend (J2), nilikuwa hata bado sijapata kifungua kinywa, nashangaa video call inaingia kwenye simu. Ile kumpokelea tu, nashangaa yuko na bwana ake guest, wamejifunika mataulo huku wanacheka, ile niko naduwaa nashangaa bibie anasema, "cheki kisura chake kilivyomshuka, halafu amejamba, jamani! Mmh Mmmh Mmmh, baby harufu, kata simu baby haruuuuufuuu".
Kwa kuwa tayari nilikuwa nshakuwa sugu la mapenzi, nilipeleka ndoo tatu bafuni kwenda kuoga, moja nilitia sabuni ya unga na mtego, nyingine maji ya kusuuzia mwili, nyingine nilitia chumvi ya mawe kwa ajili ya kuondoa huo mkosi. Yaani tuseme tu nilijifua kama gari. Mapenzi bhana!
Kilichoniwazisha, jana yake usiku nilikuwa naye somewhere tunapanga mipango ya maisha yetu ya baadae huku tunacheka na kutabasamu, idadi ya watoto tutakaokuwa nao na majina yao, tukapanga kwenda kutambulishana ukweni n.k Kisha nikampatia 30k kwa ajili ya kusuka. Nikapata denda tukaagana, kila mmoja akamwambia mwenzie asisahau kumuota