Ukweli usiopingika

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,948
Akiwa Darasa la Kwanza:
Mimi nikiwa mkubwa nataka niwe Daktari

Akiwa Form One:
Malengo yangu mimi nataka niwe Engineer

Akiwa Form Five:
Najiandaa kuwa Mwanasheria, nataka niwe na ofisi yangu mwenyewe niwe napiga hela kama Ronaldo

Akiwa mwaka wa kwanza Chuo:
Kwanza anaanza kujiona bonge ya mwanaharakati, fundi wa kukosoa ni yeye, fundi wa mipango ya migomo yeye,,,,,, akili yake inamwambia ambaye hajafika Chuo Kikuu ni MPUMBAVU TU,,,,,,, halafu utasikia nikimaliza chuo nitakuwa HR kwenye Ofisi fulani au nitakuwa Afisa Mahusiano Ofisi fulani yaani hawa wazee wazee nitawanyoosha hakuna rangi wataacha ona.

Mwaka wa kwanza Mtaani :
Jamani fans anayetaka wigi, raba, vijora, sendo za Kimasai, madela, lipstick, lotion ya kutoa madoa njoo inbox au nicheki DM au nitafute Whatsapp kwa namba hiyo na wale wa Mikoani tunapokea oda na tunatuma kwa haraka,,, lap yu ol!!! Na hapo hakuna hata kimoja chakwake, ukimuagiza na yeye anaenda kuomba ili japo apate hata buku ya udalali

Katika Maisha ukimuona mtu ana chumba chake mjini na kitanda na godoro anajilipia kodi mpe Shikamoo kabla hujamaliza chuo!!!

Life is not a rehearsal, it's a performance....
 
Umeongea kweli. Bila kusahau wale watoto wa mama ambao wanaish kwao, wanaishi kwa shemeji. Halafu kutwa kukosoa wenzao ambao wameshatoka nyumbani na kuanza kujitegemea.

Nawaasa kabla huja mkosoa mwenzio. Toka kwenu uka yaishi maisha mwenyewe bila kutegemea mtu.
 
Afanye yote kama baadae anaweza kutambua kukaa na kufanya biashara hapo angalau kuna watu wanakufa na cheti kabatini sababu amekosa kazi aliyosomea na hataki hata kuuza nguo au kufanya kazi yoyote kabisa anaona bora aombe mitahani
 
life is not a rehearsal, it's a performance.!! Na Mrisho Mpoto
 
life is not a reharsal it is a performance" msemo wa teacher wangu geography form two... umenikumbusha mbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…