Revocatus James Ngoja
Member
- Aug 15, 2023
- 7
- 7
UKWELI UNAOOGOPWA: Miaka 5 Baada ya Kifo cha John Pombe Magufuli je, Taifa Linajidanganya?
Sehemu ya 2 na Mwisho.
Kuna ukweli ambao wengi wanauogopa,na kuna ukimya ambao umejengwa kwa makusudi.
Jana nliandika Makala niliyoipa kichwa "Kati ya Ukweli na Ukimya, Miaka Mitano tangu kifo cha John Magufuli” ikiwa ni sehemu ya kwanza ya makala na Leo naomba kuendelea katika makala ya pili ambavyo ni hitimisho la tafakuri yangu kwa jamii na taifa.
Miaka mitano baada ya kifo cha John Pombe Magufuli, bado kuna maswali ambayo hayajajibiwa na pengine hayaruhusiwi kujibiwa.
1-Swali si kama tunamkumbuka.
Swali ni je tunamkumbuka kwa ukweli, au kwa simulizi tulizozoeshwa?
Taifa kati ya kumbukumbu na hofu tumejenga taswira mbili:
(a)Wapo wanaomuona Magufuli kama shujaa asiye na doa
(b)Wapo wanaomuona Magufuli kama kiongozi aliyebana uhuru ambapo mimi ni mmoja wao ijapo ukweli hauko kwenye pande hizi mbili,Bali ukweli uko katikati ya mahali ambapo hakuna anayependa kusimama.
Kwa nini?
✓Kwa sababu ukweli unahitaji ujasiri,na ujasiri ni kitu ambacho jamii nyingi hukiogopa.
Hebu fikiria kuhusu ukimya wa hatari kuliko kelele
Leo hii, hatuna kelele nyingi kuhusu Magufuli,lakini hiyo si ishara ya amani Bali ni ishara ya kitu kingine:
2-Ukimya.
✓Je hauoni ukimya wa wale wanaojua lakini hawasemi na wale wanaotaka kusema lakini wanaogopa?
✓Je hauoni ukimya pia wa wale wanaoona ni bora kusahau kuliko kukumbuka kwa maumivu?
Mdogo wenu nawakumbusha kwamba historia ina tabia moja hatari ikinyamazishwa, hurudi kwa nguvu zaidi.
3- Je, tunajifunza au tunasahau?
✓Taifa lisipojiuliza maswali magumu, hujirudia makosa yale yale ndiyo Maana tangu Jana na Leo ninawauliza maswali magumu ili mchague kujibu au kukaa kimya.
•Je, tumejifunza kuhusu nguvu ya mamlaka?
•Je, tumejifunza kuhusu mipaka ya uongozi?
•Je, tumejifunza kuhusu sauti ya wananchi?
Au tumefunika yote kwa jina la “kuendelea mbele”?
Kwa sababu hofu yangu ni kuwa ,Kuendelea mbele bila kuelewa ifaavyo kuhusu ya nyuma,ni kutembea gizani huku ukijifariji kuwa unaelekea kuliko na mwanga.
4- Je ukweli ambao hauhitaji ruhusa ni kiashirio kuwa kuna imani potofu kuwa ukweli unahitaji idhini?
Kwangu ni Hapana kwa sababu ;
√Ukweli hauhitaji kibali,ruhusa au muda maalum bali ukweli unahitaji watu wenye ujasiri wa kuuliza:
Kama ndivyo je ni kwa nini hatusemi yote?
✓Kizazi hiki kina jukumu moja kubwa:
Si kuabudu, wala si kubeza,bali kuhoji na Tena sio Kijiji tu bali kuhoji kwa heshima ujasiri na kwa dhamira ya kujifunza kwa sababu taifa lisilouliza maswali huandikiwa majibu na wengine.
Hitimisho: Ukimya si suluhisho tunaweza kuendelea kukaa kimya na tunaweza kuendelea kujenga simulizi zinazotufariji lakini ukweli mmoja utabaki kwamba Taifa lisilokabiliana na ukweli wake, hujenga mustakabali juu ya mchanga.
Swali langu la mwisho katika hitimisho la msururu huu wa tafakuri si kuhusu Magufuli bali swali ni hili:
✓Je, sisi kama taifa tuko tayari kusikia ukweli, hata kama unaumiza?
✓Wewe unaonaje? Je, tunamkumbuka kwa haki au tunaishi ndani ya simulizi iliyochaguliwa namna ya kuwasilishwa?
Nimetimiza wajibu wangu ,kazi ni yako kutoa maoni yako.
Ni Mimi
Revocatus James Ng'oja
Mwandishi huru, Mwanaharakati,Mwanasiasa na Mtetezi wa haki za binadamu.
Reha-Rombo-Kilimanjaro
18 March,2026.