Ukweli usemwe:Wanaume wanaposhindwa kuwajibika katika malezi, iweje lawama zielekezwe kwa wanawake?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
shutterstock_122640529.jpg

Malezi bora na timamu, yanapaswa kuwashirikisha wazazi wote wawili, yaani baba na mama. Wazazi hawa wanaposhirikiana katika kuwapa watoto wao malezi yenye taratibu njema za kimaadili, ni dhahiri kabisa kuwa, watakua na kuwa watu wazima wa kutegemewa na ambao watakuwa ni kielelezo cha kuigwa kwenye jamii yetu.

Lakini katika hali halisi, akina mama peke yao ndiyo wamekuwa wakiachiwa mzigo na majukumu yote ya kuwatunza na kuwalea watoto wao bila ushiriki wa kina baba. Na mara nyingi watoto hawa wanapogeuka na kuwa waasi na watukutu, lawama zote huwaendea akina mama. Ni jambo linaloudhi na kukatisha tamaa, tunapowaona akina baba wengi wakishindwa kuchukua na kuubeba wajibu wao kama ‘baba’ na viongozi wa familia ambao, watoto wao wanapswa kuiga mfano kutoka kwao.

Kwa kawaida, mtoto anakuwa ni jukumu la mama, hadi akiharibika au akinyookewa. Kama akinyookewa, baba hujifanya kwamba, yeye ndiye aliyehusika kumfanya mtoto awe hivyo, wakati hakuwa akijua alikuwa akisoma darasa la ngapi. Mtoto anapoharibika, baba huruka hatua nyingi akimlaumu mama kwamba, alimdekeza mtoto. Akina baba wengi wanaona kuwa, wajibu wa kuwatunza na kuwalea watoto wao, ni wa wake zao peke yao. Wao wanaona kwamba, wanao wajibu wa kutoa amri na kulaumu kuhusu malezi. Ni kama vile wao hawahusiki na watoto wao.

Hali hii ya kutojitambua na kutokubali kufanya marekebisho katika njia ya kufikiri na kutenda mambo na hasa yale yanayohusiana na watoto na familia kwa ujumla kwa upande wa wanaume walio wengi, imekuwa ikisababisha dhuluma dhidi ya wanawake wengi. Akina mama wengi pamoja na kukabiliwa na majukumu mengine ya uzalishaji mali, pia wamekuwa wakibebeshwa jukumu hili kubwa na zito la kuwatunza na kuwalea watoto wao, bila usaidizi kutoka kwa wanaume zao.

Jamii kwa upande mwingine imekuwa ikiwalaumu moja kwa moja akina mama kuwa, wamekuwa wakizembea na kuwadekeza watoto wao na kusahau kwamba, baba wa watoto hao wapo, lakini jamii haitaki kuwagusa wala kuwakemea……
 
Inanikumbusha way back in university kwenye somo moja la social animal behaviour... Ndo maana sishangai :smash:
Kwa hiyo unamaanisha kwamba binadamu wa kiume hana tofauti na mnyama si ndiyo....?

Naomba niwashirikishe wafuatao: cacico, ladyfurahia, Passion Lady, Asnam, Kipipi, King'asti, BADILI TABIA, Kaunga, Paloma, Madame B, MadameX, Blaki Womani, Preta, sweetlady, FirstLady1, Remmy, Chocs, Lady doctor, Binti.com, Lisa, Nivea, snowhite, Mamndenyi, gfsonwin, AshaDii, @FP, Nyamayao, Asprin, Bishanga, KakaKiiza, Jiwe Linaloishi, Kiranga, Nyani Ngabu, Bujibuji, Kipaji Halisi, Mr Rocky, Mungi, Erickb52, Don Mangi, Arushaone, Kaizer, Ruttashobolwa, LiverpoolFC, Babu DC Dark City, KOKUTONA, The secretary, watu8, Smile
 
katika maisha ya kila siku tunasema mwanamke kwanza (lady is first) hivyo nyumba ambayo imefanikiwa utaambiwa kuwa nyuma yake kuna mwanamke. pia tunaambiwa kuwa ukimuelimisha mwanamke utakuwa umeelimisha jamii nzima na kuna mwingine unasema mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. kutokana na hayo haiwezekani kutowalaumu wanawake kutokana na utukutu wa watoto au mtoto kwani hata wao hawajawahi kupinga misemo niliyoitaja hapo juu.
 
Ndio maana tukaambiwa kabla ya kuolewa au kuozesha watt wetu wa kike basi chunguza tabia ya mwanamme na uungwana wake. Si pochi yake tu matokeo yake ndo hayo.
Kuna midume mingine mingi siku hizi ni mzigo tu.

Mikuubwa lakini ovyooo!
 
Kwa hiyo unamaanisha kwamba binadamu wa kiume hana tofauti na mnyama si ndiyo....?
Mkuu Usisahau kwamba binadamu pia... Ndo maana scientific procedures nyingiii zinaanzia kwa wanyama wengine na kufuatiwa na mnyama binadamu
 
Mkuu Usisahau kwamba binadamu pia... Ndo maana scientific procedures nyingiii zinaanzia kwa wanyama wengine na kufuatiwa na mnyama binadamu

Kama ni hivyo kwa nini basi nasi tusitembee uchi?
Kumbuka pale katika bustani ya Eden baada ya wale wanadamu wa kwanza kula tunda lililokatazwa walijikuta wakiwa uchi ikabidi wajifunike kwa nyasi ili kujisitiri. Mkuu huoni kuna tofauti kubwa kati ya mnyama na binadamu?
 
Nimekusoma Mtambuzi,
anayelea ni wazazi ila pasipo msaada wa Mungu ni bure,
nimeona kwa macho yangu ya nyama familia ambazo zina ndoa imara na watoto wamekuwa mateja
nimeona tena familia duni sana na watoto wameimarika hadi unashangaa
nimeona watoto wetu tunaowashika kama yai wanavyoharibika na kushindwa hata kujitegemea,
so huu ni mchango wangu kwa leo,

Mzima lakini???
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru kwa mchango wako na kweli uliyonena yana ukweli mtupu...

Nitapita hapo kijiweni kwako mchana kasoro kuona uso wako...LOL
 
so hata wewe unapowalea akina Ngina inakubidi umweke Mungu mbele
usije jiona kuwa mko baba na mama ambao ni imara mkaona kila kitu kitakuwa sawa.

Kijiweni sitakuwepo muda fulani
but unicheki kwenye simu kwanza.

Nakubaliana nawe kwenye hili...mshirikishe mungu katika malezi ya watoto wako. Nijuavyo hakuna formula ya kulea, zipo guidelines lakini matokeo ni kubahatisha.

Pili kwa kawaida wanaume waliowengi ni wachache wenye mchango mkubwa nyumbani, nikimaanisha ushirikiano wa kihali. Kwa wanawake wenzangu ukishabeba majukumu wa mwanaume ujue ushaweka reference, maana mbele huweiz kataa na zaidi you will endup doing his task at home throughout.
 
MadameX sitaki kusema sana kwa kuwa mimi ni majeruhi wa hii kitu
nitakuwa naendelea kusoma michango yenu.

Nakubaliana nawe kwenye hili...mshirikishe mungu katika malezi ya watoto wako. Nijuavyo hakuna formula ya kulea, zipo guidelines lakini matokeo ni kubahatisha.

Pili kwa kawaida wanaume waliowengi ni wachache wenye mchango mkubwa nyumbani, nikimaanisha ushirikiano wa kihali. Kwa wanawake wenzangu ukishabeba majukumu wa mwanaume ujue ushaweka reference, maana mbele huweiz kataa na zaidi you will endup doing his task at home throughout.
 
Last edited by a moderator:
so hata wewe unapowalea akina Ngina inakubidi umweke Mungu mbele
usije jiona kuwa mko baba na mama ambao ni imara mkaona kila kitu kitakuwa sawa.

Kijiweni sitakuwepo muda fulani
but unicheki kwenye simu kwanza.
Nitakuwa hapo ICB Bank nikikamilisha taratibu zangu za kuchukua mkopo kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya madini...
Nikimaliza meeting nitaku col.....
 
Nakubaliana nawe kwenye hili...mshirikishe mungu katika malezi ya watoto wako. Nijuavyo hakuna formula ya kulea, zipo guidelines lakini matokeo ni kubahatisha.

Pili kwa kawaida wanaume waliowengi ni wachache wenye mchango mkubwa nyumbani, nikimaanisha ushirikiano wa kihali. Kwa wanawake wenzangu ukishabeba majukumu wa mwanaume ujue ushaweka reference, maana mbele huweiz kataa na zaidi you will endup doing his task at home throughout.
Duh! mama Ngina asije soma hii maneno, na wale wanoko kina King'asti, Asnam na Kipipi wasipite hapa...
 
Last edited by a moderator:
Kama ni hivyo kwa nini basi nasi
tusitembee uchi?
Kumbuka pale katika bustani ya Eden baada ya wale wanadamu wa kwanza kula tunda lililokatazwa walijikuta wakiwa uchi ikabidi wajifunike kwa nyasi ili kujisitiri. Mkuu huoni kuna tofauti kubwa kati ya mnyama na binadamu?
Mkuu tusitoke kwenye mada yetu ya malezi ya watoto na kurukia swala la ustaarabu na kujisitiri... Ebu mwangalie mkuu wa pori Panthera leo ama lion au simba dume anazalisha then anamwachia jike aendelee kutunza watoto yeye anachapa mwendo kutafuta another female lion on heat... Kumbuka atarudi next season huyo female lion akiwa heat achilia mbali mambo yatayotokea hapo kati kama kuua watoto wa kiume wote wasije wakamu out compete.... Hali ni ivyo ivyo kwa wanyama wengine kama yellow baboon.. Chacma baboon... Macaque monkey ambao wanahesabika kukaribiana uwezo wa kufikiri na wanyama binadamu... Mkuu Tafuta animal behaviour journals ujiridhishe na swala la malezi ya watoto...
 
Back
Top Bottom