Ulawiti katika shule za msingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulawiti katika shule za msingi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mhache, Sep 3, 2008.

 1. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je ulawiti wanaofanyiwa watoto wa kiume ni tatizo la jamii au la kisaikologia? Nimepata taarifa nisizokuwa na ushahidi nazo wa kutosha kwamba wanafunzi wa darasa la pili na la tatu katika shule moja ya msinigi iliyopo Sinza karibu na Vatican Bar wanafanyiwa mchezo mchafu na mzee/kijana mmoja ambaye mpaka sasa hajajulikna.

  Tatizo la kulawitiwa vijana hao wa kiume lipojulikana lilipelekwa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo. Mwalimu huyo hakuonyesha jitihada zozote katika kutatua tatizo hilo ila alikaa kimya. Kwani watoto hao walikuwa hata kukaa hawawezi. Midomo ilishaanza kubadilika na kuwa kama ya mnywa gongo au kuchubuka na kupasuka. Je kitaalamu hilo ni tatizo la kuwa wamepata uambukizo au vipi.

  Baada ya tatizo hilo kuwa sugu walimu wa afya shuleni hapo waliwaita wazazi wa watoto hao na kujadili suala hilo. Wazazi wengine walikaribia kuzimia kwa mshtuko kwani hawakuwadhania watoto wao. Baada ya hapo wazazi walikubaliana kuripoti suala hilo polisi na baadaye kwenda kuwapima afya watoto wao.

  Ushauri ninaoutoa ni vizuri wazazi tuwe na utamaduni wa kufuatilia nyendo na maendeleo ya watoto wetu kila mara na kila siku. Kwani vijana hao waliolawitiwa walikiri kutishiwa maisha na mlawiti huyo kama watatoa siri. Watoto wakabaki wakiugulia moyoni.

  Baada ya kikao cha walimu wa shule hiyo na wazazi sijajua kilichoendelea.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  This is too shocking kweli!hawa wazazi they must take actions the sooner the better maana when things get out of control hawa watoto tayari watakuwa wamekubuhu kwenye hiyo sekta na idadi ya wanaume kamili nchini itakuwa imeshuka!
  Sodomy is a crime nad heavily punished by law!
   
 3. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hii ishu nadhani iende pubilc na huyo jamaa atafutwe apatikane naye apate adhabu yake kama akina babu Seya.
   
 4. m

  mgirima Member

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo hili linaelekea kuwa kubwa kuliko Serikali, wazazi na hata jamii inavyolielewa. Tatizo hili lilishawahi kutokea shule ya Mgulani. Wahusika ni watu wazima. Inadaiwa suala lenyewe lilimalizwa katika njia isiyoeleweka.

  Kuna haja ya tabia hii kupigwa vita na vita hiyo ionekane kuwa ya uwazi. Mambo haya yakiachiwa katika shule zetu za msingi, ni kizazi gani tunachotegemea huko mbele.
   
 5. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tatizo hili ni zito,na halifai kufumbiwa macho.Sina hakika kama dalili unazozizungumzia ni za ukimwi au laa.La msingi hapa ni kwamba, kama una uhakika na unalolizungumzia,tafadhali peleka taarifa hizo kwa ungozi wa juu wilayani ili uchunguzi wa kina ufanyike kuhusu suala hilo.
   
 6. Tuya

  Tuya JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2008
  Joined: Aug 30, 2008
  Messages: 313
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Masikini inasikitisha watoto wadogo wanaanza kuharibiwa bado mapema
  na hili ni tatiso sugu ingawaje wahusika nadhani wanajitahidi kulifanya liwe kama ndio utamaduni lilishawahi kutokea maeneo ya Kawe watoto wawili walifanyiwa sina hakika kama ni wa shule moja au laa ila wazazi wao baada yakutoa taarifa polisi polisi hawakuonyesha kulipa uzito wowote na mpaka leo hii wale wazazi bado wanasota Mahakamani , najaribu kusema kwamba kwa upande wa polisi sijui kuna tatizo gani kwasababu polisi huwa hawawi siria kwa hili.
   
 7. D

  Darwin JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Shule kwa upande mkubwa nawalaumu.
  Kama jambo hilo limetokea na hata watoto walitishwa vipi, mkuu wa shule angefanya afanyavyo ili kupata huyo mhalifu.

  Yaani hao watoto wangepozwa kisaiklojia nakuambiwa kwamba hakuna litakalotokea kama watamtaja huyo mtu.

  Ushahidi wange weka mtego ili huyo jamaa abambwe live.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kama habari hizi ni za kweli basi wasiliana na Kamanda Kova, nadhani cmu yake iliisha wekwa wazi hapa JF...so sad kwa sisi wazazi na watanzania wenye nia njema
   
 9. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kuna allegation kutoka kwa mwalimu wa shule ya msingi Tandika, kwamba kulingana na umaskini wa eneo hilo vijana wengi wamearibiwa baada ya kuvutishwa bangi na kupewa pesa. Jina la shule limenitoka lakini Nahisi ni Azimio. Hali ya vijana wa shule hiyo naambiwa inasikitisha. Wadau Mlioko bongo fuatilieni hili.
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hii si habari ngeni.
  MWaka 1997 pale Bunge Pr School mambo haya yalitokea. Kijana mmoja ambaye baba yake alikuwa mfanyakazi wa serikali alikuwa akilawitiwa na vijana wa shule kadhaa za sekondari pale amaeneo ya Ikulu.
  Nijuavyo masuala haya yalimalizwa kinyemela.

  Tatizo la Vijana wa kiume kulawitiwa ni kubwa sana pale Dar.
  Viongozi wa kulawiti ni watu wale wale tunao waheshimu.
  KWenda Wilayani kulipoti ni kama kupoteza muda wako tu. Kama jamii inabidi tuliweke wazi suala hili na kuanza kulikemea kwa nguvu.

  Ndiyo maana wabunge wakati fulani waliwahi taka kupitisha sheria ya kuwaenzi wasenge na mabasha pale Tanzania. Nasikia wabunge wetu pia miaongoni mwao wako waliochafuka na kunuka katika tabia hii ya kulawiti.
   
 11. D

  Darwin JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama waliolawitiwa ni watoto wa sekondari ningeifikiria hii post yako mara mbili.

  Mtoto wa darasa la tatu au la pili analolijua hapo ninini kama sio kulazimishwa?

  Kumbuka kwamba hata huko wanakokubali mambo haya ya kifirauni basi wana kiwango cha miaka. na mbali ya hayo wanaofanya wanapenda kwa muwasho wao na sio kulazimishana.

  Ukiangalia hii thread utakuta neno watoto wa darasa la pili na la tatu.

  Mtu anayefanya mapenzi na watoto wa darasa la pili au la tatu hatakama amefanya na wasichana basi akipatikana nikushitakiwa mara moja
   
 12. Lasthope

  Lasthope Senior Member

  #12
  Sep 4, 2008
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hili tatizo ni sugu sana siku hizi, sijui dunia inaelekea wapi jamani, wazazi mkumbuke hata kusali na kuwaombea watoto, siku hizi mambo hayaeleweki kabisa, tabia ingini iliyoanza kushamiri hasa kwa wazazi wanaoishi mabali na shule wasomazo watoto wao hasa wale wanaofatwa na school bus early in the morning na kurudishwa late home wanafanyiwa michezo mibaya na madereva au makonda wa hizo school buses, yani utakuta mtoto mdogo anaamshwa usiku usiku ajiandae kwenda shule,school bus ikifika anakuwa wa kwanza kuingia anfika nasinzia analazwa kwenye kiti na ky gel inafanya kazi yake bila shida. Be aware parents, kazi si kuzaa tu bali matunzo. Usidhani unampa mtoto elimu bora kwa kumpleka shule ya academy mbali na home in the name of good education, anakuwa wa kwanza kuingia kwenye gari na wa mwisho kurudishwa, you will be shocked of the outcome, may God help us.
   
 13. m

  mgirima Member

  #13
  Sep 4, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengi wanaofanya mchezo huo kwa watoto (wa kike na kiume) ni watu wenye pesa au ni viongozi. Wanaamini watoto hawana AIDS. Waalimu na hata wazazi wanakuwa waoga kuwaripoti kwani hakuna sheria yoyote itakayochukua mkondo wake. Kinachofanyika ni polisi kuwakutanisha na kukubaliana yaishe.

  Tafuta mwalimu wa S/Msingi akusimulie. Utatamani kulia!
   
Loading...