SI KWELI Ulaji wa matunda ni chanzo cha kuua Ini

SI KWELI Ulaji wa matunda ni chanzo cha kuua Ini

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Siku hizi huku mtandaoni naona kila mmoja amekuwa mtaalamu wa masuala ya afya, huyu anasema kula matunda yenye sukari eti ni chanzo cha kuua Ini, sijui anataka tule matunda yenye chumvi, JamiiCheck tafadhali mtupe uhalisia wa hili.

1759209780118.png

 
Tunachokijua
Ama hakika unaweza kuwa miongoni mwa wasiofahamu umuhimu wa kiungo hiki mwilini.

Tovuti ya CleverLand Clinic inafafanua kwa kina kuhusu Ini ambapo inaeleza kuwa ni kiungo muhimu kwa binadamu kilichopo tumboni ambacho hufanya kazi nyingi muhimu za mwili, ikiwemo kuchuja damu. Pia huchukuliwa kama tezi kwa sababu hutengeneza kemikali ambazo mwili unahitaji. Magonjwa fulani na mitindo ya maisha inaweza kuharibu ini, lakini kuna njia nyingi za kulilinda kiungo hiki muhimu.

Ini lina kazi nyingi, na baadhi na muhimu zaidi ni pamoja kusafisha sumu (vitu hatari) kutoka kwenye damu, kuondoa chembechembe nyekundu za damu zilizochakaa, kutengeneza nyongo ambayo husaidia mwili kumeng’enya chakula, kuvunja na kusindika protini, wanga na mafuta ili mwili uyatumie, kutengeneza vitu vinavyosaidia damu kuganda, kudhibiti kiwango cha damu mwilini, pamoja na kuhifadhi glukojeni (chanzo cha nishati) na vitamini kwa matumizi ya baadaye.

Ini kwa kiasi kikubwa hujilinda lenyewe, lakini kuna vyakula na vinywaji ambavyo vinaweza kulipa nguvu ya ziada na kusaidia kuzuia au kupambana na baadhi ya magonjwa ya ini.

Daktari Christina Lindenmeyer aliyebobea katika huduma kwa wagonjwa wenye maradhi sugu ya ini anaeleza kuwa “Ni miongoni mwa viungo vichache vinavyoweza kujijenga upya, Iwapo una maambukizi au jeraha kwenye ini, kuna uwezekano kwamba ukiishi kwa mtindo wa maisha wenye afya na kula vyakula sahihi, ini lako linaweza kujiponya lenyewe.”

Faifa za matunda kwenye afya ya ini.
Dkt. Lindenmeyer anaongeza anasema unaweza kudumisha ini lenye afya kwa kulipa virutubishi vinavyohitajika. Lishe ya Mediterranean inayozingatia ulaji wa matunda, protini isiyo na mafuta mengi na mboga za majani, ni mfumo mzuri wa kufuata ili kulilinda ini lako.

Matunda asili hutoa virutubisho na nyuzi za lishe kwa ini, ambavyo husaidia mmeng’enyo wa chakula, Aina zote za matunda asili kama tufaha (apple), ndizi, chungwa, pear, blueberries, raspberries, strawberries, zabibu, embe, parachichi na tikiti maji, na kadhalika

MedWay Hospitals inabainisha kuwa matunda jamii ya machungwa, mfano ndimu, chungwa, na chenza yana kiwango kikubwa cha vitamin C na vioksidishaji (Mchanganyiko unaolinda seli kutokana na uharibifu unaosababishwa na molekuli hatarishi zinazojulikana kama free radicals.) Matunda haya ni vyakula bora vinavyosaidia afya ya ini kwani husaidia kuondoa sumu mwilini, kupunguza uvimbe, na kuamsha uzalishaji wa (Maji yenye alkalini bile production) yanayosaidia mmeng’enyo wa chakula na kusafisha ini.

Pia parachichi yana utajiri wa glutathione, kioksidishaji chenye nguvu kinachosaidia ini kuondoa sumu hatari. Kama moja ya vyakula bora vinavyosaidia kuzuia mafuta kupita kiasi kwenye ini, parachichi pia hutoa mafuta yenye afya yanayopunguza uvimbe wa ini na kuboresha utendaji wake kwa ujumla.

Kwa upande wa nanasi ni tunda lenye viambata vya bromelain enzyme (vinavyosaidia mmeng’enyo wa chakula na kazi nyingine za mwili), Utafiti uliochapishwa katika tovuti ya Science Direct unaonesha kuwa bromelain inaweza kulinda ini na pia kusaidia kuutibu wakati umeharibika. Hii inatokana na uwezo wake wa kupunguza viwango vya enzymes, kuboresha muundo wa ini, kupunguza viashiria vya uharibifu wa seli kutokana na sumu, na kusaidia kudhibiti mafuta mwilini. Kwa ufupi, bromelain inaweza kusaidia ini kufanya kazi vizuri, bila kujali aina ya uharibifu ulioupata.

Vilevile inaelezwa kuwa mtindo wa maisha unachangia sana katika afya ya ini hivyo katika kuimarisha zaidi afya ya ini inashauriwa Kunywa maji vya kutosha ambapo husaidia kuondoa sumu mwilini, kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuupunguza mkusanyiko wa mafuta kwenye ini, kupunguza unywaji wa pombe kwani inaweza kulazimisha ini kufanya kazi nyingi na kusababisha uharibifu.

Epuka vyakula vilivyosindikwa kiwandani kwani mara nyingi vina mafuta yasiyo na afya na sukari zilizoongezwa na mwisho ni muhimu kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kufuatilia afya ya ini lako.

Mtindo wa maisha wenye uwiano, pamoja na vyakula bora kwa afya ya ini, unaweza kuongeza utendaji wa ini na ustawi wa jumla kwa kiasi kikubwa.​
Duuuh,saizi kila kitu ni sumu.

Basi tusiwe tunakula kabisa
 
Back
Top Bottom