Ule utapeli wa kijuha umeanza tena...

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Rafiki yangu aliibiwa simu akiwa anasafiri, mara nikatumiwa ujumbe kuwa simu yake imeharibika na anasafiri ila amepatwa na shida kidogo hivyo nimtumie laki moja na namba ikatumwa ya kutumia hela. Nikampigia akakata na kutuma ujumbe kuwa simu mbovu hatutoelewana.

Nikiwa njiani kuelekea kwa wakala nafsi ikasita, nikampigia mama yake bahati nzuri nae(rafiki) ndio alikuwa amefika, kumueleza akastuka kweli, ikabidi aanze mchakato wa kuwajulisha alioweza kuwa ameibiwa simu. Ila kuna mjomba wake alikwishatuma pesa.
 
Kwa staili hii hata mimi nilinusurika sana kupigwa.
 
Hahaha ilinitokea mwaka jana mwishoni mwishoni ,mbaya zaidi walitumia namba ya rafiki yangu iliyokuwa imepotea. Na me nilikuwa sifahamu kama ile namba imepotea
Kilichofanya nishtuke alipokuwa hataki nmpigie simu,then nitume 100k kwa namba nyingine waliokuwa wameitaja
 
Kuna mjinga flan kanipigia juzi eti ooh!Kuna mtu kakosea kutuma pesa kwako naomba uturudishie..nikamwambia hebu jaribu kwa mwingine utapata...baada ya hapo alivurumisha matusi vby sn
Mimi aliniambia anatoka kampuni ya voda! Kuna pesa imetumwa kimakosa hivyo niirudishe. Halafu walivyokuwa hawatumii akili, code namba zao si za huduma za wateja bali ni za wateja. Alivyoona nimemshutukia ananiambia subiri sasa tukufungie line yako halafu akakata simu.
 

Hii ya kizamani sana mkuu....hawa na wale wa madawa ni wa kale sana..
 
Nafikiri ukishatapeliwa ndio unakuwa umekabidhiwa rasmi advance diploma ya ujinga.

Na ukienda polisi kushtaki automatically unakuwa umepata degree ya ujinga. ....maana kule unakuwa kituko zaidi cha karne, ... hasa wanapoanza kuuliza km huwa unasoma meseji za polisi? .....in case umepigwa kwa style ya (TUMA HELA KWA NAMBA HII.)

Huu utapeli wa meseji km aliyoletewa Mshana, ni random search ya watu wenye tamaa za kijinga (a deal is always too good to be true.)

Huwezi kutapeliwa km wewe si mjinga , na huna tamaa.
 
Dawa ni kulala kimya
Lazima uwaoneshe kwamba nawe unajua.... Mini mmoja alinipigia akaongea pumba zake alipomaliza nikamuuliza unajua unaongea na nani? Akakaa kimya... Nikamwambia hapa ni mochwari.... Nadhani alikata simu kabla sijamalizia neno chwari.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jibu zuri sana maana nilivyokuwa naanza kusoma nilikuwa nataman nipne uliwajib vip
Kajibiwa... Sisi tulifanya utapeli kama huu way back 2000+ ni wa kizamani mno... Sema nikufundishe wa kisasa unaotuweka mjini bila bughudha
 
ile itume kwenye namba hii angekula hela yangu sema kuweka neno 'itume haraka' alikosea

kuna bwana mdg nilitakiwa mtumia hela na nilimwahidi siku iyo mara msg ya itume kwa namba hii iyo hapo ila nikashangaa bwana mdg anasema itume haraka nikakausha kumbe ni bwana tapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…