Ulaya: Watu wanakula chakula cha wanyama wafugwao na kupasha chakula kwa mshuaa kutokana na ugumu wa maisha

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,895
Baadhi ya watu wanakula chakula cha wanyama wafungwao 'Pet' wakati wengine wanajaribu kupasha chakula kwenye radiator.

Haya yamesemwa na Mark Seed, mkurugenzi wa mradi wa chakula cha jamii huko Trowbridge, mashariki mwa Cardiff, mji mkuu wa Wales.

Uchanganuzi wa BBC wa data ya sensa ya 2021 unapendekeza kuwa jamii sita kati ya watu walionyimwa zaidi huko Wales, mojawapo ya mataifa manne yanayounda Uingereza, ziko katika jiji hilo.

Hata hivyo, shirika la usaidizi linaonya kuwa kaya zinazotatizika hazionekani tu katika maeneo yanayohusiana na umaskini kwa muda mrefu na kutoa wito kwa sera kulenga watu, na si maeneo.

"Bado ninashangaa kuwa na watu kula chakula cha wanyama," anasema. "[Kuna] watu ambao hujaribu kupasha chakula chao kwenye bomba au kwa mshumaa.

Hizi ni hadithi za kweli za kushangaza," anaongeza. "Cardiff ni jiji linalostawi, lakini lina mifuko ya kunyimwa ambayo haikubaliki," anasema Seed, ambaye anasema watu hawapati mapato ya kutosha kulipia mahitaji muhimu.

Mgogoro wa mfumuko wa bei umezidisha hali hiyo. "[Watu] wanatuambia kwamba wanafanya kazi kila saa wanayoweza," aeleza. Pantry, benki ya chakula ambayo Seed inaendesha, inatoa chakula bora kwa bei ya chini sana kwa zaidi ya watu 160

w

Maelezo ya picha: Seed anasema kuwa watu wengi katika jiji la Wales la Cardiff wanatatizika kula na kupata joto wakati huu wa baridi kutokana na mfumuko wa bei.​

Kwa miongo kadhaa ya Wales Magharibi na Dales zilipokea ufadhili wa ziada kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya (EU) kwa sababu zilikuwa kati ya sehemu masikini zaidi za Uropa, lakini Cardiff haikujumuishwa kwa sababu, kwa viwango vya wastani vya maisha, haikunyimwa.

Victoria Winckler, mkurugenzi wa shirika la kutoa misaada la umaskini la Wales The Bevan Foundation, alionya juu ya hatari ya kuwa na maoni potofu kuhusu maeneo makubwa au miji kama iliyonyimwa au tajiri.

"Mtazamo yaliyopo ni kwamba Cardiff ina ustawi na mabonde ni duni na takwimu hizi zinaonyesha kuwa hii sivyo hata kidogo," alisema. "kuna maeneo ya Cardiff ambayo yamestawi, ndio, lakini pia unayo maeneo muhimu ya mji mkuu wa Wales ambapo watu hawafanyi vizuri na hali ni duni," aliongeza.

zaidi ya Wales Shuhuda za watu hawa zinaongezwa kwa wananchi wengine wengi wanaoishi sehemu mbalimbali za Uingereza.

w

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha: Mamilioni ya watu nchini Uingereza kwa sasa wako kwenye njia panda ya kuamua iwapo watakula au kulipa bili zao za umeme na kupata joto kipindi cha baridi kali.​

Takriban thuluthi moja ya wazazi wasio na wenzi wa ndoa wameamua kuruka mlo mmoja wa siku ili kujikimu, kulingana na uchunguzi wa hivi majuzi wa kundi la Watu kuhusu kaya zilizoathirika zaidi na mzozo wa mfumuko wa bei nchini humo.

Wanachama wa kaya 3 kati ya 10 za mzazi mmoja waliohojiwa walisema walikuwa wameruka mlo kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula.

Kwa jumla, hali kama hiyo hutokea katika 14% ya kaya zilizoshiriki katika utafiti.

"Utafiti wetu uligundua kuwa familia kote Uingereza zinakabiliwa na matatizo kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, huku kaya za mzazi mmoja zikiwa zimeathirika zaidi na mgogoro huo," Rocío Concha, mkurugenzi katika shirika la sera na uanaharakati, anasema ni muhimu kwamba maduka makubwa yahakikishe kuwa bei ni rahisi kulinganisha na kwamba kuna matoleo mbalimbali kwa bajeti tofauti.

"Bei zinapoendelea kupanda, ni muhimu kwamba kila mtu apate chakula cha bei nafuu ambacho ni cha afya kwao na familia zao," Concha aliongeza.

Takwimu rasmi za hivi punde zinaonyesha kuwa mfumuko wa bei wa chakula nchini Uingereza ulifikia 16.4% mnamo Oktoba, kiwango chake cha juu zaidi tangu 1977.

w

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES: Hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa nguvu kwa bidhaa za msingi za kila siku kama vile maziwa, siagi, jibini, pasta na mayai.​

Kaya za mzazi mmoja na wastaafu hutoa sehemu kubwa ya bajeti yao kwa chakula, umeme na petroli, karibu 30%.

Kwa wanandoa walio na watoto, asilimia hii huanguka hadi 25%, kulingana na mahesabu rasmi.

Hata hivyo, kaya zote zinatumia kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko mwaka jana kwa bidhaa muhimu.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 aliwaambia wachunguzi kwamba kutokana na gharama ya bili zake, wiki kadhaa hawezi kulisha watoto wake.

Mtu mwingine aliongeza: "Sili chakula cha kutosha ili niweze kuwalisha na kuwavisha watoto wangu na bado sina umeme wa kutosha."

Kulingana na data iliyofichuliwa Jumatatu hii na Shirikisho la Viwanda la Uingereza (CBI, kwa kifupi chake kwa Kiingereza), uchumi wa Uingereza uko kwenye njia ya kushuka kwa 0.4% mwaka ujao kutokana na mfumuko wa bei na mashaka ya makampuni makubwa. Hususan makampuni ya kuwekeza

Chanzo: BBC
 
Kumbe ndani ya huu ulimwengu kulikuwa na mambo mengi yaliyo jificha na mgogoro wa Ukraine umekuja kuyafichua yote.

Kwanza tuliaminishwa Urusi si chochote ndani ya dunia hii lakini kuingia kwake vitani kumesababisha dunia nzima kuyumba.

Kumbe maisha mazuri yaliyo kuwa yanaimbwa ndani ya Ulaya yalitokana na gesi ya bei rahisi kutoka Urusi.

Hebu soma hizi screenshot za habari kutoka BBC.
Screenshot_20221207-091927.jpg
Screenshot_20221207-091950.jpg
Screenshot_20221207-092008.jpg
Screenshot_20221207-092025.jpg
Screenshot_20221207-092050.jpg
Screenshot_20221207-092107.jpg
Screenshot_20221207-092121.jpg
 
Chakula cha mifugo huko ni wali, nyama, ugali, hivo msidhani wanakula takataka kama tunazolisha mifugo yetu
 
Back
Top Bottom