juve2012
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 3,343
- 2,024
Monstgala nina swali.Umetumia muda mwingi kuelezea heavenly bodies.Ni somo zuri sana lakini kuna kitu kinausumbua moyo wangu.Tumeshuhudia majanga ya asili mbalimbali duniani yanayotokana na maumbile ya dunia yenyewe.Do we have any significant threat from these heavenly bodies?Kubadilika tabia ya maumbile na kuleta majanga ni jambo ambalo dunia imeshuhudia sana na kuathirika,tena katika siku za hivi karibuni inasemekana frequency ya kutokea majanga ya asili imeongezeka gradually kuliko zamani,vitu kama global warming na hivi karibuni wanasayansi wanadhani wamegundua global cooling,ni sehemu tu ya mambo yaonyeshayo kuwa as time goes on,something is not right with mother nature.Inabidi kuchunguza kila kitu ili kujiridhisha kwamba haya yanayotokea ni haya tu,au kuna makubwa yanajitengeneza chini kwa chini.So,vipi huko angani,ni salama au wanasayansi wameshaforesee matatizo siku za usoni?
Last edited by a moderator: