UKWELI unaofichwa katika Ripoti ya Tume

UKWELI unaofichwa katika Ripoti ya Tume

Acheni watoto wa watu wapate haki yako kama kweli wamefelishwa,
 
Mkuu Vuta-Nkuvute heshima yako. Nakupongeza sana kwa kuleta uzi huu kwa sababu ni kweli kabisa Tume inao ukweli mwingi ilioamua kuuficha makusudi kwa lengo la kuficha ukweli kuhusu kiini cha tatizo hilo. Habari za uhakiki kutoka katika mmoja kati ya Tume ya Pinda aliyeoneshwa kushtushwa sana na uamuzi wa serikali anasema kuwa hawakuwa wamependekeza matokeo yafutwe kwa kuwa uamuzi wa kutumia utaratibu uliotumiwa na Baraza la Mitihani ulitolewa na Waziri wa Elimu.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo aliyeonekana kukerwa sana na taarifa iliyotangazwa bungeni amesema kuwa walipoenda NECTA wakati wa uchunguzi wao walijiridhisha kuwa alama za chini za ufaulu 21 hazijawahi kutumika NECTA na kwamba waliona alama halisi za watahiniwa na gredi walizopata kwa miaka mingi na kubaini kuwa alama zilizokuwa zinatumika zilikuwa kati ya 35-45 na kilichofanyika mwaka 2012 ni kuwa na kiwango cha chini kinachofanana kwa masomo yote na kilichotumika ilikuwa alama 35. "Unajua ndugu yaani jana baada yakusikia hiyo taarifa siakuamini kabisa masikio yangu kwa sababu maelekezo ya kutumia viwango maalum vya ufaulu yalitolewa na Waziri wa Elimu na Baraza likatakiwa kupeleka viwango ambavyo vilijadiliwa kwenye kikao chini ya uenyekiti wa Waziri Shukuru Kawambwa na hata Mwenyekiti wetu alikuwa mjumbe katika kikao cha kuamua utaratibu mpya ambao umebatilishwa na Baraza la Mawaziri". Kilisema chanzo hicho kwa masikitiko na kuapa kuwa atawasiliana na wajumbe wenzake kuona kama anaweza kupata kumbukumbu hizo ili watu wajionee ukweli. Anasema kuwa walikusanya nyaraka nyingi kutoka kila sehemu walipokuwa wanafanya utafiti na kwa kuwa hapakuwa na utaratibu mzuri wa kudhibiti nyaraka hizo tulikuwa tunaweza kuondoka nazo kwa hiyo hili jambo litafumka tu kwa sababu wajumbe wenyewe tulikuwa tumegawanyika sana. Mwenyekiti wetu ni mtu wa Waziri na alikuwa mara nyingi anasema kwenye vikao "hili nitashauriana na Waziri" kwa hiyo kwa ujumla waziri ndiye aliyekuwa anatoa maelekezo kwa Tume. Yaani ni mambo mengi ndugu yangu yaani Waziri alimwita Prof Allen Mushi wa Chuo kikuu na baada ya kuwa wamefanya majadiliano naye akaongea na mwenyekiti wetu wa Tume na akamtuma Prof huyo kwenda NECTA kufanya standardisation ya matokeo. Jambo hilo lilikuwa linafanywa kwa siri sana na Mwenyekiti na Makamu wake na sisi wajumbe wengine tulikuwa tunawekwa pembeni. Ninaamini kuwa alichosema Mh Lukuvi kinatokana na huo mchezo uliochezwa na Waziri kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake na lengo la maamuzi yote hayo ni umlinda Waziri wa Elimu kwani yeye ndiye chanzo cha sintofahamu hii.

Nimemsihi sana huyo ndugu yangu anipatie hizo minutes za kikao kilichofanya maamuzi hayo ili nizimwage hapa jamvini. Wakuu nitaendelea kuwapa update lakini nimeogapa sana alichonieleza huyo mjumbe na kama ni lweli Waziri Kawambwa lazima awajibike pamoja na Mwenyekiti wa Tume aliyeamua kuficha ukweli na kusababisha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi ambayo hakiki watayajutia majuto ya kitukuu pindi watakapoja ukweli. Ni movie ndeeeeeefu, ndiyo kwanza inaanza na Serikali sikivu itasikiliza haswaaaaaaa!

Kwa hakika tunayo safari ndefu sana
 
Kwa jina la siasa yote yanawezekana. Tunacompromise ubora kwa wingi ili tu kutengeneza picha nzuri ya kisiasa
 
Sawa. Inawezekana hicho walichokiona Tume kikawa ni miongoni mwa sababu. Lakini kurudia kusahihisha mtihani siyo solution. Nasema hivi kwa sababu kama Serikali inataka wanafunzi wafaulu, basi, wanaweza kufauliswa kwa kepewa alama wasizostahili. Ingekuwa bora kama wangetafutiwa mazingira mazuri halafi wakarudia mtihani huo mwaka huu. Mimi kama mzazi kama mtoto wangu akiambiwa arudie F2 itabidi nielezwe ni sera ipi ya elimu. Kama hatutaki kukaa chini na kutumia akili zetu kufikiri na badala yake tukawa tunakuwa-moved na tume na posho za vikao tutazidi kuiua elimu ya nchi hii. NECTA walitunga mtihani kulingana na muhtasari iliyopo. Sasa kosa lao ni nini? TIE walipobadili kutoka content to comptence-based curriculum hawakutoa mafunzo kwa walimu. Hilo ni kosa la NECTA? Leo hii wako walimu ukiwauliza Mhamo wa Ruwaza (competence- based) ni nini hawajui. So what are we trying to say here.

jambo jingine ni kuhusiana na Continous Assessment (CA). Walimu hawana muda katika hili. Kwa hiyo inasemekana alama zinazotumwa ni cooked. Zoezi moja tu linatosha kutoa mazoezi mengine kama kumi. Kwa hiyo ukweli ni kwamba wanafunzi hawafundishwi kufikiri na of late wamekuwa wanafundishwa kutegemea maswali ya mitihani kitu ambacho sisi tulifanya kama revision kwenye term ya pili ya F4. But not these days. Kwa kukosa walimu baadhi ya wanafunzi, hawaingii darasani ndiyo hao waliochora mazombie kwenye karatasi. Nashangaa sana Tume kuisulubu NECTA. Binafsi sikubaliani na hili kabisa. Bora hata ingekuwa TIE. Tukubaliane. Very few teachers wanafanya kazi zao kwa weledi. Lakini pengine kama TIE ingewaelekeza kuhusu hii aina ya mtaala isingekuwa hivyo. Mwulize mkanguzi wa elimu kanda ya Dar es Salaam. Alilalamika wakati majibu ya F2 yalipotoka kwa mtindo huu mpya lakini TIE walinyamaza kimya.
 
Amini nawaambia, hii yakusahihisha upya mitihani ya kidato cha nne, 2012 ni janja ya Serikali ya chama cha Mapinduzi kutaka kuwaridhisha Wamiliki wa Shule Binafsi ambao wamemwaga lawama za kutosha Serikalini kuwa watakosa ‘wateja’ kwenye shule zao kutokana na matokeo haya mabaya mno.

Afanye mtu utafiti mdogo kwa shule za binafsi zinazomilikiwa na watu binafsi (ukiacha zinazomilikiwa na taasisi za dini), asipokuwa zaidi ya 90% ni za makada wa CCM (tena wengi wenye vyeo serikalini) aje anikate shingo...
 
Mkuu Vuta-Nkuvute heshima yako.

Nakupongeza sana kwa kuleta uzi huu kwa sababu ni kweli kabisa Tume inao ukweli mwingi ilioamua kuuficha makusudi kwa lengo la kuficha ukweli kuhusu kiini cha tatizo hilo. Habari za uhakiki kutoka katika mmoja kati ya Tume ya Pinda aliyeoneshwa kushtushwa sana na uamuzi wa serikali anasema kuwa hawakuwa wamependekeza matokeo yafutwe kwa kuwa uamuzi wa kutumia utaratibu uliotumiwa na Baraza la Mitihani ulitolewa na Waziri wa Elimu.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo aliyeonekana kukerwa sana na taarifa iliyotangazwa bungeni amesema kuwa walipoenda NECTA wakati wa uchunguzi wao walijiridhisha kuwa alama za chini za ufaulu 21 hazijawahi kutumika NECTA na kwamba waliona alama halisi za watahiniwa na gredi walizopata kwa miaka mingi na kubaini kuwa alama zilizokuwa zinatumika zilikuwa kati ya 35-45 na kilichofanyika mwaka 2012 ni kuwa na kiwango cha chini kinachofanana kwa masomo yote na kilichotumika ilikuwa alama 35.

"Unajua ndugu yaani jana baada yakusikia hiyo taarifa siakuamini kabisa masikio yangu kwa sababu maelekezo ya kutumia viwango maalum vya ufaulu yalitolewa na Waziri wa Elimu na Baraza likatakiwa kupeleka viwango ambavyo vilijadiliwa kwenye kikao chini ya uenyekiti wa Waziri Shukuru Kawambwa na hata Mwenyekiti wetu alikuwa mjumbe katika kikao cha kuamua utaratibu mpya ambao umebatilishwa na Baraza la Mawaziri". Kilisema chanzo hicho kwa masikitiko na kuapa kuwa atawasiliana na wajumbe wenzake kuona kama anaweza kupata kumbukumbu hizo ili watu wajionee ukweli.

Anasema kuwa walikusanya nyaraka nyingi kutoka kila sehemu walipokuwa wanafanya utafiti na kwa kuwa hapakuwa na utaratibu mzuri wa kudhibiti nyaraka hizo tulikuwa tunaweza kuondoka nazo kwa hiyo hili jambo litafumka tu kwa sababu wajumbe wenyewe tulikuwa tumegawanyika sana. Mwenyekiti wetu ni mtu wa Waziri na alikuwa mara nyingi anasema kwenye vikao "hili nitashauriana na Waziri" kwa hiyo kwa ujumla waziri ndiye aliyekuwa anatoa maelekezo kwa Tume.

Yaani ni mambo mengi ndugu yangu yaani Waziri alimwita Prof Allen Mushi wa Chuo kikuu na baada ya kuwa wamefanya majadiliano naye akaongea na mwenyekiti wetu wa Tume na akamtuma Prof huyo kwenda NECTA kufanya standardisation ya matokeo. Jambo hilo lilikuwa linafanywa kwa siri sana na Mwenyekiti na Makamu wake na sisi wajumbe wengine tulikuwa tunawekwa pembeni. Ninaamini kuwa alichosema Mh Lukuvi kinatokana na huo mchezo uliochezwa na Waziri kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake na lengo la maamuzi yote hayo ni umlinda Waziri wa Elimu kwani yeye ndiye chanzo cha sintofahamu hii.

Nimemsihi sana huyo ndugu yangu anipatie hizo minutes za kikao kilichofanya maamuzi hayo ili nizimwage hapa jamvini. Wakuu nitaendelea kuwapa update lakini nimeogapa sana alichonieleza huyo mjumbe na kama ni lweli Waziri Kawambwa lazima awajibike pamoja na Mwenyekiti wa Tume aliyeamua kuficha ukweli na kusababisha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi ambayo hakiki watayajutia majuto ya kitukuu pindi watakapoja ukweli. Ni movie ndeeeeeefu, ndiyo kwanza inaanza na Serikali sikivu itasikiliza haswaaaaaaa!

mkuu cambri na vuta nikuvute mbarikiwe sana kwa utayariwenu kushare nasi kuhusu hujuma katika elimu.mwongo mpe muda.misumari ya hotuba ya waziri kivuli elimu itawachomaa balaaa
 
napingana na wewe sana,,nimefanikiwa kupitia mitihani ya taifa ya fizikia tokea miaka ya themanini hadi leo,,nilichogundua miaka hiyo mitihani ilikuwa so cheap yaani unaulizwa definition,calculation ambazo kiuhalisi ni simple na explanation katika maswali mengi,,for sure msijisifu sana eti elimu ya zamani ilikuwa bora,la hasha,,,sasa kuanzia 2011 mitaala ni mipya ambapo ukisoma muongozo wa wizara na necta unapima competence na sio content,hivyo basi hakuna kurudia maswali na mitihani hii ni bora kama mitihani ya scottish examining board kama ushawahi iona,,wanafunzi hawakuandaliwa kwa mfumo huu ndo maana tunapata shida,,na ukiangalia mitihani mingi ya fizikia iliyopita maswali yalijirudia ka ugomvi lakini ya sasa hivi ni bora,,so wazee msijisifu kwa content based exams,,,madogo wamejitahidi sana,,bravo jasper kajiru of feza boys huyu dogo kafanya vizuri mno,,,,, bravo necta
Umenielewa vibaya. Nikwamba leo badala ya kutoa jibu 1 + 1 = 2, wanafunzi wanatakiwa waendembele zaidi kwanini jibu ni 2 badala ya 3. Kilichopo nikwamba walimu wengi hawafahamu jinsi ya kuwafundisha wanafunzi kujieleza (competence) zaidi ya ku base kwenye content tu na madhara yake ni kwa wanafunzi kushindwa kujibu maswali kama inavyotakiwa. NECTA hawana makosa.
 
napingana na wewe sana,,nimefanikiwa kupitia mitihani ya taifa ya fizikia tokea miaka ya themanini hadi leo,,nilichogundua miaka hiyo mitihani ilikuwa so cheap yaani unaulizwa definition,calculation ambazo kiuhalisi ni simple na explanation katika maswali mengi,,for sure msijisifu sana eti elimu ya zamani ilikuwa bora,la hasha,,,sasa kuanzia 2011 mitaala ni mipya ambapo ukisoma muongozo wa wizara na necta unapima competence na sio content,hivyo basi hakuna kurudia maswali na mitihani hii ni bora kama mitihani ya scottish examining board kama ushawahi iona,,wanafunzi hawakuandaliwa kwa mfumo huu ndo maana tunapata shida,,na ukiangalia mitihani mingi ya fizikia iliyopita maswali yalijirudia ka ugomvi lakini ya sasa hivi ni bora,,so wazee msijisifu kwa content based exams,,,madogo wamejitahidi sana,,bravo jasper kajiru of feza boys huyu dogo kafanya vizuri mno,,,,, bravo necta
Kama huna content utakuwaje competence? Kaka yangu aliyesoma miaka ya 90 kuna baadhi ya mada kwenye somo la fizikia anazielewa vizuri na amakwambia swali fulani tuliulizwa kwenye mtihani. Waulize wanafunzi waliomaliza mwaka jana mada walizojifunza kwenye somo la fizikia uone ni wangapi watakutajia. Tunazungumzia matokeo ya watahiniwa wa kidato cha nne 2012 Tanzania na si watahiniwa wa Feza boys.
 
Wanakijua wanachofanya

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mleta mada we mwenyewe inaonekana ni mwepesi sana
 
Cambri

Wakuu, hayo ndiyo mawazo na ukweli ambao ulipaswa kuelezwa toka awali. Tatizo la watanzania wengi ni kuwa kila kitu tunaingiza siasa. Wakati matokeo hayo yalipotangazwa, wapumbavu wengine waliacha kufikiri na kutafakari ili kujua chanzo cha matokeo hayo na mapendekezo yake. Kwa sasa akina mchome wametufungua macho ndo wadau wengine wanaanza kufunguka.

Watanzania tuwe na utamaduni wa kutafakari mambo na si kuyatumia matatizo ya nchi hii kama mtaji wa kisiasa

Ndo wanafunzi wamefundishwa kuchoraa Mazombie na Messi katika hiyo mitaala? Watu wamefeli wamefeli tu huwezi kuwa bize na visimu kila mda na headphone masikion badala ya sasa unaandika XAXA school unaandika XUL alafu useme eti utafaulu. Hawa hata tukiwapa mtihan ule ule watafel kwa kiwango kile kile. Zero ni extreme bwama maana inahitaji upate only one C kuepuka zero yaan hata kiswahili umeshindwa wewe unakuja kutetea ujinga hapa kwa kutuambia mambo ya Scotland? Bullshit
 
Last edited by a moderator:
Itakuaje kwa wale waliojiua kutokana na matokeo haya?!

Ni uzembe tu kila mahali.

Ngoja tusubiri division one za kumwaga wakisahihisha upya, na kama kawaida yetu tutashangilia kama mazuzu!!

Mkuu, baada ya hapo angalia, Mwenyezi Mungu akikuweka hai miaka sita ijayo uone wahitimu wa University watakavyokuwa wachahe kupindukia, kwani wengi wata-disko.
 
Ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu,Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 iko hadharani.

Jana ilisomwa Bungeni Dodoma. Tume hiyo iliyokuwa inaongozwa na Prof. Sifuni Ernest Mchome,iliainisha sababu za matokeo mabaya ya kidato cha nne na kupendekeza cha kufanywa.

Kati ya vilivyopendekezwa,nikusahihishwa/kupitiwa upya kwa mitihani ya watahiniwa wote wa kidato cha nne wa mwaka jana. Serikali ikaonekena kushabikia pendekezo hili la Tume ya Prof.Mchome. Ikasahau kujiuliza maswali muhimu na kujiridhisha na uchunguzi makini uliofanywa na Tume ya Prof. Mchome.
Matokeo mabaya ya Kidato cha Nne wa mwaka jana yasingeweza kuepukika. Zipo sababu ambazo ima zimefichwa au hazikugunduliwa na Tume ya Waziri Mkuu Pinda. Sababu hizi ndizo hasa zilizopelekea ubaya wa matokeo haya.

Kwanza, darasa husika halikuwa zuri tangu mwanzo. Watahiniwa wa Kidato cha Nne wa 2012 ni wale waliomaliza darasa la saba mwaka 2008. Wakati darasa la saba la mwaka 2007 walikuwa na wastani wa ufaulu kitaifa wa asilimia 53 ambayo ni sawa na daraja C,darasa la saba la mwaka 2008(kidato cha nne 2012) walifaulu kwa wastani wa asilimia 45.

Niseme tu kuwa darasa hili halikuwa zuri kimasomo.
Katika kuthibitisha hilo,wapo wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012 na kushindwa mtihani.

Wanafunzi hao sasa wanajisomea Masomo ya Maarifa ( QT) katika vituo mbalimbali hapa nchini kikiwemo cha Shule ya Sekondari ya Mzumbe. Kiukweli,wanafunzi hao hawaoneshi kuwa waliwahi kusoma sekondari. Wanapelekeshwa hata na walioishia darasa la saba. Hapo mnasemaje waungwana?
Pili,darasa la 2012 halikuwahi kuchujwa katika mitihani ya kidato cha pili waliyoifanya mwaka 2010.

Wote, waliofaulu na walioshindwa,waliendelea na Kidato cha Tatu mwaka 2011. Hawa waliopaswa kuchujwa na kurudia mitihani yao, waliathiri kwa kiasi kikubwa matokeo ya mwaka 2012. Ndio waliohanikiza madaraja ya sifuri na la nne.
Tatu, Baraza la Mitihani la Tafa lilibadili matumizi ya Alama za Maendeleo ya Mwanafunzi Shuleni (Continuous Assessment). Kabla ya mwaka 2012, CS zilitumika kama asilimia 50 ya matokeo ya mwisho.

Yaani, mtihani wa mwisho ulisahihishwa na kukokotolewa kwa asilimia 50 na hivyo kufanya asilimia 100 ukichanganywa na CS. Kwa maana hiyo,mwanafunzi ambaye katika somo Fulani alipata CS ya 21 na kuendelea alikuwa na uhakika wa alama D na kuendelea katika matokeo yake ya mwisho.
Hii,yasemwa na Wahusika wa NECTA, ilifanya Shule nyingi kuwa ‘zinapika’ CS za wanafunzi wao na hivyo kunogesha matokeo ya wanafunzi hao na shule zao kwa ujumla. Mwaka huu, CS zote zilichukuliwa kama daraja F(yaani chini ya 21) na hivyo mwanafunzi kubaki na mtihani wa mwisho tu kama mkombozi wake.

Hii nayo ikaleta matokeo haya mapya ya kidato cha nne-2012.
Hoja ya kuwa zilitumika alama mpya kupata madaraja A,B,C,D, na F, haina mshiko sana. Hii ni kwakuwa,hata pale zilipotumika alama za zamani matokeo hayakuwa mazuri. Taarifa rasmi toka kwa wasahihishaji zinatoa mfano wa somo la Kiingereza ambalo baada ya kusahihishwaTanzania nzima,ni mwanafunzi mmoja tu wa Shule ya Sekondari ya Ilboru aliyepata alama za daraja A. Amini nawaambia, hii yakusahihisha upya mitihani ya kidato cha nne, 2012 ni janja ya Serikali ya chama cha Mapinduzi kutaka kuwaridhisha Wamiliki wa Shule Binafsi ambao wamemwaga lawama za kutosha Serikalini kuwa watakosa ‘wateja’ kwenye shule zao kutokana na matokeo haya mabaya mno. Pia, ni kutaka kurekebisha makosa ya kimawasilino kati ya Wizara ya Elimu, Taasisi ya Elimu na Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA). Kukosekana huko kwa mawasiliano na maelewano ndiko kulikosababisha kutungwa mitihani kinyume na ‘mitaala’,kutochujwa kwa wanafunzi walioshindwa kidato cha pili, kutotumika kwa CS kama ilivyozoeleka na kadhalika. Kiujumla,Waziri wa Elimu, Katibu Mkuu wa NECTA na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania hawawezi kukwepa mzigo huu wa fedheha kwa Taifa.

Huo ndio ukweli.

VUTA-NKUVUTE
aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)

Scaning for viruses..
 
kuna vitu CCM wanafanya masihara sasa kama kweli wamaeamua kuchezea elimu na kulizaimisha serikali kufanya cheating kwenye mitihani hili taifa linaangamia, wataalamu watatoka wapi? tutakuwa taifa jinga.
 
Wale waliojiuwa watafufuliwa na maombi ya ccm, maana ufaulu sikuhizi unapimwa na juhudi binafsi na marks za upendeleo za CONTINUOUS ASSESSMENT na wala si weledi

Nilimsikia yule mnadhimu wa ccm jana nikajua kweli wamelaaniwa! Eti wataangalia juhudi za mwanafunzi na kustandardize ili kuboresha matokeo ya form 4!? Ngoja tuone!
Wazazi wanasubiri kufanya sherehe za ufaulu (walizoahirisha baada ya matokeo) wa watoto wao!

Ama kweli, "Ujinga ni kipaji"
 
Tuombe mungu atupe uzima lakini hili jambo limeficha siri kubwa. Tume imependekeza katika matokeo mapya Division I zisiwe chini ya 4,000, II ziwe angalau 9000 na III zisipungue 30,000. Sasa cha kushangaza hivi walitumwa kuandaa matokeo mapya na kuja na mapendekezo kabisa ya idadi ya wanaotakiwa kufaulu kwa kila somo? Kawambwa alikuwa anahaha sana kuwasiliana na mwenyekiti na huenda aliwapa pipi baadhi ya wajumbe ili wahakikishe wanasukumia lawama Baraza. Mara nyingi Mchome alikuwa anawaambia wajumbe kwenye vikao vya tume "hili suala tuliache kwanza nitaongea na Waziri atupe mwelekeo". Hata hivyo mwelekeo aliwapa Kawambwa sasa unataka kuwatumbukia nyongo baada ya ukweli kuanza kujulikana.

Tusubiri waendelee kujikanyaga maana limekorogeka kisawasawa
 
Back
Top Bottom