mwananyaso
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,843
- 3,128
Hali inavyojionyesha ni kwamba chama kikuu cha upinzani nchini chadema kimeporomoka sana umaarufu wake.
Ni imani yangu kinafuata njia iliopitwa na NCCR Mageuzi, TLP na CUF.
Hili limetokana na uongozi mbovu ngazi ya kitaifa, uongozi usiokubali makosa na kushaurika, mengi yamesemwa na wadau juu ya namna bora ya kukijenga na kukiimarisha, lakini mawazo hayo yalipuuzwa, na watoa maoni kushambuliwa kwa matusi na dhihaka nyingi, hivyo kuamua kukaa kimya kama watazamaji.
Kama ilivyo ada, mwanasiasa au mwananchi mfuasi wa chama chochote cha siasa huwa na malengo, kwake binafsi, kwa jamii inayomzunguka na taifa lake kwa ujumla. Malengo hayo yasipokuwa na dalili ya kutimia hutafuta namna nyingine ya kuyafikia.
Inavyoonekana, Chadema ishiriki, isishiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020, itaporomoka sana tu na kupoteza nafasi ya chama kikuu cha upinzani nchini.
Na hapa asitafutwe mchawi nje ya chama hiki, mchawi yupo ndani ya chama chenyewe.
Kuna usemi wa wahenga usemao "Kila lenye mwanzo lina mwisho wake", "Asiyesikia la mkuu huvunjika guu" na "Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Iddi". Haya kufikia mwezi October yataanza kudhihirika wazi kabisa.
Nihitimishe kwa kusema chama kitakacho kuja mbadala wa Chadema, na hili halina mjadala, kitatakiwa kujifunza kupitia makosa haya, kama kweli kitakuwa na nia ya kuleta mabadiliko ya kiuongozi nchini. Hata ikibidi kujifunza namna bora ya kuendesha chama kwa kuiga CCM kinavyoendeshwa.
Nakaribisha maoni tofauti na yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app