Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,597
- 46,230
Nimesoma bandiko la mmoja wa member ninaowashimu sana humu JF akimzungumzia Zitto kwa 'Hisia' Hasi zaidi ningependa kumjibu yeye na wale wengine wanaomchukilia Zitto kwa hali hasi zaidi.
Kuhusu Zitto kujijenga zaidi mwenyewe.
Kila mwanasisia hupenda kujijenga yeye kwanza hivyo hiyo sio ishu ya maana,ishu ni anajijenga kwa namna gani,Zitto yeye ameamua kutumia uchambuzi makini wa uchumi,mipango na bajeti za serikali akitumia zaidi vizuri elimu yake na uzoefu wa kuiongoza kamati ya PA C kujenga hoja na kuikosoa serikali.
Kuhusu msimamo;Zitto anao msimamo,na kuthibitisha hilo huwezi kupata kauli au misimamo yake inayoonyesha kubadilika badilika kila mara,yuko consistent mpaka sasa,labda tusubiri huko mbeleni.
Kuhusu kununulika;Kununuliwa kwa Zitto ni propoganda dhaifu zisizo na uthibitisho wowote na zilizaliwa kutokana na ukaribu wake na JK na viongozi wengine wa CCM
Kuhusu safari yake kisiasa;Safari ya siasa kwa Zitto mpaka wakati huu ni excellent,ukiacha misuguano yake na Chadema(ambayo ni ya kawaida kabisa kutokea katika siasa),na kuthibitisha hilo amekuwa akishinda ubunge na chama alichokianzisha kinaipa Chadema changamoto mpya ya kujizatiti upya na kurekebisha makosa yake au kikubali kuona nafasi yake kama Chama pendwa nje ya ccm ikuchukuliwa na ACT.
Kwamba ACT ilitumika vibaya katika uchaguzi wa mwaka 2015 ni uongo wa mchana kweupe ukiangalia facts za mahesabu ya Kura,Mghwira wa ACT hakupata hata kura milioni 1 za urais hivyo hata kama Lowassa angezichukua hizo kura zote za ACT asengifika mahali,ushaidi unaonyesha UKAWA kushindwa kuachiana baadhi ya majimbo ndiko kulikochangia kushindwa ubunge kwa wagombea wake katika maeneo ambayo wangeshinda kirahisi mfano mzuri ni Segerea alikopoteza Mtatiro kwa kura chache kutokana na kugawana kura na mgombea wa Chadema.
Inawezekana usimpende au usizipinde aina ya siasa za Zitto zilozoelemea zaidi msimamo wa kati ,lakini huwezi kataa kwamba Zitto ni mmojawapo wa wanasiasa makini,mbobevu,anayejua kujenga hoja makini,anayejua wapi azungumze na wapi akae kimya kwa manufaa yake na taasisi aliyopo kwa wakati huo.
Tangu kuondoka kwa Tundu Lissu bungeni sauti ya Zitto bungeni ndio imekua ikichukua nafasi ya mbele katika safu ya upinzani kuonyesha madhaifu ya serikali kwa hoja makini iwe Korosho, ripoti ya CAG,SGR,Mbaazi n.k (haitoshi tu kuzungumza, mwanasisia makini ni yule anayejenga hoja, Zitto anajenga hoja).
Tumkosoe Zitto panapostahili,lakini tusimdogoshe, tuukubali ukweli kwamba yeye ni mojawapo ya 'political heavyweights' na mwanasiasa makini sana.
Angalizo:Natambua Zitto sio Malaika,lakini ni mzalendo.
Loyalty To country Alyways,To government When it deserves