UKWELI unaofichwa katika Ripoti ya Tume

UKWELI unaofichwa katika Ripoti ya Tume

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu,Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda kuchunguza matokeo mabaya ya Kidato cha Nne ya mwaka 2012 iko hadharani.

Jana ilisomwa Bungeni Dodoma. Tume hiyo iliyokuwa inaongozwa na Prof. Sifuni Ernest Mchome,iliainisha sababu za matokeo mabaya ya kidato cha nne na kupendekeza cha kufanywa.

Kati ya vilivyopendekezwa,nikusahihishwa/kupitiwa upya kwa mitihani ya watahiniwa wote wa kidato cha nne wa mwaka jana. Serikali ikaonekena kushabikia pendekezo hili la Tume ya Prof.Mchome. Ikasahau kujiuliza maswali muhimu na kujiridhisha na uchunguzi makini uliofanywa na Tume ya Prof. Mchome.
Matokeo mabaya ya Kidato cha Nne wa mwaka jana yasingeweza kuepukika. Zipo sababu ambazo ima zimefichwa au hazikugunduliwa na Tume ya Waziri Mkuu Pinda. Sababu hizi ndizo hasa zilizopelekea ubaya wa matokeo haya.

Kwanza, darasa husika halikuwa zuri tangu mwanzo. Watahiniwa wa Kidato cha Nne wa 2012 ni wale waliomaliza darasa la saba mwaka 2008. Wakati darasa la saba la mwaka 2007 walikuwa na wastani wa ufaulu kitaifa wa asilimia 53 ambayo ni sawa na daraja C,darasa la saba la mwaka 2008(kidato cha nne 2012) walifaulu kwa wastani wa asilimia 45.

Niseme tu kuwa darasa hili halikuwa zuri kimasomo.
Katika kuthibitisha hilo,wapo wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012 na kushindwa mtihani.

Wanafunzi hao sasa wanajisomea Masomo ya Maarifa ( QT) katika vituo mbalimbali hapa nchini kikiwemo cha Shule ya Sekondari ya Mzumbe. Kiukweli,wanafunzi hao hawaoneshi kuwa waliwahi kusoma sekondari. Wanapelekeshwa hata na walioishia darasa la saba. Hapo mnasemaje waungwana?
Pili,darasa la 2012 halikuwahi kuchujwa katika mitihani ya kidato cha pili waliyoifanya mwaka 2010.

Wote, waliofaulu na walioshindwa,waliendelea na Kidato cha Tatu mwaka 2011. Hawa waliopaswa kuchujwa na kurudia mitihani yao, waliathiri kwa kiasi kikubwa matokeo ya mwaka 2012. Ndio waliohanikiza madaraja ya sifuri na la nne.
Tatu, Baraza la Mitihani la Tafa lilibadili matumizi ya Alama za Maendeleo ya Mwanafunzi Shuleni (Continuous Assessment). Kabla ya mwaka 2012, CS zilitumika kama asilimia 50 ya matokeo ya mwisho.

Yaani, mtihani wa mwisho ulisahihishwa na kukokotolewa kwa asilimia 50 na hivyo kufanya asilimia 100 ukichanganywa na CS. Kwa maana hiyo,mwanafunzi ambaye katika somo Fulani alipata CS ya 21 na kuendelea alikuwa na uhakika wa alama D na kuendelea katika matokeo yake ya mwisho.
Hii,yasemwa na Wahusika wa NECTA, ilifanya Shule nyingi kuwa ‘zinapika' CS za wanafunzi wao na hivyo kunogesha matokeo ya wanafunzi hao na shule zao kwa ujumla. Mwaka huu, CS zote zilichukuliwa kama daraja F(yaani chini ya 21) na hivyo mwanafunzi kubaki na mtihani wa mwisho tu kama mkombozi wake.

Hii nayo ikaleta matokeo haya mapya ya kidato cha nne-2012.
Hoja ya kuwa zilitumika alama mpya kupata madaraja A,B,C,D, na F, haina mshiko sana. Hii ni kwakuwa,hata pale zilipotumika alama za zamani matokeo hayakuwa mazuri. Taarifa rasmi toka kwa wasahihishaji zinatoa mfano wa somo la Kiingereza ambalo baada ya kusahihishwaTanzania nzima,ni mwanafunzi mmoja tu wa Shule ya Sekondari ya Ilboru aliyepata alama za daraja A. Amini nawaambia, hii yakusahihisha upya mitihani ya kidato cha nne, 2012 ni janja ya Serikali ya chama cha Mapinduzi kutaka kuwaridhisha Wamiliki wa Shule Binafsi ambao wamemwaga lawama za kutosha Serikalini kuwa watakosa ‘wateja' kwenye shule zao kutokana na matokeo haya mabaya mno. Pia, ni kutaka kurekebisha makosa ya kimawasilino kati ya Wizara ya Elimu, Taasisi ya Elimu na Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA). Kukosekana huko kwa mawasiliano na maelewano ndiko kulikosababisha kutungwa mitihani kinyume na ‘mitaala',kutochujwa kwa wanafunzi walioshindwa kidato cha pili, kutotumika kwa CS kama ilivyozoeleka na kadhalika. Kiujumla,Waziri wa Elimu, Katibu Mkuu wa NECTA na Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania hawawezi kukwepa mzigo huu wa fedheha kwa Taifa.

Huo ndio ukweli.

VUTA-NKUVUTE
aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam (sasa Dodoma)
 
kweli kwa staili hiyo kikwete anataka kupata kula si uchaguzi umekaribia! Ila hapo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
 
Kiukweli siku hizi wanafunzi wa sekondari hawana sifa za kuwepo sekondari, wengi wamesombwa tu toka shule za misingi hawajui kuandika vizuri, kuhesabu na hata kusoma vizuri! Ccm wameingiza siasa kwenye elimu!
 
Itakuaje kwa wale waliojiua kutokana na matokeo haya?!

Ni uzembe tu kila mahali.

Ngoja tusubiri division one za kumwaga wakisahihisha upya, na kama kawaida yetu tutashangilia kama mazuzu!!
 
Kwa uandishi huo sijui kama ninaweza soma na kuelewa huo unaoitwa upotoshaji kwenye ripoti, any way kwa maslahi ya nchi yangu nitarudi baadaye.
 
Hakuna raha kama kusahihisha somo la Hisabati, Kingereza, Fizikia, Chemia na Biolojia, kwasbabu wanafunzi wa kileo hakuna wanachojibu zaidi ya kuandika namba ya swali na kurudia kuandika swali kama lilivyo kwenye karatasi ya maswali.
 
Taifa lisilo na elimu thabit ni taifa goigoi, tegemezi na ni taifa la kuibiwa na kudanganyika wakati wote
 
Mkuu Vuta-Nkuvute heshima yako.

Nakupongeza sana kwa kuleta uzi huu kwa sababu ni kweli kabisa Tume inao ukweli mwingi ilioamua kuuficha makusudi kwa lengo la kuficha ukweli kuhusu kiini cha tatizo hilo. Habari za uhakiki kutoka katika mmoja kati ya Tume ya Pinda aliyeoneshwa kushtushwa sana na uamuzi wa serikali anasema kuwa hawakuwa wamependekeza matokeo yafutwe kwa kuwa uamuzi wa kutumia utaratibu uliotumiwa na Baraza la Mitihani ulitolewa na Waziri wa Elimu.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo aliyeonekana kukerwa sana na taarifa iliyotangazwa bungeni amesema kuwa walipoenda NECTA wakati wa uchunguzi wao walijiridhisha kuwa alama za chini za ufaulu 21 hazijawahi kutumika NECTA na kwamba waliona alama halisi za watahiniwa na gredi walizopata kwa miaka mingi na kubaini kuwa alama zilizokuwa zinatumika zilikuwa kati ya 35-45 na kilichofanyika mwaka 2012 ni kuwa na kiwango cha chini kinachofanana kwa masomo yote na kilichotumika ilikuwa alama 35.

"Unajua ndugu yaani jana baada yakusikia hiyo taarifa siakuamini kabisa masikio yangu kwa sababu maelekezo ya kutumia viwango maalum vya ufaulu yalitolewa na Waziri wa Elimu na Baraza likatakiwa kupeleka viwango ambavyo vilijadiliwa kwenye kikao chini ya uenyekiti wa Waziri Shukuru Kawambwa na hata Mwenyekiti wetu alikuwa mjumbe katika kikao cha kuamua utaratibu mpya ambao umebatilishwa na Baraza la Mawaziri". Kilisema chanzo hicho kwa masikitiko na kuapa kuwa atawasiliana na wajumbe wenzake kuona kama anaweza kupata kumbukumbu hizo ili watu wajionee ukweli.

Anasema kuwa walikusanya nyaraka nyingi kutoka kila sehemu walipokuwa wanafanya utafiti na kwa kuwa hapakuwa na utaratibu mzuri wa kudhibiti nyaraka hizo tulikuwa tunaweza kuondoka nazo kwa hiyo hili jambo litafumka tu kwa sababu wajumbe wenyewe tulikuwa tumegawanyika sana. Mwenyekiti wetu ni mtu wa Waziri na alikuwa mara nyingi anasema kwenye vikao "hili nitashauriana na Waziri" kwa hiyo kwa ujumla waziri ndiye aliyekuwa anatoa maelekezo kwa Tume.

Yaani ni mambo mengi ndugu yangu yaani Waziri alimwita Prof Allen Mushi wa Chuo kikuu na baada ya kuwa wamefanya majadiliano naye akaongea na mwenyekiti wetu wa Tume na akamtuma Prof huyo kwenda NECTA kufanya standardisation ya matokeo. Jambo hilo lilikuwa linafanywa kwa siri sana na Mwenyekiti na Makamu wake na sisi wajumbe wengine tulikuwa tunawekwa pembeni. Ninaamini kuwa alichosema Mh Lukuvi kinatokana na huo mchezo uliochezwa na Waziri kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake na lengo la maamuzi yote hayo ni umlinda Waziri wa Elimu kwani yeye ndiye chanzo cha sintofahamu hii.

Nimemsihi sana huyo ndugu yangu anipatie hizo minutes za kikao kilichofanya maamuzi hayo ili nizimwage hapa jamvini. Wakuu nitaendelea kuwapa update lakini nimeogapa sana alichonieleza huyo mjumbe na kama ni lweli Waziri Kawambwa lazima awajibike pamoja na Mwenyekiti wa Tume aliyeamua kuficha ukweli na kusababisha Baraza la Mawaziri kufanya maamuzi ambayo hakiki watayajutia majuto ya kitukuu pindi watakapoja ukweli. Ni movie ndeeeeeefu, ndiyo kwanza inaanza na Serikali sikivu itasikiliza haswaaaaaaa!
 
wameamua kuwapa faraja walio feli. huku ni kujidanganya wenyewe.
 
Itakuaje kwa wale waliojiua kuyokana na matokeo haya?!

Ni uzembe tu kila mahali.

Ngoja tusubiri division one za kumwaga wakisahihisha upya, na kama kawaida yetu tutashangilia kama mazuzu!!
Wale waliojiuwa watafufuliwa na maombi ya ccm, maana ufaulu sikuhizi unapimwa na juhudi binafsi na marks za upendeleo za CONTINUOUS ASSESSMENT na wala si weledi
 
hakika hii nchi ina maajabu sana haiwezekani watu wenye nyazifa wakakumbatia mambo kama haya na kuacha elimu yetu ina angamia kisa kuwafurahisha walio feli na kujaribu kulindana na kwakweli haingii akilini waziri kutokuwa na taarifa kuhusu kupanda kwa marks au kushuka.

Tatizo ni siasa kuingizwa hadi kwenye mambo ya msingi kama elimu.
 
Duh Tanzania ina mambo ya ajabu sana, Elimu ambayo ni tegemeo la nchi zote zilizoendelea inachezewa kiasi hicho. Maamuzi ya mabadiliko yoyote katika system inapitishwa na baraza la mawaziri, inapokuja kuleta matokeo yasiyotegemewa baraza linayakataa na kubatilisha maamuzi yake yenyewe. Hii inaonehsa kuwa Baraza la Mawaziri lipo weak, na linaharibu katika mambo mengi sana.
 
Tupa Tupa iwekee paragraph andiko lako ili lisomeke vizuri.
 
Hakuna raha kama kusahihisha somo la Hisabati, Kingereza, Fizikia, Chemia na Biolojia, kwasbabu wanafunzi wa kileo hakuna wanachojibu zaidi ya kuandika namba ya swali na kurudia kuandika swali kama lilivyo kwenye karatasi ya maswali.

napingana na wewe sana,,nimefanikiwa kupitia mitihani ya taifa ya fizikia tokea miaka ya themanini hadi leo,,nilichogundua miaka hiyo mitihani ilikuwa so cheap yaani unaulizwa definition,calculation ambazo kiuhalisi ni simple na explanation katika maswali mengi,,for sure msijisifu sana eti elimu ya zamani ilikuwa bora,la hasha,,,sasa kuanzia 2011 mitaala ni mipya ambapo ukisoma muongozo wa wizara na necta unapima competence na sio content,hivyo basi hakuna kurudia maswali na mitihani hii ni bora kama mitihani ya scottish examining board kama ushawahi iona,,wanafunzi hawakuandaliwa kwa mfumo huu ndo maana tunapata shida,,na ukiangalia mitihani mingi ya fizikia iliyopita maswali yalijirudia ka ugomvi lakini ya sasa hivi ni bora,,so wazee msijisifu kwa content based exams,,,madogo wamejitahidi sana,,bravo jasper kajiru of feza boys huyu dogo kafanya vizuri mno,,,,, bravo necta
 
Cambri

Wakuu, hayo ndiyo mawazo na ukweli ambao ulipaswa kuelezwa toka awali. Tatizo la watanzania wengi ni kuwa kila kitu tunaingiza siasa. Wakati matokeo hayo yalipotangazwa, wapumbavu wengine waliacha kufikiri na kutafakari ili kujua chanzo cha matokeo hayo na mapendekezo yake. Kwa sasa akina mchome wametufungua macho ndo wadau wengine wanaanza kufunguka.

Watanzania tuwe na utamaduni wa kutafakari mambo na si kuyatumia matatizo ya nchi hii kama mtaji wa kisiasa
 
Last edited by a moderator:
Haya mambo ya zima moto ya ajabu sana, sasa ukilazimisha kuwapa madaraja ya juu at this level, vipi matokeo yao watakapomaliza form six, ama ndo utakuwa mchezo wa kuunda tume ili wajinga tuendelee kuliwa kodi zetu?

Serikali inaposhabikia kusahihisha upya ina uhakika gani hawa vijana watafanya vizuri A level?

Tunaongozwa na wahuni ambao kwa makusudi kabisa wameamua kutengeneza taifa la wajinga.
 
Dah kweli hili shamba la bibi limemshinda baba miraji sasa linaenda litakavyo kwa maana hiyo hamna aliyefaulu wala kufeli wanasubiri matokeo kama vile hayajatoka? Na form v itakuwa hamna kwa mwaka huu au waliofaulu wataenda shule?
 
Back
Top Bottom